Mkuu wa Wilaya ya Mbozi atangaza kujiuzulu!

Kupitia WAPO FM wanasema amejiuhuzuru kufuatia baadhi ya viongozi kupinga mikakati yake ya kuleta maendeleo.
 
Wakuu wa Wilaya kazi yao kubwa ni kulinda maslahi ya CCM. Ndio maana wote ukiwafuatilia wamepewa nafasi hizo kulipa fadhila za jitihada walizofanya wakati wa kampeni. Wengine huwa wanajua wakati wa kampeni kuwa watapewa Ukuu wa Wilaya. True wote ni makada wa kutupwa wa CCM.
 
Hilo jembe sana, halina shda na maulaj ya pesa ya walala hoi, unlike to ngeleja, maige, chami, mkulo....., hawa mpaka povu liwatoke ndo.....
 
Mkuu wa Wilaya Mbozi ajiuzulu wadhifa wake04/05/2012
0 Comments

Mkuu wa Wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya Gabriel Kimolo amejiuzulu wadhifa wake wa Ukuu wa Wilaya ya Mbozi kwa kile alichosema kukosa ushirikiano na Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika ikiwa ni pamoja na kuchelewesha kupewa uteuzi mpya ambapo uteuzi wake wa awali ulikoma mwaka 2010 (kianzia mwaka 2006).

Bw. Kimolo alisema kuwa ameamua kwa hiari yake kutokana na kugubikwa na ubabaishaji wa utendaji katika ngazi mbalimbali hali ambayo imemsababisha kushindwa kufanya kazi kwa ufanisi.

''Hii hali imenifanya nishindwe kufanya kazi kwa ufanisi..nishindwe kuweka mikakati yangu ya kazi..nimekuwa mtu wa kushughulikia mambo ya dharura... na maagizo kutoka juu,'' nimeamua kuachia ngazi naenda kufanya shughuli zangu binafsi.''alisema Bw. Kimolo.

Vile vile katika blogu ya mwanahabari Gordon Kalulunga imeripotiwa kuwa sababu nyingine aliyoitaja ya kujiuzulu nafasi hiyo ni Serikali kushindwa kuwawajibisha baadhi ya watumishi ambao amedai kuwa si waaminifu.

Mkuu huyo wa Wilaya ametoa msimamo huo leo mbele ya mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro katika ukumbi wa BEACO uliopo Jijini Mbeya.

SOURCE: WAVUTI
 
Mbali na JK kutangaza marekebisho ya mawaziri wake leo,
Mkuu wa Wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya Gabriel Kimolo amejiuzulu wadhifa wake wa Ukuu wa Wilaya ya Mbozi kwa kile alichosema kukosa ushirikiano na Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika ikiwa ni pamoja na kuchelewesha kupewa uteuzi mpya ambapo uteuzi wake wa awali ulikoma mwaka 2010 (kianzia mwaka 2006).

Bw. Kimolo alisema kuwa ameamua kwa hiari yake kutokana na kugubikwa na ubabaishaji wa utendaji katika ngazi mbalimbali hali ambayo imemsababisha kushindwa kufanya kazi kwa ufanisi.

''Hii hali imenifanya nishindwe kufanya kazi kwa ufanisi..nishindwe kuweka mikakati yangu ya kazi..nimekuwa mtu wa kushughulikia mambo ya dharura... na maagizo kutoka juu,'' nimeamua kuachia ngazi naenda kufanya shughuli zangu binafsi.''alisema Bw. Kimolo.

Source: Wavuti.com
 
[h=2]FRIDAY, MAY 4, 2012[/h][h=3]BREAKING NUUUUUZ LIVE: MKUU WA WILIYA MBOZI MH.GABRIEL KIMOLO ATANGAZA KUJIUZULU MUDA HUU[/h]

MBEYA YETU BLOG IMEPOKEA TAARIFA MUDA MCHACHE ULIO PITA KUWA MKUU WA WILAYA YA MBOZI MUHESHIMIWA GABRIEL KIMOLO AMETANGAZA KUJIUZULU, MPAKA TUNALETA TUKIO LIVE HAPA BADO HAJASEMA SABABU ZA YEYE KUFANYA HIVYO...

Huyu atakuwa na bifu na waziri fulani!!Ameamua kuwahi mapema kabla hakijanukishwa!!!
 
Back
Top Bottom