Mmasai na fundi redio.

Bra-joe

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
1,562
986
Siku moja redio ya mmasai ilikuwa haishiki stesheni, kila akijaribu ililia sshiii sswiii, akaamua kuipeleka kwa fundi, fundi baada ya kuikagua alikubali kuitengeneza kwa sh 3,000. Akamwambia mmasai aje baada ya masaa3, mmasai alipokuja kuchukua redio yake, fundi akamwambi bado, kwani kuna kifaa kimeharibika, gharama yake sh7,000. Mmasai akasema haiwezi hiyo gharama, akamwambia fundi arudishie vitu vyote ndani ya redio kama vilivyokua mwanzo. Fundi alipomaliza kurudishia vitu akamkabidhi mmasai redio yake, mmasai aliipokea na kujaribu kutafuta stesheni, kilichomshangaza zile kelele za sshiii sswiii zilikuwa hazipo, yaani kimya kabisa, ndipo alipomwambia fundi anataka arudishiwe zile kelele za sshiii sswiii kama zilivyo kuwepo mwanzo, kulizuka ugomvi mkubwa sana baina ya fundi na mmsai.
 
Ugomvi tena, kwani hawa jamaa siku hizi hawatembei Na zana viunoni? Huwa hawana mjadala majuzi pale Feri Mtu kafyekwa mikono kisa alimtupia vijimaneno vya kashfa mwana lubega mmoja..
Nichukue nafasi kuuliza swali mweshimiwa sana.. Hivi kuna Konda mmasai?!?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom