Boflo
JF-Expert Member
- Jan 20, 2010
- 4,384
- 4,409
Wadau hapo zamani za kale kulikuwa na shirika la ndege East African Airlines. Ilikuwa sehemu ya East African Community. Waliokuwa wanakmiliki ni Tanzania, Kenya na Uganda.
Mwaka 1971, familia tulisafiri Mbeya hadi Dar na ndege ya East African Airways. Ilikuwa Prop Job kama ile kwenye picha ya kati kati. Tulikuwa tunatoka kijijini Manda kwa ndugu wa baba. Mkikaa kwenye kiti kama vile mnatazama hewani, halafu ilisha ruka ndo mnakuwa sawa. Ingawa nilikuwa na miaka saba nakumbuka waliwapa aibiria lunch box. Mwaka 1976 tulisafiri na ndege 727 Nairobi -Dar. Haikuwa mbaya. Pia tulisafiri na treni, lakini jamani zilikuwa safi na wenye wahudumu waliopenda kazi yao.
Nakumbuka nikiwa Form One mwaka 1977, ghafla shirika hiyo ilivunjwa. Waliokuwa na mali (treni, ndege, mabasi) kwenye nchi yao ndo ilikuwa mali yao. Wakati ule damu ulikuwa mbaya kweli kati ya WaTanzania na WaKenya.
Mwalimu shuleni alitusimulia hivi, waKenya walivizia siku ambayo ndege kubwa na nzuri zitakuwa zimetua pale Embakasi airport Nairobi, ndo wakazizoa na kuita Kenya Airways! Tanzania tuliambulia zile Fokker Friendships na ndege nyingine 737 ikawa Air Tanzania, halafu Uganda walikuwa wazembe eti walipata ndege moja tu! Ikawa Uganda Airways.
Lakini jamani nakumbuka watu walikuwa na huzuni kubwa mno jumuiya ilivyovunjika. Mbaya zaidi watu wakawa wanyama. WaTanzania walifukuzwa Kenya kama mbwa. Hasa hao waliokuwa wanafanya kazi na East African community. Wengine walirudi Tanzania kwa mguu na begi moja!
Wenye stori za wakati ule hebu mtupashe.