Mkwe anapokuwa mke

Esperance

JF-Expert Member
Jan 27, 2011
364
84
Wanajamvi kwa muda nimekuwa nikiumizwa na hili jambo. Mama mkwe wangu ni kama mke mwenzangu. Mume wangu anapanga budget na mama, kila kitu ni mama. juz kachukua mkopo bank nusu kampa mama afanye miradi. Nimejaribu kushare na familia mama kaja juu yeye ndio kamsomesha anastahil kuenziwa. Mume hashauriki bila kumshirikisha mamake. Hapa ana miez 6 tunakaa nae. Ni vurugu. Ushauri wandugu.
 
haya ndo matatizo ya familia zetu za kiafrika,
sasa hiyo ndoa ina raha gani kama bado mnazidi kuambatana na wazazi wenu?
Hapo wewe Esperancena mumeo mnakuwa kama bado watoto tu, si unajua mtoto kwa mama hakui.......?
Kila litakaloamriwa na mama ndo litakalokuwa.............

Hebu fanyeni kila namna mumrudishe mama kwa mumewe,
mumewe bado anamhitaji, misaada mingine itamfuata huko!
hii hali ikiendelea, matokeo yake hapo ni kununiana tu kila kukicha na kutafutiana visa tu...................
 
hata maandiko yanasema utaachana na wazazi nawe utaambatana na mkeo, nanyi mtakuwa mwili mmoja.
Huyo mumeo na mama yake wana taahira ya akili
 
Pole sana mamake..
Kweli itakuwa ngumu kumtenganisha
Mtu na mama yake sasa.. lakini binafsi
Naona kosa liko kwa mumeo. Kwa kutoongea
Nawe au kufanya vitu bila kukujulisha wewe
Mkeo..

Mkwe ye hupata kichwa
Sababu kijana yuko upande wake.
Kusema hivyo kuna sababu ambazo
Zinawafanya mama kung'ang'ania watoto
Wao wa kiume
Lakini hii ya kuingulia nyumba **** kiasi
Hiki imezidi..

Ushauri wangu washirikishe wazazi/walezi wako
Kwenye hili wenyewe wanajua zaidi cha
Kusema na kufanya. Pole sana..
 
Wamama wa kiswahili utawajua tu! kwani hukulijua hilo mapema kabla ya kuolewa?
Kaa na mume wako muongee kuhusu hili jambo. Kama anakupenda kwa dhati atakusikiliza
 
Mkuu bacha hapo kumrudisha kwake ndo kwenye sekeseke na kwake ni hapa hapa town nauli 600tsh kafika. Jinsi ya kumtoa, na mumewe hana sauti, kuolewa huku!!
 
mhh vimama vya namna hii kama vinananihii na watoto wao vinakera...pole mpenzi ila wanaume wa namna hii tangu mwanzo unamshtukia huwa mnaolewa nao wanini mngewasusia mama zao kama wasingebadili tabia!
 
Pole dada yangu,Umeolewa na Mume ambaye ni "Mtoto wa Mama"!!
Kisaikolojia Ipo mi Mama ambayo huwa haiiachii watoto wao hasa wanapokuwa na Vijisenti!!

Hapo haiwezekani kutatua tatizo hilo bila kuishia katika Uhasama,Unahitaji kufanya Uamuzi Mgumu tu dada,No easy way out!! Nina rafiki yangu Mmoja ambaye naye Mama yake Mzazi alikuwa Mtata kama huyo Mkweo!! Palikuwa Hapatoshi!!!

U have to be strong,Muonyeshe Mumeo ilo andiko halilotaja mdau hapo Juu kwamba Mwanaume atawaacha wazazi wake na ataambatana na Mkewe,siyo ataambatana Na Mama yake!! Mpe wiki mbili ajue kwamba Mambo ya Maisha yenu ni katika yako ww na yeye tu not otherwise na huyo Mama yake amrudishe,akikataa Sepa mpaka siku akiona yupo tayari kuwa "Mtu Mzima" na kuacha kuwa "mtoto wa Mama"!!
Kumbuka hapo vita haikwepeki,Usiogope,Pambana!!!

Pole kwa kupata Mume Dhaifu!!!
 
Loh dada pole sana, wa mama wa siku hizi hawataki maelewano katika familia za watoto wao. Nimeshuhudia mmoja anakaa kwa mtoto wake wa kike. Huko nako balaa, maana mke na share na mama yake kila kitu bila kumshirikisha mme wake, wakati ndiye mtafutaji. Dada ongea na mmeo asipoelewa somo ongea na wazazi wako. Ndoa ni tamu mkiishi wenyewe na kuamua pamoja.
 
Pole sana mamake..Kweli itakuwa ngumu kumtenganishaMtu na mama yake sasa.. lakini binafsi Naona kosa liko kwa mumeo. Kwa kutoongeaNawe au kufanya vitu bila kukujulisha wewe Mkeo..Mkwe ye hupata kichwaSababu kijana yuko upande wake.Kusema hivyo kuna sababu ambazo Zinawafanya mama kung'ang'ania watotoWao wa kiume Lakini hii ya kuingulia nyumba **** kiasiHiki imezidi..Ushauri wangu washirikishe wazazi/walezi wako Kwenye hili wenyewe wanajua zaidi cha Kusema na kufanya. Pole sana..
AD, mnaweza kupanga mambo chumbani jioni ni kitako na mamake wanajadili upya. Point taken.
 
inawezekana mumeo akili yake haipo sawa, jaribu kumtoa usingizini kwani huyo ndie mtu pekee wa kutatua hilo tatizo.
 
Wanajamvi kwa muda nimekuwa nikiumizwa na hili jambo. Mama mkwe wangu ni kama mke mwenzangu. Mume wangu anapanga budget na mama, kila kitu ni mama. juz kachukua mkopo bank nusu kampa mama afanye miradi. Nimejaribu kushare na familia mama kaja juu yeye ndio kamsomesha anastahil kuenziwa. Mume hashauriki bila kumshirikisha mamake. Hapa ana miez 6 tunakaa nae. Ni vurugu. Ushauri wandugu.

Mmeo hakuamini kama amuaminivyo mama yake....
Ridhika...chakarika....anza kujenga himaya yako....himaya yako ikikua na kuizidi ya mama, mmeo atakuwa nawe....
Simply, the mother/son bond is too strong for you at this moment....
Give it time....!
 
inawezekana mumeo akili yake haipo sawa, jaribu kumtoa usingizini kwani huyo ndie mtu pekee wa kutatua hilo tatizo.
kinyoba kama kumwambie mume wangu ukweli nishasema sana. ila toka mkwe ahamie ndio balaa zaidi.
 
AD, mnaweza kupanga mambo chumbani jioni ni kitako na mamake wanajadili upya. Point taken.
Dahh Huo ni ounevu wa hali ya juuWacha ku jadili upya mama mkwe anatakiwaAsijue mlichoongelea wewe na mmeo..Kama umeongea naye vya kutosha Na hasikii ni muda w kumsimamia kidete.Maana ukizidi kuwaonyesha upole na Watazidi kukuonea..
 
Mi ninataka nikuulize mme wako anakupenda?anajali jinsi unavyojisikia?unajua vitu anavyovipenda including unyumba mnyime akiwa anakuuliza na kulalamika unamwambia unavyojisikia vibaya ndio na mimi ninavyojisikia vibaya kutoshirikishwa na kusikilizwa,mpaka ujifunze kunisikiliza ndio ntakupa na atakapoelewa umuhmu wako,
 
Pole dada yangu,Umeolewa na Mume ambaye ni "Mtoto wa Mama"!!
Kisaikolojia Ipo mi Mama ambayo huwa haiiachii watoto wao hasa wanapokuwa na Vijisenti!!

Hapo haiwezekani kutatua tatizo hilo bila kuishia katika Uhasama,Unahitaji kufanya Uamuzi Mgumu tu dada,No easy way out!! Nina rafiki yangu Mmoja ambaye naye Mama yake Mzazi alikuwa Mtata kama huyo Mkweo!! Palikuwa Hapatoshi!!!

U have to be strong,Muonyeshe Mumeo ilo andiko halilotaja mdau hapo Juu kwamba Mwanaume atawaacha wazazi wake na ataambatana na Mkewe,siyo ataambatana Na Mama yake!! Mpe wiki mbili ajue kwamba Mambo ya Maisha yenu ni katika yako ww na yeye tu not otherwise na huyo Mama yake amrudishe,akikataa Sepa mpaka siku akiona yupo tayari kuwa "Mtu Mzima" na kuacha kuwa "mtoto wa Mama"!!
Kumbuka hapo vita haikwepeki,Usiogope,Pambana!!!

Pole kwa kupata Mume Dhaifu!!!

Hili ndio tatizo pekee. Mimi nilipoolewa, mama mkwe wangu alijaribu sana kuvuruga nyumba yangu. Lakini, mume wangu was and is still a strong man. He made it very clear to her mother that our house was not an extension of her house. Nakwambia, alikoma!

Take our advise, kaa na huyo mume wako mtoto wa mama, mweleze na hata ikibidi mwitie watu wazima wamweleze, Mwambia akafundwe!
 
Duh, hapo sina ushauri mamii..polee, Muombe Mungu atakuonyesha njia!

oh oh oh btw, kuna posibility ya nyie kuhama mkoa!?? (nliwahi kumsikia mama akimshauri mtu hivi...sijui if it can apply kwenu.)
 
Pole sana, sasa huyo mama miezi 6 anafanya nini hapoooo! na huyo mume wako inaonekana 'hajaondoka'. ndoa ni pamoja na kuondoka kwa pande zote mbili yaani mume na mke, jaribu kuongea na mumeo kama atakuelewa na umueleze jinsi unvyojisikia
 
Back
Top Bottom