Mnaonaje Baraza hili jipya la Mawaziri linalotarajiwa?

Wakuu wana JF,naomba tumsaidie Rais Juu ya nani abaki na nani aondolewe na nani abadishiwe wiraza kwenye baraza jipya linalotarajiwa soon:

mawazo yangu:
1.Ngeleja na Malima OUT,wametusababishia madeni makubwa yakiwemo DOWANS
2.Nundu na Naibu wake wabadilishiwe wizara,cant work together kila sikumigogoro
3.Ciril na Nyalandu watenganishwe,na kama nafasi mpya ni chache Nyalandu OUT
4. waziri wa afya abadilishiwe wizara,ya afya imemshinda ila kwa kuwa bado ni kijana mdogo with limited experience apelekwe wizara ndogo ndogo kama ile ya Simba.
5.Sophia Simba OUT-> none existent
6. Mwakyembe na Magufuli should be separated,kila mmoja awe waziri kamili.
7. Kabaka OUT none existent
8. Magembe abaki na wizara yake
9. Mali asili na Utalii OUT
10.Pinda abakie waziri mkuu. SIO FISADI.
11.MKULO OUT ameshindwa kuthibiti matumizi ya dollar nchini.
12.

endeleeni wadau

Hiyo na. 10 nitamshangaa sana kama Pinda hajaomba kupumzika! Kufanywa kote kama mtoto then bado awe na hamu na uwaziri wa jk-ni utaahira!
 
Wana jamvi,

katika gazeti la Mtanzania la leo kuna habari inayosema kamati kuu ya CCM inakutana leo saa 4 IKULU kujadili mambo mbalimbali ikiwemo kupokea mapendekezo ya party caucus ya kutaka mawaziri 8 kujiuzulu.

Inasemekana kwamba CCM inafanya haraka kubadili BLM ili kuipokonya CHADEMA ajenda yake ya OPERESHENI UWAJIBIKAJI.

Sehemu iliyonivutia katika habari hii ni pale chanzo hicho kilichotaja majina ya mawaziri wanaotarajiwa kuchukua nafasi zitazoachwa wazi kuwa ni:

-GODFREY ZAMBI
-ABDALLAH KIGODA
-KHAMIS KIGWANGALLA
-FAUSTINE NDUGULILE
-CHARLES TIZEBA
-JANUARY MAKAMBA
-STEPHEN MASELE

Wana jamvi, mnawaonaje mawaziri wetu hawa wapya watarajiwa?

HUyu malarushwa na eyey yumo? Kweli magamba wameishiwa!
 
Tizeba aligombea ubunge akijua kuwa atateuliwa. Hakuteuliwa lakini ameanza kutajwa basi hapa naona kama ataukwaa. Ila akiukwaa tutakuwa tunarudi kulekule kwa kujuana.
 
Hapa wamesahau swahiba wa kiranya mkuu SAID RAMADHANI BWANAMDOGO
Mkuu naye huyu aligombea akijua anapata nafasi baada ya yule wa zamani nadhani maneno kuonekana hawezi kuteuliwa. Jamaa akaacha ukuu wa wilaya akaingiza timu akashinda lakini haku appear kwenye Cabinet. This time inaweza kuwa wasaa wake.
 
binafsi kwa serikali ya kikwete kubadili mawazili ni kubadili tu watu wakula pesa za walipa kodi no new kwa vile naona yaya ndi tatizo anashindwa kuwa na sauti dhidi wa anaowateua, zambi nae hana jipya jimbo lake la mbozi mashariki limemshinda uwaziri ni mzigo kwake
 
Wana jamvi,

katika gazeti la Mtanzania la leo kuna habari inayosema kamati kuu ya CCM inakutana leo saa 4 IKULU kujadili mambo mbalimbali ikiwemo kupokea mapendekezo ya party caucus ya kutaka mawaziri 8 kujiuzulu.

Inasemekana kwamba CCM inafanya haraka kubadili BLM ili kuipokonya CHADEMA ajenda yake ya OPERESHENI UWAJIBIKAJI.

Sehemu iliyonivutia katika habari hii ni pale chanzo hicho kilichotaja majina ya mawaziri wanaotarajiwa kuchukua nafasi zitazoachwa wazi kuwa ni:

-GODFREY ZAMBI
-ABDALLAH KIGODA
-KHAMIS KIGWANGALLA
-FAUSTINE NDUGULILE
-CHARLES TIZEBA
-JANUARY MAKAMBA
-STEPHEN MASELE

Wana jamvi, mnawaonaje mawaziri wetu hawa wapya watarajiwa?

Kwa mtazamo wangu wanabadilishana vijiti tu hao,sasa ni zamu ya kula watu wengine......daaaah inauma sana,watz tunasikitisha sana.
 
wale maswaiba wake wa karibu wakula inatosha sasa atafute heshima mwishoni awaweke wawajibikaji aina magufuli
 
ni vema rais ateue watu wenye taaluma na wizara husika dr awe waziri wa afya na mtu mwenye uwekedi wa maswala.ya uchumi awe waziri wa fedha. na ikiwezekana chambo wa miundo mbinu awe katibu mkuu wizara ya madini kwenye fani yake. Hakafu si vibaya kwa nafasi zake kumi anichague ili niwawakilishe vijana au mnasemaje?
 
Kama ilo lipo na majina haya tajwa basi,kuna moto kuwawakia CCM kwa baadhi ya wateuliwa na kuibua mzigo mwingine wa aibu kubwa kwa kuwa kwa sasa Serikali inaitaji watu wasafi kuitetea kwenye jamii.

1: GODFREY ZAMBI-
kama atapata sawa kidogo madhaifu machache

2: ABDALLAH KIGODA-
Huyu ni muhimu kuja kuimarisha na kustwaisha uchumi tunavyokwenda ukingoni

3: KHAMIS KIGWANGALLA-
Anafaa ila anaitaji kuangaliwa kwa makini

4: FAUSTINE NDUGULILE-
Swadakta pasi na shaka ni aina ya viongozi ambao walitakiwa kujengwa toka anaingia madrakani

5: CHARLES TIZEBA-
anastahiki Pia

6: JANUARY MAKAMBA-
Aibu nyingine ya mwaka na hapa ndipo homa itapoanza kupanda na kushuka.Hakika kwa jinsi alivyoishupalia wizara ya madini,akipewa wizara hiyo na kwa sababu ambazo ziko ndani ya box,basi wamekaribisha kelele nyingine ya umma zaidi hata ya huyo aliyekuwepo.Na hakika ataingia asubuhi ofisi leo baada ya masaa matatu kinanuka upya.

Kwa watu wenye kutumia busara ingekuwa si vyema basi kumpa mtu madaraka ambae ananegative attention na vyombo vya habari tena hasa Jamii Forum ambayo kwa sasa ni moja ya source and centre of information kwa baadhi ya vyombo vya habari.Hakika wateuzi wake kama wanataka kumpumzika kelele za vyombo vya habari ambavyo vinaibua na kutibua nyongo ya chuki ya umma dhidi ya Serikali basi ni kumuacha huyu jamaa nje ya baraza la mawaziri.Lakini kitendo cha kumweka ndani eti kumpunguza makali na kumfanya asiwe active kushupalia mambo kwa tiketi ya kunuifaika yeye na si Taifa itakula kwa Serikali zaidi ya ambavyo ingemuacha nje ya Serikali.

7: STEPHEN MASELE

Anastahiki ukiondoa soo la jimboni kwake,ila anitaji uangalifu wa karibu.

Mkuu umeshindwa kutoa details, naona umejiuma-uma tu,naweza kusema subiri wachambuzi wasema upate pa kudanda/kuigilizia/kudesa
 
Wana jamvi,

katika gazeti la Mtanzania la leo kuna habari inayosema kamati kuu ya CCM inakutana leo saa 4 IKULU kujadili mambo mbalimbali ikiwemo kupokea mapendekezo ya party caucus ya kutaka mawaziri 8 kujiuzulu.

Inasemekana kwamba CCM inafanya haraka kubadili BLM ili kuipokonya CHADEMA ajenda yake ya OPERESHENI UWAJIBIKAJI.

Sehemu iliyonivutia katika habari hii ni pale chanzo hicho kilichotaja majina ya mawaziri wanaotarajiwa kuchukua nafasi zitazoachwa wazi kuwa ni:

-GODFREY ZAMBI
-ABDALLAH KIGODA
-KHAMIS KIGWANGALLA
-FAUSTINE NDUGULILE
-CHARLES TIZEBA
-JANUARY MAKAMBA
-STEPHEN MASELE

Wana jamvi, mnawaonaje mawaziri wetu hawa wapya watarajiwa?

Mkuu, Dr Charles Tzeba ni janga huyu alikuwa anasambaza sms kutoka kwa mkulu kwa washikaji wake hata kwa changudoa. Huyu jamaa hafai kabisa uongozi wa juu hana siri kabisa ni majivuno tu.
 
Mwigulu Nchemba kabla hatujamnyang'anya vyeti, apewe uchumi na fedha!!!!! yule aliyemsaidia kule igunga kafumu akalie kiti cha ngeleja. NIMEZINGATIA TAALUMA ZAO.

Angalizo:
hatutakuwa salama mpaka ccm tuizike. na kadri wanavyoteuliwa mawaziri wabovu ndivyo wananchi wanavyozidi kuerevuka na kujiunga na wachimba kaburi la ccm.
 
Nundu na Mfutakamba siyo watenganishwe bali mmoja wao lazima aondoke akafuge nyuki. Kati ya hao wawili lazima mmoja ni fisadi wa kutupwa na wamegombea maslahi wizarani.
 
ni vema rais ateue watu wenye taaluma na wizara husika dr awe waziri wa afya na mtu mwenye uwekedi wa maswala.ya uchumi awe waziri wa fedha. na ikiwezekana chambo wa miundo mbinu awe katibu mkuu wizara ya madini kwenye fani yake. Hakafu si vibaya kwa nafasi zake kumi anichague ili niwawakilishe vijana au mnasemaje?
Mkuu unamfahamu vizuri Omari Chambo?
JK alijitahidi sana kuwaweka watu kwenye taaluma zao akidhani watamsaidia. Angalia Nundu na Mfutakamba. Hawa ni wataalam wa mambo ya ndege walitarajiwa kulifufua shirika la ndege lakini wapi. Mponda ni PhD wa utawala wa afya lakini ndio hatakiwi na madaktari! Mama Tibaijuka sijaona makazi yoyote!
 
Mm nafikiri Mh Pinda anafaa na abaki pale pale Uwaziri Mkuu ni mchapakazi mzuri na muadilifu, Mh Mwakyembe ampe Nishati na Madini,Mh Sitta muweke Tamisemi ,Magufuli abaki palepale ila tunaomba mh Kabaka amtoe kabisa huyu mama hafai ata kidogo pamoja na hao wengine wanaotuhumiwa!
 
[h=2][/h] [h=3]KAMATI KUU YA CCM YAAFIKI KUVUNJWA KWA BARAZA LA MAWAZIRI[/h]
Rais amepokea taarifa na maazimio ya Kamati ya wabunge wa CCM na Kamati ya uongozi ya wabunge wa CCM juu ya kilichotokea kwenye bunge lililopita mjini Dodoma.
Taarifa hizo zimewasilishwa kwenye kamati kuu na kujadiliwa. Pamoja na taarifa hizo kamati Kuu imepokea taarifa ya jinsi Rais alivyojipanga kuchukua hatua za kuwawajibisha mawaziri na watendaji wa serikali na wale wa mashirika ya umma waliobainika kuhusika na ubadhirifu ulioinishwa na taarifa ya Mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za Serikali, Kamati za kudumu za bunge na wabunge bungeni.

Kamati Kuu imeamua yafuatayo; 1. Kamati Kuu inatambua na kuheshimu haki na wajibu wa wabunge kujadili utendaji wa serikali yao.Inapongeza juhudi za serikali kuhakikisha kuwa ripoti ya mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali inajadiliwa kwa uwazi na hivyo kuibua mapungufu yaliyojadiliwa.
2. Kamati Kuu imeridhika na imebariki uamuzi wa Rais KULISUKA UPYA BARAZA LA MAWAZIRI na taasisi zingine zilizoanishwa katika ripoti hizo. Imesisitiza utekelezaji wa uamuzi huo ufanywe mapema iwezekanavyo.
Aidha kamati Kuu imeipongeza Kamati Teule ya baraza la wawakilishi Zanzibar iliyoundwa kuchunguza utendaji katika sekta mbalimbali kwenye serikali ya mapinduzi Zanzibar kwa taarifa yao.
Kamati Kuu inawapongeza wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kwa jinsi walivyojadili taarifa hiyo na pia Kamati Kuu inaipongeza Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa kuipokea taarifa na kuanza kuifanyia kazi.
 
Back
Top Bottom