Mliona msajili wa vyama alivyobanwa TBC?

EDOARDO

Senior Member
Oct 4, 2010
115
13
Nilikuwa naangalia kipindi cha "This Week In Perspective" kinachorushwa na TBC1, na mada ilikuwa "FUNZO LILILOPATIKANA KATIKA UCHAGUZI MDOGO ARUMERU MASHARIKI". Hii ni baada ya kufanya tafsiri toka lugha ya kimombo.

Miongoni mwa maswali aliyoulizwa Mheshimiwa huyo na kujikuta akitokwa jasho ni pamoja na:
1. Siasa ya vyama vingi ilipoanza Tanzania, vyama vya siasa vilitakiwa kusajiliwa. Je, CCM nayo ilisajiliwa tena? Jibu likawa "No". "Why?" Jibu likawa "Because it was already there". Mjadala mrefu uliendelea baada ya hapo.

2. Wewe ndiye alinukuliwa na vyombo vya habari akimtaadharisha Lema asiende Arumeru Mashariki. Ni kweli? Jibu Likawa "Exactly!". Ulifanya hivyo kwa manufaa ya nani? Jibu, "That order was given by Wazees called "Washili" from that area, so I just wanted to make sure that all political parties are respecting culture of that place".

3. Mbona mimi nilikuwa huko muda wote wa kampeni na Lema alikuwepo na hao wazee hakumfanya chochote? Jibu, " I don't know what Happened"

Wageni wengine walikuwa kina Prof. Baregu, Dr. Waitama na mmoja kutoka UDSM. Hili linatufundishanini?
 
Nashukuru mkuu wa kurekebisha hilo jina. Huyo Dr. yuko vizuri sana!
 
Sijawa na uhakika kinarudiwa lini, ila nafuatilia mkuu kisha tutajuzana!
 
Dr kitila Mkumbo nae alikuwepo.kiukweli Tendwa alibanwa sana..kwa mara ya kwanza jana nimemuona tendwa akipata kigugumizi kila sekunde..
 
Tendwa ni mtu wa majivuno sana .Pia nafasi aliyonayo kwa mshike mshike wa sasa hawezani na hii kasi.
 
Tatizo la Tendwa ni kuwa ingawa nafasi hiyo ya Msajili anapaswa kutekeleza majukumu yake akiwa huru, badala yake anaabuse hiyo nafasi kwa kujiegemeza kwa magamba, miongoni ya grave mistakes alizofanya akiwa registrar wa vyama ni hilo la kumkataza Lema asiende kwenye kampeni Arumeru, kwa madai kuwa Wazee wa huko watamdhuru, sasa amepata aibu ya mwaka, kwa kuwa Lema alikuwepo Arumeru fulltime, na hakupata madhara yoyote!!
 
Ni ajabu kutegemea utendaji mzuri kutoka kwa msajili wa vyama ambaye loyalty yake iko kwa CCM.
Amewekwa pale kutekeleza matakwa ya mabwana wakubwa haijalishi ana uwezo na vigezo au la.
Conflict of interest at its highest degree.
 
Kipindi kilikuwa kizuri sana na kilionyesha upeo na uelewa wa wageni kwenye mazungumzo. Tatizo la mkuu Tendwa ni ushabiki wa kisiasa ambao umefikia mahali anajiabisha si yeye tu bali hata yule aliye mteua na wale anaowashabikia maana kuna vitu anashabikia mpaka inakuwa kero hata kwa anaowapigia debe.Jaji anashindwa kunyumbulisha siasa na uhalisia wa mambo yalivyo tokea Arumeru. Panelist wote walikuwa objective isipokuwa jaji Tendwa pekee maana kwangu mie kila alichokuwa anajaribu kuelezea kiligeuka kuwa chukizo, fikiria suala la wazee wa Arumeru na Lema. Ukimsikiliza katikati ya maneno aliyokuwa anatamka yalijaa hila, giriba (it was pure cooked story) ili kuharibu haiba ya Lema mbele ya wanaArumeru lakini walianza na mungu na walimalinza na mungu na alisikiliza kilio chao ndo maana wakazi wa Arumeru walifanya chaguo sahihi.
 
Back
Top Bottom