Mlioagiza magari mkailipa tbs mkachukue hela zenummeibiwa :mkurugenzi akiri akuna ofisi nje ya nchi

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,720
21,779
Unaweza hisi hii nchi ni zaidi ya jehanum jamani basi tu tunapata kauwezo cha kununua ugali na mkate jamani
mkurugenzi wa wa tbs amekoswa koswa kuchapwa ngumi na mbunge mmoja kwenye kamati ya bunge pale
alipokiri kuwadanganya wabunge alioenda nao huko hongkong na korea na kusema akukuwa na ofiisi za tbs ila alizowaonyesha alizipata gafla kwa ajili ya safari za wabunge

mbunge huyo machachari amesema huyu mzee hana adabu kabisa ni m shenzi kabisa mkurugenzi gani anatuchukua hapa mpaka nje tunapanda first class alafu mwisho wa siku anasema ati tumsamehe yaishie huku kwa kuwa tbs awakuwa na ofisi ni mtu alikuwa na oisi yake mkononi watu wanampeelekea hela wanasepa

mkurugenzi huyo ambae inasemekana alipojua wabunge wanakwenda nje kukagua alimjulisha rafiki yake mmoja ambae alitafuta uchochoro wa ofisi ambapo walipofika awakumkuta hata mfanyakazi wala mafaili zaidi ya kukuta imefungwa...inasemekana alipopigiwa mhusika wao waliomweka mkurugenzi alidai jamaa apatikani hayo hayo yakaendelea hongkond na korea na ilibidi waairishe kurudi baada ya kuona nchi zaidi ya tatu wamedanganywa hata hizo tulizoambiwa twende azina haja tena alisema mbunge huto

ndugu zangu watanzania huyu baba alidiriki ksuema kila gari lazima liwe limelipiwa tbs na hii ni kutokana na hili aliskiri kusema wana ofisi uk..usa na sasa wameanza kukodi ofisi nchi za asia ...hakika huyu ni zaidi ya muuwaji lakini kwakkuwa anakula na wizara hjusika na hata katibu wa wizara husika alidiriki kutaka kumtetea akatukanwa na mbunge mmoja ndipo alipoamua kukaa kimyaaa

hii ni aibu ya ajabu na shame ya serikali na je nimejiuliza huyu kama anaweza kudiriki kudanganya wana ofisi nje na watu wanalipa kwa nini mliolipa msichukue nafasi hii kwenda tbs kuchukua hela zenu..hakuna ushahidi hata kidogo wa hela zilizolipwa kuja dar tbs office na hili mbunge amesema ameshindwa kuamini kwa nini katibu wa wizara husika anamtetea mpaka sa sa
 
ndio hivyo mkuu

hii nchi bwana,tukisema tunaelezwa kuwa tunalalama sana,ili watu wale kiulaini,kila mtu ofisini kwake anakula kamkate alichopewa na MH RAISI
 
Sijaelewa,
Kwa sie wadau wa magari ya kijapani hua twalipia JAAI Inspection ambao twaamini wapo on behalf of TBS, sasa hapa imekaaje???
 
Pdidy asante kwa kuileta hii. Mimi nimebakia kucheka tu. Mishe mishe mpaka wazee...nani hajatapeliwa sasa? Inasikitisha sana
 
Utashangaa mtu kama huyu anapeta tu mpaka anastaafu. Hii nchi imeoza kabisa! Sasa kama tbs ambayo tunategemea kwa viwango vya kila bidhaa inafanya haya usalama wa nchi na wananchi upo wapi? Hivi UWT(TISS) huwa wanafanya kazi gani?
 
inakera sana inakuwaje hadi mda huu hajafukuzwa kazi
kumbe TBS ndo hao hao wanaoidhinisha matumizi ya bidhaa feki
wabunge tupate majibu mapema na awajibishwe ikiwa ni pamoja na kufilisiwa na kufikishwa mahakamni
mashagidi ni wabunge wenyewe.
loh bahati yake huyo mbunge alipaswa kumla kichwa na teke kabisa
 
Tulieni hivyo hivyo Watanzania muendelee kunyolewa kwa wembe butu mpaka muote sugu...na bado mpaka atokee masiha au mkombozi wa nchii tutakuwa tumeumizwa sana...mengi tu yapo njiani mtayagundua....
 
Halafu eti tunasubiri mpaka Bunge lianze ndio mlolongo wa Protocols kama za kina Jairo uanze,
Yaani Polisi wako wapi mpaka huyo Babu hajakamatwa??
Ilitakiwa muda huu awe ndani kwanza ili Jumatatu afikishwe mahakamani, mambo ya Bunge hayo yatafuata Baadae Na Protocols zake!
 
Huyo afilisiwe ale na risasi ya ubongo na wote alioshirikiana nao, hawezi kuwa peke yake.
Dada FaizaFoxy umenena, hayo Wachina wanayafanya kweli, na wahujumu uchumi wote wanaangamizwa, lakini hapa, sijui. Wakati tukitafakari kama wahujumu uchumi kama Ekelege wanaweza kuangamizwa, ebu tujikumbushe kidogo sakata hili: Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (PAC), Deo Filikunjombe amemshutumu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Charles Ekelege kwa utendaji wake mbovu, uliojaa utapeli ambao Kamati hiyo iliugundua katika ziara nje ya Nchi ya kukagua kampuni za ukaguzi wa magari yanayoingizwa nchini. Filikunjombe alikuwa anazungumza hayo katika kikao cha kamati za Bunge za Hesabu za Serikali (POAC) na PAC cha kujadili utendaji wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dar es Salaam. Naye Mbunge Lugora akielezea kikao hicho jinsi alivyoakasirishwa na ubabaishaji wa Ekelega, na kuamua kumrushia konde ambalo ( kwa bahati mbaya) lilidakwa na Filikunjombe wakiwa Ughaibuni baada kamati kupewa sumu feki ya kampuni ya nje inayokagua magari yanayoingizwa nchini. Picha hapa chini ni muonekano wa Ekelege kama vile anataka kulia au kuigiza Ze Komedi katika kikao hicho (picha ya 1 na 2) na Mbunge Lugora (picha ya 2) na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (PAC), Deo Filikunjombe (picha ya 4).

Ekelege 2.jpg Ekelege 1.jpg Mbunge Lugora.jpg Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (PAC), Deo Filikunjombe.JPG Source: http://kingkif.blogspot.com/2012/01
 
wapumbavu sana hawa,yaani akawasafirisha mpakahuko,hii confidence ametoa wapi kama sio anashirikiana na mafisadi???good country stupid imbecile leaders
 
DUh! Kaazi kwelikweli! Tutaendelea kweli kama nchi! Uzalendo u wapi sasa!
 
Mbona tulifundishwa uzee ni ishara ya hekima busara na uadilifu? Kama ni kweli basi watz tumeliwa. hata wazee? duh
 
Unaweza hisi hii nchi ni zaidi ya jehanum jamani basi tu tunapata kauwezo cha kununua ugali na mkate jamani
mkurugenzi wa wa tbs amekoswa koswa kuchapwa ngumi na mbunge mmoja kwenye kamati ya bunge pale
alipokiri kuwadanganya wabunge alioenda nao huko hongkong na korea na kusema akukuwa na ofiisi za tbs ila alizowaonyesha alizipata gafla kwa ajili ya safari za wabunge

mbunge huyo machachari amesema huyu mzee hana adabu kabisa ni m shenzi kabisa mkurugenzi gani anatuchukua hapa mpaka nje tunapanda first class alafu mwisho wa siku anasema ati tumsamehe yaishie huku kwa kuwa tbs awakuwa na ofisi ni mtu alikuwa na oisi yake mkononi watu wanampeelekea hela wanasepa

mkurugenzi huyo ambae inasemekana alipojua wabunge wanakwenda nje kukagua alimjulisha rafiki yake mmoja ambae alitafuta uchochoro wa ofisi ambapo walipofika awakumkuta hata mfanyakazi wala mafaili zaidi ya kukuta imefungwa...inasemekana alipopigiwa mhusika wao waliomweka mkurugenzi alidai jamaa apatikani hayo hayo yakaendelea hongkond na korea na ilibidi waairishe kurudi baada ya kuona nchi zaidi ya tatu wamedanganywa hata hizo tulizoambiwa twende azina haja tena alisema mbunge huto

ndugu zangu watanzania huyu baba alidiriki ksuema kila gari lazima liwe limelipiwa tbs na hii ni kutokana na hili aliskiri kusema wana ofisi uk..usa na sasa wameanza kukodi ofisi nchi za asia ...hakika huyu ni zaidi ya muuwaji lakini kwakkuwa anakula na wizara hjusika na hata katibu wa wizara husika alidiriki kutaka kumtetea akatukanwa na mbunge mmoja ndipo alipoamua kukaa kimyaaa

hii ni aibu ya ajabu na shame ya serikali na je nimejiuliza huyu kama anaweza kudiriki kudanganya wana ofisi nje na watu wanalipa kwa nini mliolipa msichukue nafasi hii kwenda tbs kuchukua hela zenu..hakuna ushahidi hata kidogo wa hela zilizolipwa kuja dar tbs office na hili mbunge amesema ameshindwa kuamini kwa nini katibu wa wizara husika anamtetea mpaka sa sa

Mkuu kila wizara ni uozo sijui msaada wetu uko wapi.chamsingi kuitoa serikali madarakanitu tupandishe watu wengine
 
Kuna mzee moja kwenye FUTUHI ya STAR TV anafanana sana kwa sura na huyu Ekelege na hata kwa vituko vyake. Kuna uwezekano huyu mkurugenzi huwa anafanya part time kama comedian wa FUTUHI?
 
Back
Top Bottom