MMU yaabudu ngono?

Kwamba MMU member kutokana na hoja mbali mbali za kimapenzi zinazojadiliwa kwa ushabiki mkubwa je member hao wa JF waliojikita sana kwenye jukwaa hilo wanaabudu ngono bila kujijua?

Naona ni mtazamo wako tu mkuu,

Walioamua kuweka jukwaa la MMU, naamini walijua kuwa kuna watu ambao wanapenda sana hadithi na michango ambayo ina mrengo wa kimapenzi na ngono...Ndio maana wakalianzisha. Na kwa kuwa lina wafuasi wa kutosha, hili jukwaa limekuwa likishambuliwa mara nyingi kana kwamba wadau wanachangia nje ya mategemeo ya jukwaa lenyewe....

Hii ni sawa na biashara nyingine yoyote, kwa kuwa kuna supply na demand, na vyote ama viko kwenye balance basi uhai wa jukwaa unakuwa guaranteed. Sasa kama hili jukwaa limesababisha mengine kupwaya, si kosa la wadau bali ndiyo kitu watu anapenda na kufurahia. Ila tukiendelea na mtazamo kama huu unaoelezea au wa Ruta, basi tunaweza kujikutana tunashauri MMU iwe inafungwa kwa muda ili kuruhusu wadau watembelee majukwaa mengine....Je hilo ndilo ambalo ungelitaka??
 
  • Thanks
Reactions: LD
Kuabudu ni kufanya Ibada.....

Inamaana Mzee Ruta watu humu MMU wameacha kumuabudu Mungu wao wanaabudu NGONO au?

Mmmmh basi kusaidia watu wasiendelee kuabudu Ngono tuwaombe walioliweka jukwaa la MMU waliondoe.

Halafu sasa na wale kule kwenye Siasa nao si watakuwa wanaabudu SIASA? Na lenyewe liondolewe au?

Mmmmh Naona na mimi sijaelew vizuri hi.
 
Back
Top Bottom