Mlimani city "kama nawatch movie"!

...sio mlimani city tu, hata kwenye hii mada naona wazee wa swaga nao wamo.......wameanza kutaja ma-place makubwa ya nje........

Acha tu utawajua, yaani mtu anajikataa humu humu, halafu wanalaumu hao wa mlimani City, sijui tutafikaje?
 
Huu mjengo pembeni ya Sam Nujoma Road unambwembwe zake ukiingia mle ndani watu wanabehave kama vile si watz, kama vile hii nchi haina matatizo (umeme) watu wanaspeak kwa Swaga balaa..mara "you know" or "actually" nasema haya coz nilizungumza watu tofauti mle ndani nkasema may be huku siko tz nnayoijua,watu wako class ,happy ,watanashati ,health ! mazingira hayo yakapelekea nione kama Nawatch aina fulani ya movie!

nchi yetu nzuri, watu wazuri,wanapenda vitu vizuri, basi tu hii miana siasa inatuchanganya. ila one day yeeees!
 
Bloomingdales, Nordstrom, Nieman Marcus, Dillards, Saks Fifth Avenue, Lord & Taylor, Brooks Brothers, Coach, Talbots, Starbucks, Aeropostale, Tory Burch, Filene's Basement, Stuart Weitzman, DKNY, Cartier, etc. etc.

Hizi ni nini aisie? Au ni majina ya magari..? Duh!
 
Jamani hiyo ndio sehemu pekee ya kwenda kuShow off na kukutana na raia wengine wa type hiyo ( Ebu cheki Fairly Delights jioni watu wamejaa tu bila mpango hawajaagiza chochote hata kama ukienda mteja wa kweli unakosa siti).. Hawawezi kukutana Kariakoo sokoni au Buguruni Rozana HAKUNA ac za bure kule, then kama hao mabrazameni wanaovaavaa maplastic kuanzia viatu,jeans,miwani, vizibao, kofia, mikanda na minyororo hawezi kwenda sehemu nyingine zaidi ya Mlimani city ndio sehemu pekee hizo pigo zao hazichemshwi na jua na kuwaunguza...
 
Juzi nilikaa pembezoni mwa meza iliyokuwa na kama familia 2 hivi kulikuwa na watoto wadogo 4 wa miaka kama 4-6 hivi! Mwanangu sikusikia Kizwahili hata kimoja, isipokuwa tu pale anapopita jamaa anayewafahamu karibu! My take, Mliman City ni eneo la Middle class watu ambao they can shop na kuaford kupeleka watoto wa English Medium schools! Ukienda pale na sh 2000 yako kwa lengo la kununua uhai ya 600 na kisha urudi kwa daladala utakuwa uko mbali na pepo!
 
unaweza ukantajia mall ya ukweli bongo labda nnaweza kuta huko watu wako real???

Kama uko ulaya, au US or wherever, ambako unadhani ni pazuri kuliko Bongo, you must be very inferior! Mawazo ya namna hii yanawafanya hata huko mliko mjione mnabaguliwa, kumbe mnajibagua wenyewe sababu ya inferiority zenu. Namna hii huwezi huelewana na wazungu, sababu unavyowakimbia kwa kujibagua (because of your inferiority) na wao wanadhani unawabagua, wanakukimbia pia.
 
Hizi ni nini aisie? Au ni majina ya magari..? Duh!

Ni majina ya vibanda na mighawa tu sawa na ile iliyopo Sinza kwa remmy, sema kwa mtu ambaye hajui anaweza akadhani labda ni chain ya shopping malls kwenye universe.

Ni kama kuna mama fulani alikuwa hajui kusoma wala kuandika, alikuwa kaollewa na messnger alikuwa anafnya kazi TRC. Jioni mme akirudi amelewa ananza kutamka maneno "NASACO, TACOSHILI, etc mbele ya mke wake, halafu mke wake kesho yake akiwa na mashoga zake jirani anaanza kusimulia wenzake anasema "mmh kama baba fulani akirudi amelewa kiingereza siyo kiingereza hicho maana utamsikia anaonge,.... NASACO, TACOSHILI,..." ndiyo analogous to majina majina yanayotajwa hapa



Bloomingdales, Nordstrom, Nieman Marcus, Dillards, Saks Fifth Avenue, Lord & Taylor, Brooks Brothers, Coach, Talbots, Starbucks, Aeropostale, Tory Burch, Filene's Basement, Stuart Weitzman, DKNY, Cartier
 
Tatizo watu hawajiamini, sasa unataka kuto kujiamini kwako uambukize na wengine... watu wako hivyo unaona wana act!! maisha yamebadirika jamani na nyinyi badirikeni nchi yetu iende mbele!!
Acha watu wafurahie maisha yao kama hapo ndio wanaona panawafaa, na wewe nenda panako kufaa eti Mall ya uhakika, myfoot!!!
 
Mlimani City ni KUBWA SANA
hivi unajua humo wanajaa Tembo wangapi?

Haya utalinganisha na duka la mpemba au genge la mangi?

Mbona mnalinganisha utamu wa nyama na chungwa?

Linganisha nyama kwa nyama na chungwa kwa chungwa

Heavy weight hawezi pigana na Light weight.

Najua mnajua ni kubwa saana hata twiga anaingia na hajikunji

ha ha haaaa....uko juu bwana Kongosho
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom