Mkwasi Rostam na Vodacom

Lunyungu has a point. Sisi wananchi tunachoweza kufanya ni kuanza kumark mali za mafisadi na kuwakimbia. Honestly kama RA et al... wapo Voda tuanzishe campaign za kugomea bidhaa zao..sasa what else can we do? Mkuu Lunyungu tuko na wewe. Hata kama waajiriwa ni ndugu zetu..ni katika mapenzi mema na nchi yetu, watatusamehe. Jamaa analipwa millions every day---kodi zetu....na bado tunampelekea nyingine..why?

Hata Gandhi alisema...hiyo ni silent protest! Hakuna la soko huria wala nini..mali yoyote ya fisadi, ni kuigomea..infact wenzetu huko majuu hii trick ya kugomea vitu imefanikiwa sana! Lets try it..na isiishie kwenye Vodacom tuu..ni kote mafisadi wanakohusika...

Vodacom situmii line yao tena....
 
Masaka hadi muda nina shawishika kuelewa kwamba kichwani u mtupu na kumejaa takataka .Kama huoni makosa ya Rostam kaa pemben tuache sisi tunao yaona tupigane mana CCM wala Serikali ya CCM hawawezi kumgusa kwa kuwa alikodisha helikopta na CCM kushinda Uchaguzi kiteto .

huyu masaka katumwa na mafisadi toka mwanzo mm naona anapinga sana na hoja zinazo wagusa mafisadi toka anaingia hapa JF namwona tu.
Unajua mkuu kwanza VODA gharama zao zipo juu sana ukilinganisha na mitandao mingine.Kwa hiyo hawafai....inabidi tuelimishe na jamaa zetu wahame voda kwani ni mtandao wa mafisadi.
Mimi nimesha wahamisha watu karibia 100 toka voda wamejiunga na tigo na zantel na hawa 100 nao wanawashawishi wenzao sasa.
 
Sasa tutumie celtel? inamaana wote tumeshasahau celtel ilivyoanzishwa? hata haijapita miaka mingi jamani?
ilivyobadili sera ya nchi kuhusu kampuni ya ttcl kutokuwa na mobile company, wakauza nusu wakaachattcl inaangamia? skendo tumeshazisahau?
kweli wadanganyika tuna kazi.
wale waliolipiwa schoolfees za watoto nje ya nchi?
tigo ni yanani?
je alipataje hizo pesa.
Kiukweli nakubaliana na Waziri mkuu kuwa mafisadi wana pesa wa wanamiliki kila investor wa kampuni yoyote iliyoshinda zabuni.
kama kuna mtu anaweza kutaja kampuni kubwa safi tuanze kwa kuiunga mkono.
Ka ufupi mafisadi sio hawa tu walioshatajwa, hao ni asilimia 5 tu.
Wengi tu wapo wanaendelea kupeta,
Makatibu wakuu wawizara,
madirector wa wizara, mabalozi, wafanyabiashara wa zamani ambao wanawaweka viongozi wetu, wamiliki wa mahoteli wagiriki waliokimya kabisa,
nchi ilishauzwa zamani tu mbona, mtashikilia lowasa weeeee, kuna wengine walioweza kutoka serikalini kabla ya kufichuliwa je hao je?
Jamii forum itapotea kuhimiza watu kudhani fisadi ni rostam, lowasa, na mkapa tu.
 
huyu masaka katumwa na mafisadi toka mwanzo mm naona anapinga sana na hoja zinazo wagusa mafisadi toka anaingia hapa JF namwona tu.
Unajua mkuu kwanza VODA gharama zao zipo juu sana ukilinganisha na mitandao mingine.Kwa hiyo hawafai....inabidi tuelimishe na jamaa zetu wahame voda kwani ni mtandao wa mafisadi.
Mimi nimesha wahamisha watu karibia 100 toka voda wamejiunga na tigo na zantel na hawa 100 nao wanawashawishi wenzao sasa.

Jamani tuachane na akina Masaka mana tunapoteza muda. Please kisheria imekaa vipi hii move? nataka nitangaze hadharani. wataalamu niambieni. Sikupenda kuajiriwa Caspian Mining bcos ya mawazo kama haya. leo jion naondoa watu wawili. Na nitawaambia wazi why, nikipata wengine nitawanunulia hata line. Nipeni ushauri kisheria imekaa vipi.

Asante, tukifanikiwa hii itakuwa na impact kubwa sana
 
Madhara ya muda mrefu baada ya kususia vodacom yatakuwa yapi?

Atalazimishwa kuuza hisa zake au atafilisika.

Mie baada ya wito huu, nimitupa line yangu ya Voda. Samahani kwa mtakaonitafuta. Ntawapa nyingine ntakayonunua.
 
Nakubaliana na hoja zenu kuhusu Vodacom na Celtel(Zein to be), sasa tuhamie mtandao gani? Kwa nini tusitumie mitandao hiyo hiyo ya mafisadi kutumiana ujumbe wa kuwamaliza mafisadi wenyewe? Mimi niko celtel. Mkiniambia mtandao mzuri wa kuhamia, usio na ufisadi. Nitahamia.

Asha
 
Kama TICS walimuondoa Karamagi kwanini Voda wasiwaondoe Rostam na Noni? Hivi Benki M walikamilisha kumuondoa Jeetu Patel?

Asha
 
Bora kugomea mashirika yote ya simu hapo Bongo, kwani kwa namna moja ama nyingine yamehusika na yanaendelea kuhusika na ufisadi.. Ni bora kurudi kwenye Land line... na hawa ni wafisadi vilevile.. Heri kuachana kabisa na mawasiliano ya simu zao, ni bora kurudi nyuma kimfumo wa maisha kuliko kuendelea kupata huduma zenye harufu ya kifisadi...
 
Hii ni muhimu kabisa tusilijadili kwa utani na unazi kwa mafisadi kwani ni muhimu kubadilisha upepo wa nchi yetu, tukiachana na Vodacom wamiliki wataamua kumlazimisha RA kuuza share zake kwa manufaa ya kampuni na kumrudishia pesa yake, akainvest nje ya nchi lakini tukiziona hapa nchini tutamsusia vilevile.

Hii ndo njia pekee ambayo ni effective ya kumwadhibu RA moja kwa moja na hasira zetu.
 
Bora kugomea mashirika yote ya simu hapo Bongo, kwani kwa namna moja ama nyingine yamehusika na yanaendelea kuhusika na ufisadi.. Ni bora kurudi kwenye Land line... na hawa ni wafisadi vilevile.. Heri kuachana kabisa na mawasiliano ya simu zao, ni bora kurudi nyuma kimfumo wa maisha kuliko kuendelea kupata huduma zenye harufu ya kifisadi...

As your signature suggests, save water drink what....vituko vya zenj. Naomba wakati mwingine uwe unaviweka kwenye http://ashawazenj.blogspot.com au kwa kuwa wewe CCM hutaki majamvi ya wapinzani wako?

Asha
 
Kwa hilo la vodacom siafiki kabisa.....labda kama tumeishiwa mambo ya kufanya....na hoja zenye mvuto na kujadili mambo nyeti...kuyatafutia ufumbuzi.....

Kama huafiki toa sababu za wewe kukataa haya ni mawazo yangu na wewe unasema huafiki bia ya sababu , mie nimesema naafiki na sababu nimetoa .Tusaidie kuelewa sasa .Mambo ya kufanya yamekosekana ? Hili ni jambo zito ila inategemea wewe jambo zito kwako lina nini .
 
Watanzana tufike mahali tuchukie tuonyeshe kwa vitendo .Rostam na genge lake hawagusiki hili liko wazi ,nasi tuna imba na wao wanasema tutasema mwisho tutakaa kimya .Now it is time tuache na lile ambalo liko wazi kama hili .Kwamba Rostama na Lowasa wana connection na Vodacom basi tuanze nao .Tutaendelea naupelelezi wetu kama kuna supermarket ama hata kisimi cha mafuta kina mkono wa fisadi we avoid them .Ndiyo njia pekee .JF onyeshini njia sasa .Tumekuwa tuna sema sana .Mafanikio yapo lakini we need to hard on them .Hakuna utani.Mimk nafurahi kutangaza kwamba jana hadui leo asubuhi nimewaondoa watu 15 toka Vodacom .Niliwanunulia wachache like jana na leo nimenunua 3 za Tigo.

Jamani naomba tusimame imara kwa hili tumechoka kila kona tunanyonywa tu sasa angalau tunaweza kugomea bidhaa zao .
 
Mimi kwa mtazamo wangu naona kama mnalihukumu hilo vodacom kwa yasiyowahusu...utasusia kila kampuni ambapo watanzaniaa wengi amabao wana connection na hao mafisadi wana hisa humo...taja makampuni makubwa yenye wana hisa wa tz uone nini kitafuata...je ukikuta pesa alizowekeza huko alikopa au kuna wana hisa wadogo wadogo weengi sana humo na wamekopa si kulihukumu kampuni na wengineoo ???ni mtazamo wangu piaa...nina haki ya kujadili na kuwa upande mmoja lunyungu
 
inajuulikana kuwa rostam lowasana na mkapa sio mafisadi pekee wa tanzania. kuna na wengine wengi pia. lakini haimaanishi kwa kuwa mafisadi hawa wana wenzao ndio wasiadhibiwe!
adhabu ikimpata mmoja na wengine wanaweza hata kupunguza ufisadi wao
 
Kama huafiki toa sababu za wewe kukataa haya ni mawazo yangu na wewe unasema huafiki bia ya sababu , mie nimesema naafiki na sababu nimetoa .Tusaidie kuelewa sasa .Mambo ya kufanya yamekosekana ? Hili ni jambo zito ila inategemea wewe jambo zito kwako lina nini .

Nakubaliana kabisa hoja ya kususia bidhaa na huduma za mafisadi, lakini sasa sio ndio iwe marketing strategies ya kampuni moja.
Kwa kuanzia, hii kampuni ya TIGO ulioiona ni safi, shares zake zikoje?
Nasikia kuna giriki mmoja ambaye serikali zote zinamuheshimu wala hazimgusi, tangu awamu wa zamani. ndio baba lao mafisadi wote na mikataba ya ajabu ajabu, sina uhakika kama ni kweli, labda huko ilikotoa data za Vodacom kuna nyingie.
Please do not preach hatred here.
 
Kenya waligomea hata vyakula kwenye supermarket when they felt kwamba pesa zao zilienda kwa Kibaki na zikatumika kuwanyima haki yao .Tanzania Rostam Aziz kila kukicha ana wezi mpya lakini iko kimya na support anapewa .Sisis tuna lalamika lakini bado tunatumia huduma za simu za Vodacoma ambazo yeye ni mmoja wa share holders .Kama tuna uchungu kweli na huyu ambaye analindwa na CCM na serikali yake , tuhamie sote kwenye tigo ama zantel ama Celtel .Hii itakuwa njia nyingine ya sisi kuonyesha kwamba tumechoka kuibiwa na kuzidi kukamuliwa kila mara .Mimi nimesha hama na huhu unakaribia mwaka tangia nimejua kwamba Rostam anatumaliza bado na vodacom yumo .Mie natumia Zantel sasa na Celtel .Je wewe unangoja nini ?Tuambiane tuachana nao hawa .Wanatuona wajinga katika maamuzi yao je waendelee kutuona wajinga hata katika pesa zetu wenyewe za kutumia katika simu ?

Lunyungu,

Hii ni move ya kijasiri sana na natumaini ya kwamba kama Watanzania tutafikia kiwango hicho cha Uzalendo basi hawa Mafisadi watachomoka tu. Kwa vyovyote vile.

Lakini nina mawili matatu ambayo nataka fumbuliwa zaidi maana naamini kila ambalo tunafanya tunatakiwa kujua matunda yake:

1. Je katika Wamiliki Hisa wa hapo Vodacom wote ni Mafisadi ama ni huyu Rostam peke yake?

2. Huyu Fisadi ni Mfanyabiashara, sasa je tunatakiwa susia Bidhaa zake zote ama ni hii ya Mawasiliano tu?

3. Kutokana na sisi kutumia huduma za VODACOM kuna Watanzania wengi wamefanikiwa kupata ajira na kupunguza makali ya Maisha. Wao wamewekwa katika Kundi la Mafisadi kwa kuwa Wanamtumikia Fisadi ama? Na je Huoni kwamba tutakapoamua kufanya Hivyo tutakuwa tumewahukumu na wao kwa kiwango kikubwa?

Naomba tufikiri kwa upana zaidi!
 
Alphatel ni Fredrick Lowasa ambaye tayari kuna malalamiko jinsi alivyopata exclusive license ya kutengeneza card za simu kwa mchangamanuo ambao marehemu mtoto wa Mengi aliubuni, andika na kuuza kwa serikali kwa muda mrefu ili aweze kuanzisha hiyo biashara pasipo mafanikio.

Hapa tupo ukurasa mmoja mkuu!
 
Back
Top Bottom