Mnaonaje Baraza hili jipya la Mawaziri linalotarajiwa?

Wana jamvi,

katika gazeti la Mtanzania la leo kuna habari inayosema kamati kuu ya CCM inakutana leo saa 4 IKULU kujadili mambo mbalimbali ikiwemo kupokea mapendekezo ya party caucus ya kutaka mawaziri 8 kujiuzulu.

Inasemekana kwamba CCM inafanya haraka kubadili BLM ili kuipokonya CHADEMA ajenda yake ya OPERESHENI UWAJIBIKAJI.

Sehemu iliyonivutia katika habari hii ni pale chanzo hicho kilichotaja majina ya mawaziri wanaotarajiwa kuchukua nafasi zitazoachwa wazi kuwa ni:

-GODFREY ZAMBI
-ABDALLAH KIGODA
-KHAMIS KIGWANGALLA
-FAUSTINE NDUGULILE
-CHARLES TIZEBA
-JANUARY MAKAMBA
-STEPHEN MASELE

Wana jamvi, mnawaonaje mawaziri wetu hawa wapya watarajiwa?

Huyu jamaa simpendi huyu kana sifa ya unafiki nafiki
 
Jamani yaaani kuna kiongozi yeyote ndani ya mfumo wa CCM ya sasa anayeweza kuwa na jipya katika kutukwamua kutoka katika umasikini huu tuliosukumiwa na watawala hawa hawa?????????

I dont care about who is who to replace whoever minister now!! Total Regime change is the ANSWER.
 
Hatujasema baraza ni suluhisho bt tia maji 2fike 2015 chadema 2ingie rasmi magogoni.JANUARY MAKAMBA JANGA LA KITAIFA.
 
wana jamvi,

katika gazeti la mtanzania la leo kuna habari inayosema kamati kuu ya ccm inakutana leo saa 4 ikulu kujadili mambo mbalimbali ikiwemo kupokea mapendekezo ya party caucus ya kutaka mawaziri 8 kujiuzulu.

Inasemekana kwamba ccm inafanya haraka kubadili blm ili kuipokonya chadema ajenda yake ya operesheni uwajibikaji.

Sehemu iliyonivutia katika habari hii ni pale chanzo hicho kilichotaja majina ya mawaziri wanaotarajiwa kuchukua nafasi zitazoachwa wazi kuwa ni:

-godfrey zambi
-abdallah kigoda
-khamis kigwangalla
-faustine ndugulile
-charles tizeba
-january makamba
-stephen masele

wana jamvi, mnawaonaje mawaziri wetu hawa wapya watarajiwa?

same forest...different monkeys
 
Yani Kigoda? Liuza viwanda na mashirika ya umma kwa wawekezaji hewa (wasio na sifa). Tulimsikia Mkapa alipokua anaongea kwenye kigoda cha mwalimu Nyerere! Kwamba watuambia mashirika yaliyobinafsisha yale yameleta tija gani kwa watz! sasa huyu huyu apewe uwaziri? Tazito letu tena hapa ni mfumo mbaya wa kupata mawaziri. Sasa angalia hiyo oradha iliyotolewa inamaanisha CCM watu wasafi wameisha. Inabidi huu mfumo wa kuteua wabunge kuwa mawaziri tuukate kwenye katiba mpya, ili mawaziri watoke sehemu nyingine kabisa, wawe watu wenye utaalamu na mambo ya wizara husika, siyo wanasiasa wanadanganywa kila siku na wafanyakazi wao kwa sababu hawaelewi chochote.

Nakubaliana na wewe kuwa Abdallah Kigoda ni mmoja kati ya mafisadi waliotufikisha mahala pabaya tulipo sasa, huyu ndiye aliyeingia mikataba mibovu ya madini akiwa waziri wa madini na nishati na ni huyu huyu aliyesimamia uuzwaji kiholela wa mashirika ya umma na kitu kibaya kuliko vyote ambavyo Kikwete anaweza kufanya ni kumteua tena kama waziri!! Akidiriki kumpa wizara ya fedha badala ya Mkullo that will be his worst nightmare; the guy is worse than Mkullo!!Chonde chonde msimpeleke huyu mwizi wizara ya fedha atatulaza na njaa.
 
Chupa mpya mvinyo ule ule. Mafisadi ama watoto wao watupu. Kwani CCM imebaki na hata msafi mmoja? Kimsingi wabunge wangeamua kuikabidhi serikali upinzani kidogo ndipo tungesonga mbele zaidi ya kucheza ngoma ile ile na manju wale wale... wachovu na walioishiwa hasa mkuu wao.
 
1.Faustine Ndungulile janga la kitaifa hafai uongozi ni mbovu sana,si mtu wa jamii kabisa kashindwa kuchangia ujenzi wa kituo cha polisi kibada mpaka sisi wakazi tukamuomba diwani atusaidie na kituo kishajengwaa(akiongea mkazi m1 wa kgmbni)
2.February Janga la kitaifa,hafai hata kidogo ana deni anadaiwa la usd 2mils sasa atatumia uwaziri kulipa fadhila,sisi wakazi wa bumbuli atashindwa kutuwakilisha vyema(akiongea mkazi wa tanga)
3.Hkigangwalla-Huyu ni mnafiki na mzandiki hafai hata kuwa mjumbe wa kamati za kudumu bungeni angetolewa nje kabisa
4.Nzambi @ ls anafaa
 
Kigoda na January tena.Ovyo sana.No, nategemea watendaji wazuri zaidi,sio hawa.
Wana jamvi,

katika gazeti la Mtanzania la leo kuna habari inayosema kamati kuu ya CCM inakutana leo saa 4 IKULU kujadili mambo mbalimbali ikiwemo kupokea mapendekezo ya party caucus ya kutaka mawaziri 8 kujiuzulu.

Inasemekana kwamba CCM inafanya haraka kubadili BLM ili kuipokonya CHADEMA ajenda yake ya OPERESHENI UWAJIBIKAJI.

Sehemu iliyonivutia katika habari hii ni pale chanzo hicho kilichotaja majina ya mawaziri wanaotarajiwa kuchukua nafasi zitazoachwa wazi kuwa ni:

-GODFREY ZAMBI
-ABDALLAH KIGODA
-KHAMIS KIGWANGALLA
-FAUSTINE NDUGULILE
-CHARLES TIZEBA
-JANUARY MAKAMBA
-STEPHEN MASELE

Wana jamvi, mnawaonaje mawaziri wetu hawa wapya watarajiwa?
 
Wakuu wana JF,naomba tumsaidie Rais Juu ya nani abaki na nani aondolewe na nani abadishiwe wiraza kwenye baraza jipya linalotarajiwa soon:

mawazo yangu:
1.Ngeleja na Malima OUT,wametusababishia madeni makubwa yakiwemo DOWANS
2.Nundu na Naibu wake wabadilishiwe wizara,cant work together kila sikumigogoro
3.Ciril na Nyalandu watenganishwe,na kama nafasi mpya ni chache Nyalandu OUT
4. waziri wa afya abadilishiwe wizara,ya afya imemshinda ila kwa kuwa bado ni kijana mdogo with limited experience apelekwe wizara ndogo ndogo kama ile ya Simba.
5.Sophia Simba OUT-> none existent
6. Mwakyembe na Magufuli should be separated,kila mmoja awe waziri kamili.
7. Kabaka OUT none existent
8. Magembe abaki na wizara yake
9. Mali asili na Utalii OUT
10.Pinda abakie waziri mkuu. SIO FISADI.
11.MKULO OUT ameshindwa kuthibiti matumizi ya dollar nchini.
12.

endeleeni wadau
 
..aondoke Kikwete, he has proven to be a failure.

..mtabadili mawaziri lakini kama Raisi siyo competent basi ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu.

..kwa system yetu ni lazima uanze na kuchagua Raisi competent. ukiharibu ktk kuchagua Raisi basi nchi ndiyo inakwama kama tunavyoshuhudia sasa hivi.

NB:

..JK, ambaye kitaaluma ni mchumi, alipomchagua Zhakia Meghji kuwa waziri wa fedha na uchumi, it became evident to me kwamba kwamba JK ni janga la kitaifa.
 
imefika wakati achaguliwe mtu kama anaweza na sio kwa sababu ni mwanachama wa chama tawala hata kama hawezi. Kwanini Lipumba asiteuliwe kuwa mbunge na akapewa wizara ya fedha na uchumi? Anazeeka na ujuzi wake na sisi tunazidi kudidimia kiuchumi.
 
Waliotajwa na kashfa mbalimbali wote out!
Pinda nae ni wa kumtimua as he is becoming muoga ata kuwapiga bit mawaziri!
Ila Ngeleja na Mkulo wasepe kwa kuanzia uzembe wao una impact kwa uchumi wetu!
Magufuri,Mwakye,Sitta wabaki!
 
sijui tunafurahishana tu ama tunamshauri nani.Kama ni JMK mshaurini aachie ngazi aingie kwenye historia kuwa aliondoka kwa amani madarakani baada ya kuona kuwa kufanya hivyo ni kwa maslahi ya Watanzania, miaka mitatu kabla ya muda kwa kuitimiza falsafa ya kuachiana kijiti kwenye relay
 
lile kundi pale hakuna mtu makini kwa maslahi mapana ya taifa hili hivyo ukiniuliza nitasema tu watoke wote!
 
Unaacha kununua kiatu kipya unataka kuweka viraka na soli za viatu vilivyochakaa kila siku? wote waondoke na kuna tetesi kua atawapa wapinzani nafasi za uwaziri
 
Wakuu wana JF,naomba tumsaidie Rais Juu ya nani abaki na nani aondolewe na nani abadishiwe wiraza kwenye baraza jipya linalotarajiwa soon:

mawazo yangu:
1.Ngeleja na Malima OUT,wametusababishia madeni makubwa yakiwemo DOWANS
2.Nundu na Naibu wake wabadilishiwe wizara,cant work together kila sikumigogoro
3.Ciril na Nyalandu watenganishwe,na kama nafasi mpya ni chache Nyalandu OUT
4. waziri wa afya abadilishiwe wizara,ya afya imemshinda ila kwa kuwa bado ni kijana mdogo with limited experience apelekwe wizara ndogo ndogo kama ile ya Simba.
5.Sophia Simba OUT-> none existent
6. Mwakyembe na Magufuli should be separated,kila mmoja awe waziri kamili.
7. Kabaka OUT none existent
8. Magembe abaki na wizara yake
9. Mali asili na Utalii OUT
10.Pinda abakie waziri mkuu. SIO FISADI.
11.MKULO OUT ameshindwa kuthibiti matumizi ya dollar nchini.
12.

endeleeni wadau

Labda wale tu waliotia saini kumfukuza PM wengine wote ni mzigo ila mbaya zaidi ni JK. lkn tuache hayo, swali ni hela yetu watarudisha au ndo wanabadilishwa na upepo unapita?

Hatutaki ujinga huu tena!!! kwahiyo mleta mada unatutega? Ulidhani tutafurahia utumbo huu?

Namuunga mkono iwapo atahamisha mawaziri wa kambi ya upinzani wamsaidie bila kuweka walinda mafisadi ka kigwangala anayesema eti hawezi kusaliti chama chake!!!!
 
:crying::fear::A S shade: Kwa jinsi nionavyo mimi hilo baraza is irreplaceable maana chichiem wote ni wachafu, wabadilishwe tuu au turudi meza ya uchaguzi. ingekuwa sheria inaruhusu ingefanyika serikali ya mseto, otherwise hata hao wengine wakija itakuwa kama waliokuwepo kabla maana kila mmoja atataka kuchota shamba la bibi.:frusty::nono:
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom