Mmeishindwa kuinyanyua atcl;hela ya viwanja mpate wapi kama si aibu-dk silaa

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,956
22,148
Slaa: Mimi mtu makini sitendi kwa kukurupuka
• Asema CCM imepanga kuibua uongo mpya dhidi yake

na Mwandishi wetu, Meatu


amka2.gif

MGOMBEA urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, amesema kamwe hafanyi jambo lolote kwa kukurupuka.
Dk. Slaa alitoa msimamo huo jana wakati akihutubia mamia ya wananchi wa Meatu mkoani Shinyanga, kuhusiana na tuhuma kadhaa zinazoelekezwa kwake.
Mgombea huyo ambaye alipata mapokezi makubwa alipowasili mjini hapa kwa kutumia helikopta yake iliyotengemaa baada ya kupata hitilafu siku chache zilizopita, alisema Kikwete na vigogo wenzake ndani ya CCM wanaweweseka kutokana na mwamko unaoonyeshwa na Watanzania kuiunga mkono CHADEMA tangu kuanza kwa kampeni hizo na ndiyo maana wamekuwa wakimzushia kashfa mbalimbali.
“Sasa hivi nasikia wameenda kuwatafuta watu wasioona ili waseme nilipokuwa kiongozi wao nilitafuna fedha, mwanzoni walisema nimetumwa na kuungwa mkono na Kanisa Katoliki, hivi sasa wamenifungulia kesi kudai sh bil. moja. Kwa kawaida sifanyi jambo kwa kukurupuka, tutakutana huko huko mahakamani,” alisema Dk. Slaa na kushangiliwa na maelfu ya wananchi waliofurika kumsikiliza.
Alisema anashangazwa na ahadi nyingi zinazotolewa na mgombea huyo wa CCM ikiwamo ya kutaka kujenga viwanja vya ndege, wakati serikali yake haina hata ndege moja baada ya kuuawa Shirika la Ndege la Tanzania (ATC).
“Lakini hata kama kungekuwa na ndege, Watanzania wa Wilaya ya Meatu mtapanda hiyo ndege kusafirisha ng’ombe wenu sokoni? Kina mama wajawazito watapanda ndege hizo kwenda kupata matibabu? Ndiyo maana huwa nasema Kikwete si makini, kwa nini hizo pesa asizitumie kujenga zahanati, kununua magari ya wagonjwa na kujenga barabara?” alihoji Dk. Slaa.
Akisikilizwa kwa makini na wananchi hao, Dk. Slaa alitaja ahadi nyingine aliyoiita kuwa ni ya ununuzi wa baiskeli za miguu mitatu 400 (Bajaj) kwa ajili ya kina mama wajawazito.
“Leo wakati nakuja, nilikuwa napitia kumbukumbu za Bunge lililomalizika, nikaona ahadi hiyo ya Kikwete ya kununua Bajaj, ilikuwa kwenye kumbukumbu za Bunge wakati akilihutubia Bunge mjini Dodoma, leo miaka minne baadaye anatoa ahadi hiyo hiyo. Sijui kama Rais Kikwete huwa anasoma, hiyo ahadi alishaitoa na leo anaitoa tena kwenu,” alisema Dk. Slaa.
Alisema kama Rais Kikwete ana nia ya kuwasaidia kina mama wajawazito, alipaswa kupunguza ukubwa wa baraza lake la mawaziri ambao kila mmoja ana shangingi la sh mil. 200, sawa na kujenga zahanati nne ili fedha hizo zitumike kununulia magari ya wagonjwa. “Kabla sijapanda hii helikopta yangu, nilifanya mikutano kadhaa njiani na wakati nakuja, nilishuhudia mikokoteni mitano ya kuvutwa na punda na nyingine ng’ombe, ikitumika kuwabeba wagonjwa kuwapeleka hospitalini, lakini Kikwete anaahidi Bajaj 400 ambazo hata njia za kupita hazipo kutokana na uchakavu, huo ni mzaha kwa Watanzania, safari hii msimchague, chagueni CHADEMA,” alisema.

Akizungumzia tatizo la elimu nchini, Dk. Slaa alisema taifa liko kwenye msiba kubwa wa umaskini uliotokana na ukosefu wa elimu.
Alisema licha ya serikali ya CCM kutamba na ujenzi wa shule za kata, matokeo ya mitihani ya shule hizo ni mabaya na elimu inayotolewa haiwasaidii vijana wanaomaliza masomo yao kutokana na ukosefu wa walimu, maabara na vifaa vingine katika shule hizo.
“Hapa Meatu, takwimu za serikali ni hizi hapa, zinasema kuwa wilaya yenu ilikuwa na wanafunzi 8,461, waliofaulu walikuwa 1,962 na waliobaki takriban 6,000 wametupwa mitaani. Hii ndiyo sera ya CCM inayojivunia ya Kasi Mpya, Ari Mpya na Nguvu Mpya, sasa wamekuwa na Nguvu Zaidi,” alisema Dk. Slaa.
Kwa mujibu wa Dk. Slaa, CHADEMA ikiingia madarakani itahakikisha elimu ya awali kutoka darasa la kwanza hadi kidato cha sita itakuwa bure, afya itatolewa bure huku akisisitiza kuwa itafuta kodi ya vifaa vyote vya ujenzi ili kuwawezesha wananchi kujenga nyumba bora.
“Wapo wanaohoji tutapata wapi pesa, sisi tunasema fedha zipo, tatizo CCM haina vipa umbele. Kwenye suala la kufuta vifaa vya ujenzi, tutaangalia uwezekano wa kutoa ruzuku kwa viwanda vinavyozalisha vifaa vya ujenzi ili mabati, nondo, sementi, misumari, rangi na vingine vipatikane kwa bei ya chini,” alisisitiza.
Kabla ya mkutano huo, Dk. Slaa alifanya mikutano ya kampeni katika Kata ya Kidarafa, Jimbo la Iramba Mashariki, mkoani Singida na Bukundi, Wilaya ya Meatu, ambapo aliwaomba wananchi kuipigia kura CHADEMA kwa ajili ya kubadili hali zao za maisha. Kwa upande wake, mgombea mwenza wa CHADEMA, Mzee Said Mzee, aliwataka wananchi wa maeneo hayo kutokubali kuuza shahada zao za kupigia kura na kuacha kufanywa mabango ya CCM kwa kuvaa fulana zenye picha ya Kikwete. “Msikubali kuuza shahada zenu kwa sh 5,000 au kwa kanga, fulana na kofia yenye picha ya Kikwete. Tunawaambia kabisa kwamba mwaka 2010 hatudanganyiki,” alisema Mz
 
Alisema anashangazwa na ahadi nyingi zinazotolewa na mgombea huyo wa CCM ikiwamo ya kutaka kujenga viwanja vya ndege, wakati serikali yake haina hata ndege moja baada ya kuuawa Shirika la Ndege la Tanzania (ATC).
"Lakini hata kama kungekuwa na ndege, Watanzania wa Wilaya ya Meatu mtapanda hiyo ndege kusafirisha ng'ombe wenu sokoni? Kina mama wajawazito watapanda ndege hizo kwenda kupata matibabu? Ndiyo maana huwa nasema Kikwete si makini, kwa nini hizo pesa asizitumie kujenga zahanati, kununua magari ya wagonjwa na kujenga barabara?" alihoji Dk. Slaa.


NILISEMA JANA JAMANI ATUITAJI NYETI ZA SILAA TUNAITAJI HII KICHWA YAKE ILIOTENGENEZWA NA KUREKEBISHIKA NA SI MNAZOZIITAJI NYIE SISIEM....KEEP T UP DK
 
Back
Top Bottom