chiko
JF-Expert Member
- Feb 24, 2010
- 580
- 245
Wana JF
Kuna dada wa 'Kilokole' ananisumbua sana. Alianza kwa kuninunulia Biblia ndogo ya mfukoni na kunishawishi niache dhehebu langu la Kikatoliki. Yeye anasema ameoneshwa katika maono kuwa napaswa kubadilika kabla ya mwaka huu kuisha na Mungu amwemwahidi 'kupanda cheo na kupata faraja' iwapo nitamkubalia ombi lake.
Kama haitoshi, kila siku lazima anitumie meseji za neno la Mungu na nyimbo za injili.
Waungwana nishaurini, nifanyeje?
Wanikumbusha rafiki yangu, kitambo kidogo. 'Jamaa hakuwa mkristo, lakini kajitupa sana kwa Mtawa (Sister), rafiki yangu kajifanya ameokoka...ikifika jumapili, Biblia ya kizungu kwapa la Right, Biblia ya Kiswahili kwapa la Left. Alipomkamata huyo Mtawa, kajaza Boli, alafu akamuoa...akarudi kwenye dini yake..Laaahhha. Akawa akijipiga kifua mbele yetu.....Shemegi yenu huyu, nilimnyanganya YESU!!!!!!, Nikakubali, kweli IBILISI ni MTU!!!!