Mnamkumbuka Mambokoso soko la Songea ?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,475
39,988
Sijui ndio lilikuwa jina lake au mimi nimechanganya; alikuwa kichaa pale soko la Songea. Alikuwa na sifa moja ambayo wachache wanaikumbuka. Nimeiona picha fulani nikamkumbuka. Hivi bado yupo hai?
 
"Sijui", "nimechanganya" = hujui, unachanganya na bado unajisifu?

"kichaa" = mlilie aliopotea usimlilie aliokufa".

Ulifikiri kaomba hayo? ni majaaliwa ya Mungu. Nawe uko hai "hujafa hujaumbika".
 
mimi namkumbuka PAUDONGO! alikuwa crazy fulani hivi makao yake makuu mitaa ya mahenge pale karibu na ofisi za mifugo.
 
Si lazima kuchangia kila thread
 
namkumbuka sayo pale mugumu serengeti bado yupo anadunda
 
"Sijui", "nimechanganya" = hujui, unachanganya na bado unajisifu?

"kichaa" = mlilie aliopotea usimlilie aliokufa".

Ulifikiri kaomba hayo? ni majaaliwa ya Mungu. Nawe uko hai "hujafa hujaumbika".
We dada!
Una maana gani kuweka marangirangi kwenye thread ya mtu?
Mbona hakuna kilichokosewa?
Umeamkia Mnyamani kwa muuza supu za mapupu nini?
 
Si lazima kuchangia kila thread

Binaadam mzima nafaham zake, hawezi kuishi kama mnyama mwitumi ambae uhai wa kila mmoja wake, hutegemea urefu wa makucha yake na ukali wa meno yake.

U"kichaa" wake hajauomba, tusitake kumuumbuwa hapa kwa maradhi yake!
 
We dada!
Una maana gani kuweka marangirangi kwenye thread ya mtu?
Mbona hakuna kilichokosewa?
Umeamkia Mnyamani kwa muuza supu za mapupu nini?

Kaa kimya, au jibu hoja. Marangi mekundu waliyaweka ya nini kwenye forum si ya kutumika?, na hapa ndipo pahala pake, kwani niliendea kuyanunua dukani nikayapaka hapa?
 
Binaadam mzima nafaham zake, hawezi kuishi kama mnyama mwitumi ambae uhai wa kila mmoja wake, hutegemea urefu wa makucha yake na ukali wa meno yake.

U"kichaa" wake hajauomba, tusitake kumuumbuwa hapa kwa maradhi yake!
U r very wrong!
Kusema habari za uwepo wa kichaa mtaa fulani si kumuumbua wala kuomba aendelee kuwa hivyo!
Kwani ni mzima (kiakili) sasa?...au unatafuta kuonekana wa huruma sana!
Jazba zenu hizo zinawasidia nini?
 
mimi namkumbuka PAUDONGO! alikuwa crazy fulani hivi makao yake makuu mitaa ya mahenge pale karibu na ofisi za mifugo.

Kama huwezi kumsadia, japo muombee kwa Mungu wako amuondoshee hayo maradhi, hajaomba kuwa nayo hayo. Tusiwaumbue hapa wenye maradhi.
 
ah ah ah Mwl wa darasa la kwanza C kazini lol!nina wasiwasi na jinsia yako.umeelewa kweli somo?au umesoma tu kwakuwa imeandikwa?Hakuna neno baya alotumia mwanakijiji hapo kauliza kama tunamfahau huyo mtu,so acha tunaomfaham tuchangie basi.Si lazima wote tuwe waandishi wengine tunaweza kuwa wasomaji tu.
"Sijui", "nimechanganya" = hujui, unachanganya na bado unajisifu?

"kichaa" = mlilie aliopotea usimlilie aliokufa".

Ulifikiri kaomba hayo? ni majaaliwa ya Mungu. Nawe uko hai "hujafa hujaumbika".
 
U r very wrong!
Kusema habari za uwepo wa kichaa mtaa fulani si kumuumbua wala kuomba aendelee kuwa hivyo!
Kwani ni mzima (kiakili) sasa?...au unatafuta kuonekana wa huruma sana!
Jazba zenu hizo zinawasidia nini?

Sina haja ya kuonekana na huruma, lakini ukweli ntasema, si vyema kukaa hapa na kuanza kuumbuwa wenye matatizo ya akili, Jee, akiwa mama yako au baba yako utafanya hivyo?
 
Ukichaa ni ugonjwa, hakuna anayeoomba kuwa kichaa, kwa maana hiyo hata huyo "Mambokoso soko la Songea" hakuomba kuwa kichaa. Kwa kuwa wewe bado unaishi. Yanaweza kukukuta zaidi ya hayo. Mgonjwa tunapaswa kumwonea huruma na sio kumdhihaki.
 
ah ah ah Mwl wa darasa la kwanza C kazini lol!nina wasiwasi na jinsia yako.umeelewa kweli somo?au umesoma tu kwakuwa imeandikwa?Hakuna neno baya alotumia mwanakijiji hapo kauliza kama tunamfahau huyo mtu,so acha tunaomfaham tuchangie basi.Si lazima wote tuwe waandishi wengine tunaweza kuwa wasomaji tu.

Kumuita "Kichaa" pekee ni neno baya. Jifunze maadili.
 
sasa ulitaka amuiteje?Mbn hatusemi kikwete,obama?tunasema Rais.......,au yule kaka mrefu,mfupi,mnene etc kwani ukiambiwa mueleze mtu fulani mfano Idd Amin utasemaje?

Asingemuita wala kutaka kumtolea mfano humu JF, huyo hajayaomba hayo. Msitake kutetea upumbavu, fikiri.
 
sasa ulitaka amuiteje?Mbn hatusemi kikwete,obama?tunasema Rais.......,au yule kaka mrefu,mfupi,mnene etc kwani ukiambiwa mueleze mtu fulani mfano Idd Amin utasemaje?

Kwa kuwa kichaa ni ugonjwa kama magonjwa mengine wanayomtesa mtu na kuwahuzunisha ndugu zake , haionyesha maadili na huruma kusema kushabikia suala hilo. Ndio maana hatusemi yule mgonjwa wa Ukimwi au wa Kansa bado yupo hai? Kwa maoni yangu swahili hilo linamtakia mtu mauti, ni afadhali lingekuwa bado yupo eneo pale? ikimaanisha kuwa labda alishaenda eneo lingine.
 
Back
Top Bottom