Kipeperushi
Senior Member
- Aug 17, 2011
- 167
- 33
Hivi habari hii ina ukweli? Mbona sipati picha? Rais Kikwete anamaliza muda wake wa kutawala kama Rais mwaka 2015, Lowasa, kama ni kweli inavyosemekana, wakati huo atakutana na upinzani toka kwa mtu/watu wengine kabisa, wala sio Kikwete. Sasa huu mpango unaofanywa na Lowasa wa kumharibia Kikwete kiutendaji (kama inavyodaiwa) unamasilahi ki-vipi kwa Lowasa kwa ajili ya 2015? Binafsi siamini kama hii propaganda inaukweli ndani yake. Naomba ufafanuzi.Gazeti la Dira Ya Mtanzania linamuhusisha Mh. Edward Lowassa kuwa ndio chanzo cha mgomo wa madaktari ili kumkwamisha Rais kiutendaji kwa manufaa yake ya kuusaka urais 2015. Vilevile linazidi kuripoti kwamba, Ikulu imetayarisha mipango kabambe kukabiliana naye. Licha ya Yote, inasemekana waziri huyu mku wa zamani kutokana na ukwasi wake wa kifedha, ametayarisha mipango kabambe pamoja na kutumia uwezo wake wa kifedha kuwanunua wabunge kuhasi dhidi ya mwenyekiti wa chama ambaye ndiye Rais. Hii ina maana kwamba, Lowassa anaweza kuwa Rais kabla ya 2015