Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mlipuko wa mabomu ulijulikana kabla ila ni usembe tu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Akiri, Feb 19, 2011.

 1. A

  Akiri JF-Expert Member

  #1
  Feb 19, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,347
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 38
  Wakuu nina ndugu yangu wa karibu ambaye ni mwanajeshi anasema taarifa za kulipuka kwa hayo mabomu zilijulikana tangu siku ya j'tatu . askari wa wadogo ambao ndiyo hasa walinzi wa hayo maghala waliona dalili za milipuko na wakatoa taarifa kwa wakubwa wao ,ambao nao wakatoa taarifa ngazi zinazofuata. akasema mpaka jumanne walikuwa bado hawajaambiwa ni nini cha kufanya na juma tano ikawa sikukuu hivyo walikuwa wanasubiri mpaka siku ya alhamisi ndipo waambiwe nini cha kufanya .

  na pia kaniambia baada ya milipuko wanajeshi wengi wamekufa sababu waliambiwa waingie kwenye hayo maghara na wachukue hayo baadhi ya mabomu na wayaelekeze upande wa juu ili kuepusha madhara ya kulipua kambi nzima. japo hajaniambia ni idadi gani ya hao wapiganaji wetu waliopoteza maisha yao.

  jamani urasimu huu mpaka lini ona unavyotugharimu mtu anapelekewa taarifa muhimu mara hayopo ofisini na taarifa zinabaki mezani kwake. kama habari hizi zinaukweli kazi tulionayo ni kubwa sana
   
 2. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #2
  Feb 19, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 6,475
  Likes Received: 172
  Trophy Points: 63
  Mkuu kama hii ni kweli basi tuna kazi ya ziada ya kufanya! Bila kusahau nakuomba usahihishe huu msemo USEMBE/ni UZEMBE halafu na hii pia ULASIMU/ni URASIMU!
   
 3. A

  Akiri JF-Expert Member

  #3
  Feb 19, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,347
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 38
  asante mkubwa nashukuru sana nitasahihisha
   
 4. m

  mamakunda JF-Expert Member

  #4
  Feb 19, 2011
  Joined: Jul 4, 2010
  Messages: 371
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama ni kweli, basi aliesababisha urasimu huo awajibishwe!
   
 5. A

  Akiri JF-Expert Member

  #5
  Feb 19, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,347
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 38

  hayo maneno uliyonisahihisha mbona siyaoni?
   
 6. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #6
  Feb 19, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 6,475
  Likes Received: 172
  Trophy Points: 63
  Akiri soma heading yako halafu nenda kweye thread yako soma kwa umakini utajua ninini cha kusahihisha!
   
 7. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #7
  Feb 19, 2011
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 3,959
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 63
  Mleta mada angekuwa amefanya kazi nzuri kama angeweka hapa nalaka ya hiyo taarifa. Naamini taarifa zinaenda kimaandishi na zinapigwa mhuru wa lini ilipokelewa, angeiweka hapa ili tuitumie kuwalazimisha waliosababusha mauaji wajiuzulu
   
 8. mgt software

  mgt software JF-Expert Member

  #8
  Feb 19, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 8,896
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 83
  nakala kweli utaipata eneo la jeshi kabla ya kufika unaweza kula mgwala tano na kuruka kichura mara hansini, hata waandishi ka saeed Kubenea hawezi fika, si ulisikia ya juzi hakuna mtu wa kujiudhuru, jeshi ni jeshi hakuna siasa wanasiasa ndio wanajihudhuru,
   
 9. Avatar

  Avatar JF Gold Member

  #9
  Feb 19, 2011
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 674
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 18
  Mh!.. Urasimu everywhere!..
   

Share This Page