Mnakumbuka kifo cha Dr. Ouko?

matawi

JF-Expert Member
Mar 29, 2010
2,052
242
Inashangaza kuona mkulu amerilax sana kuhusu Mwakyembe.

Watanzania wameona jinsi viongozi wakuu waandamizi wanavyotofautiana lugha hasa DCI, Waziri wa mambo ya ndani, Waziri wa afya na hata Mzee Sitta kuhusu ugonjwa wa Mwakyembe; cha ajabu naona mkulu umekaa mbali hata hutaki kutoa maoni yako au hutaki kuwasimamia watu wako wasiwachanganye wananchi.

Lakini hakika nakwambia JK, kama huyu mpiganaji atapoteza maisha bila ya uwazi nchi itayumba na wewe utahusishwa na tatizo hili kama EL alivyowaambia wajumbe wa NEC kuwa wizi wa Richimond ulikuwa unajua?
 
Jamani mbona mnamuonea Jakaya; yeye alishatamka kuwa huko ccm uhasama kati ya viongozi ulikuwa umefikia hatua ambapo walikuwa hawaaminiani mtu kuacha glasi yake ya kinywaji bila ULINZI MAHUSUSI!! Yeye kama kiongozi wa nchi asingesema maneno haya bila kuwa na ushahidi kuwa uhasama huo ulifikia hatua ya kuuana kwa kutumia sumu. Sasa mnamtaka Kikwete aseme nini zaidi ya haya aliyoyasema?
 
He na JK huyo ana uhusiano gani na Ouko?

Ni lazima a comment kwa kila tukio si itakuwa balaa tena
 
sa mbna hujamuelezea huyo dr.aouko wengne vjana sana hatumjui.

Haya vijana niwape somo; Dr.Robert Ouko alikuwa waziri wa mambo ya nje wa Kenya aliyeuawa na majasusi katika hali ya kutatanisha ambayo iliwahusisha waziri mmoja wa Kenya Nicholas Biwott na rais wa wakati huo wa Kenya Daniel Arap Moi!!
 
Haya vijana niwape somo; Dr.Robert Ouko alikuwa waziri wa mambo ya nje wa Kenya aliyeuawa na majasusi katika hali ya kutatanisha ambayo iliwahusisha waziri mmoja wa Kenya Nicholas Biwott na rais wa wakati huo wa Kenya Daniel Arap Moi!!

Well,sasa mtoa thread hata hajaeleweka,heading na aliyozungumza ndani tofauti kabisa! kimsingi anachanganya watu au lengo lilikuwa kumsema tu JK?
 
Back
Top Bottom