Mlipuko mkubwa watokea kwenye Kanisa Katoliki Arusha, watu kadhaa wajeruhiwa

Status
Not open for further replies.
ehhh ehhh ehhh CHADEMA sasa mmezidi, wananchi walidhani gaidi Lwakatare akiwa mahabusu hali ya ugaidi itatulia, kumbe gaidi Lwakatare ana wafuasi wengi? naona wanazidi kutekeleza maagizo ya babu wa CHADEMA kwa kasi iliyo tukuka.

Mahakama kazeni buti ili muhukumu hiyo kesi ya huyo gaidi Lwakatare mapema, maana hukumu ikiwa kali (kama vile kunyonga hadi kufa) inaweza kupunguza au kutokomeza kabisa vitendo vya kigaidi hapa nchini, maana magaidi wataogopa kutii maagizo ya babu.
 
Kwanini usilizuie wakati linarushwaaa? Umeliona?

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Habari nilizozipata sasa hivi toka Arusha, ni kuwa watu kadhaa waliokuwa wanahudhuria ibada maalum ya uzinduzi wa Parokia katoliki ya Olasiti wanaaminika kufa na wengine wengi kujeruhiwa, baada ya watu wanaoaminika kuwa ni wa itikadi tofauti kuingia na kurusha bomu kwa mkono na kukimbia na gari lao haraka. Vilio na simanzi vimetawala katika eneo hilo ambalpo pia damu zimetapakaa kila mahali.
habari zaidi zitatolewa baadaye.........
 
Mungu saidia lakini kumwachia Mungu kila kitu si Vema ni lazima kanisa lichukue Uamuzi.
 
Yeah! kuna uwezekano huo -- maana under CCM kila kitu kinawezekana! Si kuna chaguzi za u8iwani wa kata nne ambazo CCM watazipoteza kwa kishindo.

Hivyo mtasikia chaguzi zimeahirishwa na FBi wataitwa kuchora mtuhumiwa na mchoro utakaochorwa utakuwa ni wa yule hasimu mkubwa wa CCM hapo Arusha - you know whom!
Fbi si wapo hapo arusha kufuatilia money laundry,pengine watasaidia hapo.
 
Kuna watu watatokwa povu kwa kauli yako, lkn ukweli ndio huo Raisi dhaifu kuliko wote duniani ndiye katufikisha hapa!!
Yuko bize na kuwatumia amashushu kwenye mambo ya kijinga kama vili kumfuatilia Dr Slaa toka Iringa ha DSM, Huku magaidi wa kweli wakijiimarisha!!!

Yaani baada ya kugundua kwamba Ushahidi wa Lema kuwa Kikwete ni mdini ulishafika Dodoma pasipo wao kutegemea naona wameamua kuanzisha episode mpya kuuzuia asiufikishe kwa spika.
 
Leo ndiyo ilikuwa inazinduliwa kuwa Parokia rasmi leo, katikati ya ibada bomu hilooo!!! Kha!
Mungu atusaidie sana kwa kweli
 
watu wawili waliovalia kanzu walishuka kwenye gari na kurusha bomu na kukimbia na gari

Ukisoma makala hayo hapo chini unaweza kupanua mtazamo wa nini kinaendelea kama kweli kwa tukio hilo.


''Tukiweka kando suala la Lwakatare, wakati ninafahamu kwa nini polisi wamemkamata kiongozi huyo wa CHADEMA, ninashindwa kabisa kuelewa kwa nini kanda kadhaa za video zilizozagaa huko YouTube zilizorekodiwa hadharani zikimwonyesha Ustaadh Ilunga akihamasisha mauaji ya maaskofu, mapadre na walei wa Kikristo hazijawafanya polisi wamkamate''.
 
Aisee! Is this true. Poleni wakazi wote wa Arusha! Walioko karibu na eneo la tukio, endeleeni kutujuza ukweli na uhalisia unaondelea hapo, with supportive facts. Reporting ya matukio kama haya yanahitaji umakini na uangalifu, kuepuka upotoshaji na kupindisha ukweli.

Hivi uchunguzi juu ya mlipuko wa kitu kilichodhaniwa kuwa bomu nyumbani kwa kiongozi wa BAKWATA uliotokea mjini Arusha umefikia wapi? Yet no one held responsible! Kimya na bado tukio jingine la namna hiyo linatokea tena?

Closely and seriously following up
 
na pia fbi wapo arusha kuchunguza fedha chafu kuna watu walikuja walikua wawevaa kanzu wakashuka na kurusha bomu

......Maaskofu pia si wamevaa kanzu !? Mmewasachi na wao ?
Gaidi bado ameshikiliwa, sasa ni nani anaendeleza ugaidi ?
Serikali imekuja (Magesa Mulongo) ?!
 
Watanzania wenzangu hasa Vijana mnaotumia akili zenu kwenye kila jambo ni Siasa basi......Stop It!
Tunatakiwa kulaaani vikali tukio hili na kuzidi kuliombea Taifa letu liwe na Utulivu hasa kwenye masuala ya Dini.
Mambo ya Chadema au RC Mulongo ayahusiana kabsa hapa!
 
Kwanini usilizuie wakati linarushwaaa? Umeliona?

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums

Hivi unawezaje kulizuia bomu lililokwisha kufyatuliwa likisubiri kutua ktk ardhi na kulipuka?,haya tunayoyazungumzia hapa kesho yanaweza kukukuta wewe au ndugu ktk familia yako hivyo usifanye mzaha tena kwa makusudi.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom