Mmoja afariki dunia akijaribu kuongeza ukubwa wa nyeti zake

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,268
33,040
MMOJA AFARIKI DUNIA AKIJARIBU KUONGEZA UKUBWA WA NYETI ZAKE
attachment.php





DUNIA haikaukiwi matukio ya kustaajabisha, kwa hakika huu ni ulimwengu maridhawa na hawakukosea walionena kwamba dunia hadaa ulimwengu shujaa.


Stori ya kusikitisha, inatokea nchini Marekani ambako kijana Justin Street, amepoteza maisha akiwa kwenye jaribio la kuongeza ukubwa wa nyeti yake.


Habari kamili ipo hivi; Justin, 22, akiwa baba wa watoto wawili alikwenda kwa mwanamama Kasia Rivera ,35, aliyejitangaza kuwa ni mtaalamu wa tiba za kuongeza ukubwa wa nyeti za kiume.


Kasia aliweka matangazo barabarani kuwa anayo tiba ya kuongeza ukubwa wa nyeti za kiume, hivyo kumfanya Justin ahamasike kwenda kupata dawa hiyo ili kujiongezea ushababi.


Wanasema tamaa mbele mauti nyuma, ndivyo ilivyotokea kwa Justin, kwani baada ya kuomba dawa ya kuongeza ukubwa wa maumbile yake ya kiume, alidungwa sindano yenye madini ya silikoni.


Madini hayo, alidungwa kwenye nyeti yenyewe na baada ya muda mfupi, hali ya afya yake ilibadilika kuwa mbaya, alizorota na siku iliyofuata alifariki dunia.


Kutokana na tatizo hilo, Kasia alifikishwa mahakamani kwa kesi ya mauaji akituhumiwa kufungua zahanati bubu ndani ya nyumba yake iliyopo New Jersey, vilevile kutoa tiba za kiafya wakati hana taaluma hiyo wala leseni ya kuendesha kazi hiyo ya utoaji huduma za afya.


Kasia alipandishwa kizimbani wiki iliyopita, uchunguzi wa maiti umethibitisha kwamba Justin alifikwa na mauti baada ya madini ya silikoni aliyodungwa kwa sindano kuziba njia za mishipa ya damu.


Mmoja wa madaktari waliomfanyia uchunguzi Justin alisema kuwa hii ni mara ya kwanza kusikia silikoni inayotumika kuongeza ukubwa wa matiti ya wanawake imetumika kwenye kuongeza ukubwa wa uume.Kasia, amekana kuhusika na mauaji hayo.
 

Attachments

  • nyeti.jpg
    nyeti.jpg
    53.6 KB · Views: 1,417
Kufuga ujinga tu, na ukimwi huu nani anataka shurba. Kibamia is the best bwana, utamu wa pipi mate yako.
Sina hakika kama unachokisema ndicho unachokimaanisha. Wakina dada wa leo mna mambo sana, mara "ooh mb kubwa ndio mpango mzima", mara "ooh kibamia kinaleta shombo tu." Sasa kwa maneno hayo unafikiri mumeo atakuwa na amani ndani ya nyumba kama "faragha" yake ina utata?
 
Mungu alipoumba aliweka kila size na kila saizi inamtosha mwanamke yeyote yule,tatizo hapa ni ulimbukeni wa kudhani ukiwa na size kubwa ndio utaweza kumridhisha mwanamke.

Nenda salama kaka na ukifika huko utamjibu Mungu ulichokuwa unatafuta hata baada ya kupewa.

Wanaume turidhike na tulivyonavyo.
 
Ninyi akina dada wa kileo ndio tatizo. Vijana wakiume wanafuata mkondo tu

Sio akina Dada tu wa kileo, hata akina kaka wa kileo nao wanafanya wakina dada kuhangaika na hata kupoteza maisha, wakati wakiongeza makalio, hips, matiti, kujichubua nk, unadhani kama wanaume wa kileo wasingekuwepo hawa wadada wangehangaika kiasi hiki?
 
Mimi sisikitiki kwa kuwa kafa, nasikitika kwa kuwa lengo lake halikutimia. Tamia alisema atamuongezea kitu yake ukubwa lkn hakusema kama anachukua dhamana ya maisha yake. Kwa kweli kama angeongezeka halafu akafa, Tamia hakuwa na kosa, ila kwa sasa ashitakiwe kwa utapeli
 
kwake huyo mapenzi ni kukomoana,hilo liukuni alitaka la nini???eh,kinapita kichwa cha mtoto sembuse ukuni????
 
Ale dushelele dushe dushe dusheleleee x2. Nilimwambia asile ye alikula, akavimba akaja, mtoto mzuriii wa OBAMA.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom