Mmh..Mashaka yanazidi kuniwia kuhusu JW

Sizinga

Platinum Member
Oct 30, 2007
9,101
6,027
Nina rafiki yangu mmoja alitegemea kufunga ndoa mwezi huu wa 10 na mdada falni ambae ni mwanajeshi wa JW. Vikao vishakaliwa na kila kitu kilikuwa pouwa kabisa, ila juzijuzi tu yule dada kapewa tamko kwamba jeshi limezuia Likizo na hamna Ndoa kufanyika mpaka uchaguzi uishe. Na yule mshkaji kaniambia kwamba wapo kweye mazoezi makali kiasi kwamba yule dada kwa sasa ni full time service huko jeshini. Nashikwa na wasiwasi sana hasa nikiifikiria na ile kauli ya Mnadhimu SHOMBO.......
 
Hatma ya taifa hili ipo mikononi mwa Mwenyezi Mungu na wala siyo hao wababaishaji ambao kila kukicha nao humwomba Muumba awatunukie rehema Zake kebekebe
 
kumbuka safari ya wana wa israel, kutoka nchi ya misri wakienda nchi walio ahidiwa na mungu, lakini farao na jeshi lake walipania kuwaangamiza, wakiwa wanaielekea bahari ya sham,nyuma jeshi la farao, mungu alisema na musa bahari ikafunguka nchi kavu ikaonekana na wana wa israel wakapita salama salimini, lakini kilicho wakuta jeshi la farao? hakusalia mtu, hao wanajeshi ni kaka zetu, dada zetu watoto wetu, sasa wanatumwa na watu wenye maslahi yao binafsi kuja kututendea uovu, labda huyu mungu tunaye mwomba ni mungu wa akina farao na jeshi lake, tena nawasihi, wasije wakasubutu, kubeza maombi ya watanzania, hakika wataangamia wao na makombora yao na mabomu yao ya machozi nayakuwasha zitawalipukia wenyewe, Watanzania tumwombe sana mungu wala tusibadili nia zetu za kutaka mabadiliko, Mungu wetu si kiziwi hakika atasikia kilio chetu. wacha watii mamlaka ya wakuu wao. na wanasiasa.
 
Nina rafiki yangu mmoja alitegemea kufunga ndoa mwezi huu wa 10 na mdada falni ambae ni mwanajeshi wa JW. Vikao vishakaliwa na kila kitu kilikuwa pouwa kabisa, ila juzijuzi tu yule dada kapewa tamko kwamba jeshi limezuia Likizo na hamna Ndoa kufanyika mpaka uchaguzi uishe. Na yule mshkaji kaniambia kwamba wapo kweye mazoezi makali kiasi kwamba yule dada kwa sasa ni full time service huko jeshini. Nashikwa na wasiwasi sana hasa nikiifikiria na ile kauli ya Mnadhimu SHOMBO.......

Mkuu, ni SHIMBO si Shombo. Iwapo ulibadilisha makusudi yafaa ufikirie upya ili JF isijeonekana ya kihuni. Hata kama tunatofautiana naye hakuna haja ya kufanya majadiliano ya ki-maji taka. Huo si utamaduni wetu.
 
mimi naamini kwa maombi ya watanzania hakuna kibaya kitakachotokea muhimu ni mabadiliko octoba 31
 
Ni kweli wamerudishwa makambini kwa ajiri ya mazoezi ya kulinda usalama wakati maandalizi ya uchaguzi na baada ya kutangazwa matokeo yake. I hope wakuu wa jeshi ambao kwa statement ile wameonyesha wazi JW si jeshi lile lililokuwa na culture tofauti na upuuzi huu tunaouona, wameamua kulinda maslahi ya wale wanaowaona wanawafaa. Ingekuwa vema wangeheshimu maaamuzi ya wapiga kura.
 
Anayetishia kwa upanga huishia hivyohivyo. Ole wake uongozi wa Kikwete, ole wake utawala wa Shimbo. Kura kwa Slaa, hatudanganyiki, hatutushiki, habari ndiyo hiyo. Mambo ya Kenya yanakuja Tanzania. Nchi hii ni ya wananchi wa Tanzania. Si ya Kikwete, wala Shimbo.
 
anayeingia ikulu kwa karamu, atabakia hapo kwa bunduki "sumaye"
 
Ukiingia kwa mtutu utangoka kwa mtutu.
Vijana naona wamekuwa idle kitambo wameamua wawageukie watanzania wenzao KHAAAAAAAAAAAA
JWTZ Slaa UKISHINDA KUNA HAJA YA KULIPANGUA ILI JESHI MAANA LASTAILI KUITWA JESHI LA CCM SIO WATZ
 
anayeingia ikulu kwa karamu, atabakia hapo kwa bunduki "sumaye"

Hii kauli ingekuwa imetamkwa na upinzani huenda huyo mtamkaji angeitwa juha. Hakika nitamkumbuka sana Sumaye kwa kauli hii, alilenga mahali sahihi na kwa mtu sahihi. Huenda 2015 jamaa akabadili katiba na kujiongezea term nyingine kwa kisingizio kwamba anapendwa sana.
 
kumbuka safari ya wana wa israel, kutoka nchi ya misri wakienda nchi walio ahidiwa na mungu, lakini farao na jeshi lake walipania kuwaangamiza, wakiwa wanaielekea bahari ya sham,nyuma jeshi la farao, mungu alisema na musa bahari ikafunguka nchi kavu ikaonekana na wana wa israel wakapita salama salimini, lakini kilicho wakuta jeshi la farao? Hakusalia mtu, hao wanajeshi ni kaka zetu, dada zetu watoto wetu, sasa wanatumwa na watu wenye maslahi yao binafsi kuja kututendea uovu, labda huyu mungu tunaye mwomba ni mungu wa akina farao na jeshi lake, tena nawasihi, wasije wakasubutu, kubeza maombi ya watanzania, hakika wataangamia wao na makombora yao na mabomu yao ya machozi nayakuwasha zitawalipukia wenyewe, watanzania tumwombe sana mungu wala tusibadili nia zetu za kutaka mabadiliko, mungu wetu si kiziwi hakika atasikia kilio chetu. Wacha watii mamlaka ya wakuu wao. Na wanasiasa.

alfu lela-u-lela( siku elfu namoja)

 
Nafikiri kuna kitu furani kinaandaliwa ,ambacho sisi wananchi wa kawaida hatukifahamu,hawa jamaa sijui wanatupeleka wapi?
 
Sikumbuki nchi yetu kupitia kipindi cha mgawanyiko mkubwa kama uliopo sasa - thanks to JK's "heroics".
- sentiments za udini zimekithiri sana na kutishia kuwagawa wananchi in those lines
- jeshi kuanza kujihusisha na siasa na hata kuwatisha watu

HAIJAPATA TOKEA KWA RAIS MWINGINE YEYOTE KWA KUMBUKUMBU ZANGU!

My compatriots, this only goes on to confirm the need for change (and fast) before things start going astray. Uongozi ukiwa imposed kwa wananchi kama wanavyotaka kufanya CCM, nchi itakuwa vigumu sana kutawalika - or kujitawala yenyewe for that matter. If CCM wins, I can see the possibility of the govt being run from the barracks within the 1st 2 years after Oct 31. Hali hii ikitokea, haitam-suit hata JK & cronies kama wao hawajui, hivyo mlionao karibu washaurini waache fujo zao za kitoto wanazozifanya sasa - zitawatokea puani kwani jeshi si Shimbo peke yake....kuna army men wengi sana ambao resentment yao against CCM haina kipimo.
Let JK & cronies help this blessed nation to stay in peace by ensuring that the army men stay in their barracks where they belong!
 
du mwambie nduguyo avute subira tu baada ya mwezi mambo yatamwendea swafi. Pia mpongeza kwa niaba yangu kufunga ndoa na mwanajeshi maana wanaume wengi have negative feelings about wanajeshi to be wives.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom