Mlio kwenye ndoa kuweni makini, ona huyu alichofanywa

Uaminifu ni issue ngumu mno kwa wanandoa wa kileo. Matatizo ni mengi kwenye mahusiano kila mtu anali na mwenzake kuwa si mwaminifu. Je chanzo cha yote haya ni nini? Yafaa tujiulize kwa nini ni asilimia kubwa ya waathirika ni wanandoa na si makundi mengine? Tukifanya utafiti wa kina tutajua sababu na tukishajua sababu tuifanyie kazi naamin kiwango cha maambukizi kitapungua na vifo kwa wasio na hatia kama huyu dada navyo vitapungua
 
Mi bado siamini kuwa maambukizi makubwa ni kwa wanando; ni kwa kila mwasherati. Huyo alomkuta nae (housegirl) ni mwanandoa? Unajua wanawake wenye mimba wengi wanacheki afya zao na wengi wako kwenye ndoa ndio maana maambukizi kwa wanandoa yanakuwa overstated. Wanaume wengi wanachiti na singles. AU kwa kuwa wao ni single UKIMWI unawaogopa??? Hawa single hawana sababu za kupima ndio maana wanaonekana ni wachache wenye VVU; dada ambaye yuko single ukiona anapima jua kesha ugua;

Niliangalia documentary moja inasema wanaochukua dawa za ARV asilimia kubwa ni wanawake; ila si kuwa wanawake ndio wameathirika zaidi; ila wanaume wanaona aibu kupanga foleni ma hospitalini kuchukua dawa; leave alone kupima. Wengi wanatumia vipimo vya wake zao wakiwa wana attend clinic kujigamba kuwa wazima
 
Very sad jamani. Haya ndo yaliyopo nz ndo uhalisia ktk ndoa na mahusiano ya siku hizi. Tutulie jamani, ikishindikana kabisa basi ANTIVIRUS itumike, maana wengine wanasamaga hawawezi kutulia na mmoja.
 
RIP,shetani ndiye anayetutesa jamani,tumgeukie Mungu,hana huruma hata kidogo anafurahia sana anapokuona umeshaumia kwa kitu amabacho ulikuwa unafikiria kuwa una faidi.
 
So sad, hapo kitu cha kushukuru Mungu labda hakuna mtoto aliyezaliwa na maambukizi! Maana watoto wananiuma zaidi ya wazazi.

Ni topic ngumu sana hii, kuchagua kuaminiana au kufiatiliana.

Heri niwe peke yangu,
Heri niwe na mmoja,
Heri kubadili tabia,
Ukimwi watisha!

Asante kwa kutukumbusha!
 
na huwezi kuwa Peke yako Kaunga hii ni mambo ya nature :confused2:
 
Last edited by a moderator:
Mungu atuepushe na hili maana inauma sana kama unamwamini unamsadia lakini yeye haonyeshi kukupenda matokeo kukuleta magojwa ni aibu na nisimanzi sana ndani jamii na familia kwa ujumla
 
Habari zenu wana jamii,

Leo nina ushauri kwa wale walioko kwenye ndoa, na nimeona niwape ushauri huu kufuatia yalompata dada yangu.

Dada yangu aliolewa miaka ya 1990 na baba mmoja ambae by that time alikuwa mfanyakazi ktk shirika moja la uma. Alifukuzwa kazi, na sifahamu sababu ya yeye kufukuzwa kazi miaka ya 2000. Toka hapo sister kwa upendo aliishi na shemeji na hakuwahi kumsimanga kwa kutokuwa na kazi na mahitaji yake yote yalitimizwa na sister.

Sister alikuwa mfanyakazi wa benk na kwa kweli kifedha alijiweza. Alimwamini sana mumewe na maisha yao yalikuwa ya upendo na amani. they had 4 kids. Wakati dada akimwamini sana mumuwe, kumbe mumewe alikuwa akifahamika mtaani kwa jina la POPOBAWA! Alikuwa MALAYA wa kupindukia! All those days ni kama sister alikuwa kafungwa akili kwani hata siku moja hakuwahi dhani kuwa the famous popobawa pale mtaani alikuwa ni mumewe. Alikuja kupoteza imani na mumuwe baada ya kumkuta usiku akufanya ngono na house girl wao jikoni.

Hofu ya kupata maambukizi ya Ukimwi ilitawala maisha yake, na hakuchukua muda aliugua na kufariki kwa VVU.

USHAURI: Kuna slogan moja ya wanajeshi, inasema TRUST NOTHING SUSPECT EVERYTHING! Pamoja na kuwa mnaaminiana sana na waume/wake zenu lakini jaribuni kuwa makini sana katika huu uaminifu kwani wanandoa wengi wamekuwa wakitumia neno kuaminiana vibaya! Mume hataki mke aguse simu yake, na ikitokea hivyo basi atalalamika mke wangu huniamini na wakati huo huo ana vimada zaidi ya kumi na anataka aaminike kwa mkewe.

Ni mtazamo wangu tu Mahunguchila.

So sad jamani. Kwa kweli mi hapo kwenye red ndo moto wangu, yaani nikiwa na mpenzi ntamchunguza kupita maelezo! Anayetaka kujua jinsi ya kumchunguza mpenzi wake ani PM nimpe maujanja!!
 
Hizi story ndizo ambazo Smile akizisoma kuhusu wanandoa anachanganyikiwa kabisa. Ila ukweli ni kuwa kuna mamilioni ya wanandoa wanaoishi kwa uaminifu na habari zao hazisikiki kwani hazisisimui wasomaji. Hii ni sawa kabisa na ambavyo huwezi kusikia habari za watu kula wali maharage.
 
Mi bado siamini kuwa maambukizi makubwa ni kwa wanando; ni kwa kila mwasherati.
Niliangalia documentary moja inasema wanaochukua dawa za ARV asilimia kubwa ni wanawake; ila si kuwa wanawake ndio wameathirika zaidi; ila wanaume wanaona aibu kupanga foleni ma hospitalini kuchukua dawa; leave alone kupima. Wengi wanatumia vipimo vya wake zao wakiwa wana attend clinic kujigamba kuwa wazima

Nyumba Kubwa umepigilia msumari ni kweli tupu yani mi namsikiaga wangu akiona ile kadi tu meno nje sasa kwakweli tunayo kazi kina mama...na ukute hata hizo foleni za ARV WANAPELEKEA NA WANAUME WAO MASIKINI!!!!Wanaume wengi wanajifanyaga majasiri ila ukweli wao tunaujua...
 
....uaminifu unapatikana katika Upendo. Huyo mke aliishi na mumewe kwa Upendo,....ukishaanza 'kuwa makini' unakaribisha wivu ambao ni sumu ya Upendo, ....yatabakia mapenzi tu.
 
Mtandao wa ngono ni mkubwa kuliko tunavyodhani na normally unapostukia game wewe unakuwa wa mwisho maana wengineo wote wanaokuzunguka wanakuwa tayari wameshanyaka issue.....

Honestly nyie watu hivi kweli mwanandoa unawezazuia uasiambukizwe Ukimwi kwa nguvu zako mwenyewe? Kama anavyosema nani huyu nyumba kubwa kuwa unachunga na kuchunguza?? Kweli?

Mi ninadhani kwanza ni kuntanguliza MUNGU katika ndoa na mahusiano yenu kisha KWA PAMOJA mnie mamoja ya kulindana kwa upendo. Otherwise kupigana vita hivi kwa kutegemea nguvu na mbinu zako mwenyewe kama mke au mume ni sawa na kupiga risasi hewani ukitegemea kuona simba akianguka na kufa. Ni mtazamo wangu tu na ndio maana nikasema ni sacrifice; sacrifice kila kitu for the sake of your loved ones!

Sent from my BlackBerry 9790 using JamiiForums
 
Kuna kipindi huawa naishia kUsema Namwachia Mola maana yeye ndiye alinileta duniani na anajua nitaondokaje.ina lake lihimidiwe
 
mkuu hii habari kama naifahamu vile ilimtokea dada mmoja wa kichaga aliekuwa anafanya kazi huko bank baba na alikuwa anaishi tabata.if so poleni sana ndo ubaya wa sisi wanaume kuw aviwembe bila kujali familia.
Habari zenu wana jamii,

Leo nina ushauri kwa wale walioko kwenye ndoa, na nimeona niwape ushauri huu kufuatia yalompata dada yangu.

Dada yangu aliolewa miaka ya 1990 na baba mmoja ambae by that time alikuwa mfanyakazi ktk shirika moja la uma. Alifukuzwa kazi, na sifahamu sababu ya yeye kufukuzwa kazi miaka ya 2000. Toka hapo sister kwa upendo aliishi na shemeji na hakuwahi kumsimanga kwa kutokuwa na kazi na mahitaji yake yote yalitimizwa na sister.

Sister alikuwa mfanyakazi wa benk na kwa kweli kifedha alijiweza. Alimwamini sana mumewe na maisha yao yalikuwa ya upendo na amani. they had 4 kids. Wakati dada akimwamini sana mumuwe, kumbe mumewe alikuwa akifahamika mtaani kwa jina la POPOBAWA! Alikuwa MALAYA wa kupindukia! All those days ni kama sister alikuwa kafungwa akili kwani hata siku moja hakuwahi dhani kuwa the famous popobawa pale mtaani alikuwa ni mumewe. Alikuja kupoteza imani na mumuwe baada ya kumkuta usiku akufanya ngono na house girl wao jikoni.

Hofu ya kupata maambukizi ya Ukimwi ilitawala maisha yake, na hakuchukua muda aliugua na kufariki kwa VVU.

USHAURI: Kuna slogan moja ya wanajeshi, inasema TRUST NOTHING SUSPECT EVERYTHING! Pamoja na kuwa mnaaminiana sana na waume/wake zenu lakini jaribuni kuwa makini sana katika huu uaminifu kwani wanandoa wengi wamekuwa wakitumia neno kuaminiana vibaya! Mume hataki mke aguse simu yake, na ikitokea hivyo basi atalalamika mke wangu huniamini na wakati huo huo ana vimada zaidi ya kumi na anataka aaminike kwa mkewe.

Ni mtazamo wangu tu Mahunguchila.
 
RIP,shetani ndiye anayetutesa jamani,tumgeukie Mungu,hana huruma hata kidogo anafurahia sana anapokuona umeshaumia kwa kitu amabacho ulikuwa unafikiria kuwa una faidi.

Wala msimsingizie shetani kwa mambo yenu mnayofanya. Hata Shetani mwenyewe anawashangaa maana imefikia hatua hampo kwa Shetani wala kwa Mungu !!!! Kama Mungu amekupatia mke/mume wa ndoa, na shetani naye akakupati Nyumba Ndogo/Kidumu Ki/moja, ni nani anayekupatia nyumba ndogo/Kidumu cha/ya pili, ya tatu ya nne au ya tano ?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom