Mlipuko wa CHADEMA watokea Mtaa wa Mavurunza, Kimara

WanaJF

Jumamosi iliyopita kulitokea Mlipuko wa CHADEMA kwenye Mtaa wa Mavurunza, Kata ya Kimara ikiwa ni muendelezo wa kuimarisha, kuendeleza na kudumisha CHADEMAambako kulifanyika Mkutano wa hadhara wa CHADEMA Tawi jipya la Mavurunza kama ni Maandalizi ya uzinduzi rasmi na harambee kwa ajili ya ofisi ya Tawi hilo inayotarajiwa kufanyika Jumamosi ya wiki hii kwenye Mkutano mwingine wa Kata ya Kimara. Awali, Mh. Dr. Wilibroad Slaaa alitarajiwa kuwa Mgeni rasmi kwenye Mkutano huo wa Kata Jumamosi ya wiki hii ingawa bado haijathibitika kama atahudhuria au atateuwa mwakilishi wake.

Akisoma Risala Mwenyekiti wa Tawi hilo ambaye pia ni muasisi wa Tawi hilo na mwanaharakati wa Maendeleo, kwenye Mkutano huo wa hadhara mbele ya Mgeni rasmi Diwani wa Kata ya Kimara Mh. P. Manota; Mwenyekiti huyo alisema katika jitihada za kuhamasisha wananchi kujiunga na CHADEMA, tayari walipatikana wanachama zaidi ya 150 na bado kuna wananchi wengi wameshawishika kujiunga na chama hicho. Aidha, kwenye mkutano huo kulikuwa na wanachama wapya wengi sana walijitokeza kujiunga na CHADEMA ikiwa ni pamoja na wajumbe wa mashina kutoka CCM. Hadi kufikia usiku bado wananchi waliendelea kuorodhesha majina yao na kuchukua kadi za CHADEMA kutoka kwa Mwenyekiti wa Madiwani wa CHADEMA mkoa wa DSM.
Mkutano huo wa Jumamosi iliyopita ulihudhuriwa pia na makamanda wengine ambao ni Madiwani (CHADEMA) kutoka kata za Saranga, Makuburi, Ubungo, Sinza, Viti maalum na Mwenyekiti wa Wilaya Kinondoni. Makamanda hao ndio waliokuwa walipuaji wakuu wa masuala yanayohusu hali mbaya ya uchumi wanchi hii kutokana na Utawala wa Chama tawala (CCM) ikiwa ni pamoja na kuanika hadharani tuhuma za kifisadi dhidi ya Diwani wa zamani wa Kata ya Kimara (CCM) na Mwenyekiti wa Mtaa huo wa Mavurunza (CCM). Mikutano hii ni sehemu ya Operation Ondoa CCM Mkoa wa Dar es Salaam.


WITO: Ukiwa kama Mwanachama, Mdau na Mwanaharakati wa Maendeleo unaombwa kuhudhuria Mkutano wa Kata ya Kimara Jumamosi ya wiki hii tarehe 25 Februari 2012 kwaajili ya uzinduzi wa matawi kadhaa ndani ya Kata hiyo.
Taarifa kamili kuhusu mkutano huu ikiwa ni pamoja na Mgeni rasmi, Ratiba na namna ya kufika kwenye eneo la tukio nitawasilisha mapema kesho. KARIBUNI SANA…!



Nawasilisha….!

Mkuu ni kweli huko kimara kuna muamko mkubwa sana. Kuna watu wanasema kwamba wakaazi wengi wa Kimara wanatoka kasikazi lakini mimi siamini. Ni muamko tu wa mahaba kwa CHADEMA.
Ila kitu kimoja muhimu mshaurini mwalimu Manota aache jazba za kisukuma na kikurya; hilo tu basi.
 
Aisee mi nilivyoona hicho kichwa ilibidi nimpigie ndugu yangu aliyeko huko kimara mavurunza. Nimemuuliza kama kweli kulitokea mlipuko akashangaa kwani hana habari hiyo...Kumbe mlipuko anaozungumzia huyu jamaa sio ule niliokuwa naufikiria!

Safi mlipuko
 
Back
Top Bottom