Mlevi kaenda Kanisani

Malunkwi

JF-Expert Member
Jan 19, 2011
339
79
Mlevi mmoja alikuwa akilewa sana pombe hadi kusahau kwenda Kanisani siku za ibada Jumapili.

Jana Jumamosi pia alilewa sana, lakini aliweza kuamka leo asubuhi na kuamua kwenda Kanisani huku akiwa na kiporo cha pombe kichwani, hali iliyomfanya awe anasinzia Kanisani tokea misa ilipoanza.

Mchungaji aliligundua hilo hivyo akaamua kumfanyisha mfano.

Mchungaji akasema, “WALE WOOTE MNAOTAKA KUINGIA MBINGUNI SIMAMENI”

Watu wote wakainuka, isipokuwa Mlevi.

Mchungaji akairudia tena kauli yake, lakini Mlevi hakusimama kwa kuwa alikuwa kalala.

Mchungaji akabadili sentensi yake na kusema, “WALE WOOTE MNAOTAKA KUUNGUA MOTONI, SIMAMENI”

Safari hii, Mlevi akasimama haraka sana kama mwanajeshi aliyepewa amri kumbe kasikia neno la mwisho tu la ‘SIMAMENI’

Mlevi akageuza shingo, kushoto, kulia, nyuma kisha akasema, "Mchungaji sijui tunapiga kura za nini ila naona ni mimi na wewe peke yetu tu, ndiyo tumesima."
 
ha ha haaa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom