Mliopo arusha: Ni kweli AICC inavunja nyumba za makazi?

solution

JF-Expert Member
Apr 6, 2009
492
99
Mwanangu amepewa barua ya kuhama makazi anayoishi kwa kisingizio yanavunjwa na anatakiwa kuhama si chini ya miezi sita.

Anaishi nyumba za AICC SOWETO ... nini kinaedelea?

AICC hawawezi kujenga makazi na kuhamishia wakazi wake kama ilivyokuwa NHC dar es salaam?

Hawana sehemu za kujenga makazi mapya? Kuna uhalali gana kwa kitendo hili?

Nani yuko nyuma ya zoezi hili?

 
Ni kweli kuna notice zimetolewa kwa wakazi wa AICC Soweto lakini si wote. Ni wakazi walio barabarani upande wa Florida, wanataka kujenga majengo ya biashara na sio makazi tena, alafu watawahamisha na wakazi wengine kama mradi ukiwa fit.
 
Binafsi sijasikia suala hilo, japo huenda lipo!
Ila kwa mtazamo tu, nitapongeza sana iwapo nyumba zile zitavunjwa!
Kota za AICC soweto ni vibanda vya kizamani sana vilivyo katikati ya mji, vinatia aibu sana!
Ukiingia kwenye apartment ya familia utakumbana na maajabu ya Musa, na huwezi kuamini kama ni family inaishihumo...hata kwa mtu mmoja (single) kukaa humo bado hailipi!
Kama wana mpango huo wafanye haraka sana kuondoa uchafu ule mjini!...
Kwa suala la huyo nduguyo, naamini wameshawapa notice ya kutosha kabla ya kuwaondoa!
Cha msingi ni prior information ikiwajulisha kuwa hautapokelewa mkataba mpya as from date so and so!
Waingie tu mtaani wakapange mjomba, kwani wanaopanga wana mkia?
Kama watajenga zingine , well and good, zitakuwa available kwa public!
 
Wana eneo kubwa sana ingependeza kama wangejenga kitu kinachofanana na mlimani city ili kupunguza tatizo la nyumba za biashara linaloikabili Arusha. Hivi sasa Arusha kuna watu wengi wana mitaji lakini hakuna maeneo ya kupanga, na ukipata kuna ufisadi wa ajabu unaoitwa "kilemba" na ni pesa nyingi ya kutosha kununua computer za internet nzima unampa mtu ambaye wala siyo mmiliki wa hiyo nyumba
 
Mimi nimesikia AICC wamebinafsisha eneo hilo na kinachotakiwa kujengwa hapo ni Mall yaani ile supermarket kubwa inaitwa Nakumat Supermarket! Hata mimi naunga mkono eneo hilo livunjwe kwakua watu wanaoishi kwenye nyumba hizo Huh! nyie angalieni kwa nje tu ukiingia ndani na ukaona maisha ya watu wanaoishi si mchezo yaani mpaka sehemu ya store wapangaji wamefanya ni vyumba vya kulala.
 
Back
Top Bottom