Mlioichagua CCM nimewasamehe lakini msirudie

Joblube

JF-Expert Member
Mar 4, 2011
369
151
Pamoja na kuwa CCM haikushinda kihalali, lakini ndugu zetu mlioichagua CCM mmesaidia wao kupata njia ya kuchakachua na kuweza kurudi madarakani. Matokeo yake mateso tunayopata sasa na mbaya zaidi dereva wetu hana tena uwezo wa kutufikisha salama, naamini tutafika lakini kwa mateso na uchungu kama tunavyopata sasa. Cha ajabu mateso haya tunapata wote nyie mliochagua CCM na sisi ambao tuliikataa wote Mangana kama wazanaki wanavyosema.

Mimi siwalaumu magamba nawalaumu nyie mlioichagua CCM angalia
sasa tuapigika wote, kapelo na Tshirt mlizopewa zinamewasaidia nini. Lakini kwa ujumla wake kutenda kosa sio kosa bali kurudia kosa. Mimi binafsi nimewasamehe na nawapenda kwa dhati kabisa kwa kuwa na jua ni ujinga tuu ulisababisha mkachezewa cheupe chekundu mkaingia kichwa kichwa ikala kwenu mbaya zaidi na kwetu.

Ndugu zangu 2015 tusikubali tena propaganda za magamba na tuonyeshea kuwa ule msemo wao wa kututusi kuwa Watanzania ni wepesi wa kusahau sio kweli, tuwachane kwa kishindo ili wakichakachua ishindikanea kabisa.

Mungu ibariki Tanzania pamoja tutafika.
 
Heee wewe ndugu, hatusubiri mpaka 2015. Nani kakuambia Vasco Da gama Tutamning'iniza kama Mubarak wa Misri, Egypti.

Wanaharakati wa Tanzania wamelala sana, tumechelewa sana kumtimua ikulu na Watanzania tu waoga tena mazoba.

Tukiandamana wanasema oo uchochezi oo amani. Kumbe wanataka amani ili waendelee kutafuna kwa ulaini.

Mhh na hawa wabonge wa magamba!!! thinking by using masaburi

Wabonge wa magamba ni kama wildebeest, yaani wanaburuzwa na wanaacha vigogo wanatafuna nchi kama akina Luhanjo, Msekwa na vasco da gama wao
 
Pamoja na kuwa CCM haikushinda kihalali, lakini ndugu zetu mlioichagua CCM mmesaidia wao kupata njia ya kuchakachua na kuweza kurudi madarakani. Matokeo yake mateso tunayopata sasa na mbaya zaidi dereva wetu hana tena uwezo wa kutufikisha salama, naamini tutafika lakini kwa mateso na uchungu kama tunavyopata sasa. Cha ajabu mateso haya tunapata wote nyie mliochagua CCM na sisi ambao tuliikataa wote Mangana kama wazanaki wanavyosema.

Mimi siwalaumu magamba nawalaumu nyie mlioichagua CCM angalia
sasa tuapigika wote, kapelo na Tshirt mlizopewa zinamewasaidia nini. Lakini kwa ujumla wake kutenda kosa sio kosa bali kurudia kosa. Mimi binafsi nimewasamehe na nawapenda kwa dhati kabisa kwa kuwa na jua ni ujinga tuu ulisababisha mkachezewa cheupe chekundu mkaingia kichwa kichwa ikala kwenu mbaya zaidi na kwetu.

Ndugu zangu 2015 tusikubali tena propaganda za magamba na tuonyeshea kuwa ule msemo wao wa kututusi kuwa Watanzania ni wepesi wa kusahau sio kweli, tuwachane kwa kishindo ili wakichakachua ishindikanea kabisa.

Mungu ibariki Tanzania pamoja tutafika.

Kwa kifupi sana, unataka kutuambia nini hasa??
 
inabidi kina ritz, mwita25, GeniusBrain, Mlengo wa kati, Bollo yang, Bi zakia, Muhadhir,edina na suzana na wenzao waje hapa wakushukuru kwa msamaha uliowapa, na waseme asante kwa msamaha!
 
Back
Top Bottom