Mnaoharibu kiswahili mnaniudhi

rosemarie

JF-Expert Member
Mar 22, 2011
6,887
3,412
sipendi kuona watu wanasema usariti!!!badala ya usaliti----wanasema rema badala ya lema-----wanasema haroo badala ya haloo-----wanasemo hiko badala ya hicho------wanasema kukuhalibia badala ya kukuharibia----------naomba mjifunze kiswahili
 
Kuna sehemu bango kubwa wameandika wanauza ugari na wari.
Wengine hawafanyi makusudi nafikiri.
 
ahh hautakiwi kupatwa na hasira kw avitu/mambo km aya cz wengine hatujui/awajui kweli....

labda uwahurumie tu lakin kukasirika ju ya kitu km icho dah utajiumiza bure ...eg case ya r na l mtu kazaliwa kakulia uko kijijini tarime ndani ndani then unategemea atakutendea haki panapo la na ra?


tak t easy ..hifadhi hasira zako kwa mambo mengine ya msingi....thou kweli inaboa na aipendez tunavyokosea lugha lakin ndo ivyo sasa ishakua na kupandsha hasira si fresh...labda uwe kifimbo cheza ukimwona mtu kakosea fasta mpe bakora zake ....naenda kupasha kiporo karibuuuuuuuuu
 
sipendi kuona watu wanasema usariti!!!badala ya usaliti----wanasema rema badala ya lema-----wanasema haroo badala ya haloo-----wanasemo hiko badala ya hicho------wanasema kukuhalibia badala ya kukuharibia----------naomba mjifunze kiswahili

Kuna matatizo makubwa sana kwenye matumizi sahihi ya lugha yetu. Ukiachilia mbali matumizi ya istilahi, lakini hata matumizi ya nahau na methali yamedidimia sana siku hizi, si ajabu nyingi ya semi zinapotishwa sana. Tatizo nadhani linachangiwa na watu kudhani kwua wanakifahamu Kiswahili kwa sababu wao ni 'waswahili', kunawafanya wasijifunze lugha fasaha
 
husninyo nimecheka sana,nafikiri sio makusudi kuna haja ya kujireekebisha

mi mwenyewe nilipoona nilicheka halafu nikasikitika. Hapo ndio nikagundua kuwa wengine hawafanyi makusudi. Ila pia inakera na kibiashara sio vizuri. Nilitaka kwenda kula nikahairisha maana nilijiuliza kama uandishi tu hawapo makini, huo ugari na wari utakuwa umeiva kweli!
 
halafu hako kaneno "hiko" nakisikia sana radio one,,ina maaana program manager hayupo makini?
 
mimi napenda kweli sababu najua huyu jamaa original yake ni ipi!
 
kwa mfano ukimsikiliza mrema burudaaani kabisa, Unanua huyu ni Mchaga, na hii imefika mpaka kwenye kuandika!
 
Acheni kutoa hoja za kuwahurumia wasiojua mahali pa La na ra. Hii ni dalili ya mtu kutojithamini na kutothamini chake. Mbona mtu huyo huyo hataandika 'ranguage' badala ya language au 'erectricity' badala ya electricity wakati anaandika Kiingereza? Naweza kumfahamu akizungumza hivyo, lakini kuandika pia? Inaonesha ubovu wa elimu na kutothamini lugha yako.
Binafsi, ndiyo maana sisikizi nyimbo za kizazi kipya wanaosema ufukala badala ya ufukara.
 
Back
Top Bottom