Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,470
- 911,173
Mmiliki Palm beach kumburuza Tibaijuka
Wednesday, 22 December 2010 20:24
Nora Damian
MMILIKI wa kiwanja kilicho jirani na Hoteli ya Palm Beach ambacho ukuta wake umevunjwa, Taher Muccadam, amesema anarudi tena mahakamani kudai fidia na atahakikisha haki yake inatambuliwa.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Muccadam alisema amesikitishwa na kitendo hicho, kwani yeye ni mmiliki halali wa kiwanja hicho.
Makucha aliyoyaonyesha Waziri (Anna) Tibaijuka ni dharau kubwa kwa amri iliyotolewa na Mahakama, sisi tulitegemea yeye angekuwa mstari wa mbele kufuata na kusimamia sheria, alisema Muccadam na kuongeza kuwa:
Kama hakuridhika na maamuzi ya Mahakama Kuu, angerudi mahakamani kuomba mahakama itengue uamuzi wake sio kunyata na kuvizia muda wa usiku kuvunja sheria.
Mmiliki huyo alisema, kitendo hicho kimedhalilisha majaji, mahakimu na wananchi kwani, hawatakuwa na imani na mahakama katika utoaji haki.
Alisema anaamini atakaporudi mahakamani haki itatendeka na atalipwa fidia kutokana na uamuzi uliofanywa na serikali.
Muccadam alinukuu kifungu namba 107 cha Katiba, ambacho kinazungumzia utoaji haki na kusema, Waziri Tibaijuka amedharau na amepiga teke katiba ya nchi aliyoapa kuilinda.
Katiba ya Jamuhuri ya Muungano inasema, mamlaka ya utoaji haki itakuwa mikononi mwa Idara ya Mahakama na Idara ya Mahakama Zanzibar na kwa hiyo hakuna chombo cha serikali wala Bunge au Baraza la Wawakilishi kitakachokuwa na kauli ya mwisho katika utoaji haki, alisema Muccadam akinukuu kifungu hicho.
Alisema alipewa vibali vya kujenga uzio na jingo la ghorofa kumi baada ya kufuata taratibu.
Juzi usiku, serikali ilivunja uzio uliokuwa umejengwa katika kiwanja hicho na uzio mwingine uliojengwa jirani na Hospitali ya Aga Khan.
Kazi ya kuvunja ukuta huo ilifanywa majira ya saa 1:00 usiku na tingatinga la Halmashauri ya Manispaa ya Ilala chini ya ulinzi mkali.
Mmiliki huyo tayari alikuwa ametoa notisi ya siku saba kwa Profesa Tibaijuka kumtaka amuombe radhi na kumlipa fidia ya Sh2 bilioni kwa madai kuwa, amemdhalilisha kwa kusema alikipata kiwanja hicho kwa njia ya rushwa.
Kiwanja hicho namba 1006 kilicho Upanga jirani na Hoteli ya Palm Beach, ni kati ya viwanja ambavyo Profesa Tibaijuka alisema maeneo ya wazi na kwamba haviruhusiwi kuwa makazi.
Kwa mujibu wa Muccadam, kiwanja hicho kilikuwa kinamilikiwa kwa hati namba 186164/25 iliyotolewa Januari Mosi, 1975 kwa wamiliki wa kwanza ambao ni Shantaben Narottambahi Patel na Nilaben Girishumar Patel.
Alisema kiwanja hicho kilimilikishwa na Manispaa ya Ilala na miliki hiyo ilidumu kwa miaka 99, kabla yeye hajakinunua mwaka 2000.