Mkuu wa Wilaya ya Liwale afia Guest House!

hahaaaa ....pumzika mkuu wangu wa wilaya ya liwale..unachezee viuno vya wana Lindi....pigwa mapangaboi ya kufa mtu mpaka mzee wetu anapata cardiac arrest kama ya Muamba...
 
Habari zilizothibitshwa na Radio one break news Mkuu wa wilaya ya Newala Paul amefariki dunia baada ya kukutwa amekufa kwenye nyumba ya wageni ya mission iliopo lindi alipokwenda kwenye semina.

Put clear...Liwale au Newala???
 
CONFIRMED!.
Mkuu wa wilaya ya Liwale, Paul Chiwile amefariki usiku wa kuamkia leo katika nyumba ya wageni aliyofikia mjini Lindi.
Mkuu huyo wa wilaya alikuwa Lindi kuhudhuria mkutano uliokuw aunatarajiw akuanza leo wa utekelezaji wa mpango wa kitaifa wa magonjwa yasiyokuwa na kipaumbele.
Kwa mujibu wa Radio One mwili wa marehemu upo katika hospitali ya mkoa ya Sokoine ukisubiri kufanyiwa uchunguzi.
Imefahamika kwamba atazikwa kwao Kibaha.
 
Mode, naomba badili headline, ondoa jina "guest house", ireplace na nyumba ya kulala wageni, au hoteli aliyofikia!
Neno "guest house" linabeba bad cannotation kwa watu wa mambo ya guest hivyo kufikiri kila anayelala guest, analala kwa yale!.
 
.... yale yale ya Adam Malima, Ukiwaona Ditopile Mzuzuri kule Morogoro. Ugonjwa wa wenzetu hawa kujifunika blanketi si yao sasa imeshakua ni nongwa kubwa. Mambo ya kulala na WATU WASIOFAHAMIKA sasa ni kero.

Poleni sana familia ya marehemu, ni Mtanzania mwenzetu kapoteza uhai hapo.

Wanabodi,

Mkuu wa wilaya ya Liwale, Paul Chiwile amefariki usiku wa kuamkia leo katika nyumba ya kulala wageni ya Vission aliyofikia mjini Lindi.
Mkuu huyo wa wilaya alikuwa Lindi kuhudhuria mkutano uliokuwa unatarajiwa kuanza leo wa utekelezaji wa mpango wa kitaifa wa magonjwa yasiyokuwa na kipaumbele.

Kwa mujibu wa Radio One mwili wa marehemu upo katika hospitali ya mkoa ya Sokoine ukisubiri kufanyiwa uchunguzi.
Imefahamika kwamba atazikwa kwao Kibaha.

RIP DC Paul Chiwile!.
 
Au ugomvi wa chini chini utakua ni kwenye kupata Ukuu wa Mkoa huo maana nakumbuka yule aliyeletwa toka Mwanza kulipwaya sana na kukawepo na hadithi za kwenda mbele hatua tano rudi nyuma hatua 20 vile.

Mkuu Kamanda Manumba, hapa sasa ndio penyewe na wala si kumpima Daktari Mwakyembe kutokana na picha za kwenye magazeti kisha kutoa jibu kwamba hakupewa sumu.

Kuna mshkaj wangu yuko eneo la tukio anasema polisi wanajiandaa kuvunja mlango wa hiyo lodge then akafanyiwe post mortem. Tutapata majibu leo leo (kama yatakuwa ya kweli) maana nchi hii nayo.
 
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi, sote ni binadamu na njia yetu ni moja. mh imeelezwa alikuwa anahudhuria semina, hivyo ilibidi afikie nyumba ya wageni
 
Kuna haja hawa viongozi wetu kubadili muelekeo na tabia zao. Maana haya machakula ya siku hizi hatari sana, yanaleta mafuta kwenye damu, ambayo in turn inaweza leta vifo visivyo tegemewa! Waaanza kukimbia kimbia kuchoma mafuta kuacha mwili uko safi!

Itakuwa mzee wetu alikutana na kwata la kufa mtu, ukichanganya na makonyagi ya kukomeshea, ndo inkuwa tabu kabsa! RIP DC na poleni wana-CCM.
 
alikuwa anasukuma ngozi au ni nini mkuu??manake magamba wao wanawaza uasherati basi!

chezea orgasm wewe! Mzee pressure ikapanda,pressure ikashuka akapatwa na cerebrovascular accident. RIP kama Mungu atakusamehe,maana ni mshiri wa wahujumu wa nchi hii.
 
Mkuu wa Wilaya angekuwa wa kuchaguliwa sasa tungekuwa tunajadili kivingine
 

Mbunge wa Jimbo la Liwale Faith Mitambo (wa pili kushoto), akikabidhi seti ya
jezi kwa Nahodha wa timu ya soka ya Serengeti FC, Johnson Raymond (kulia, wakati
wa hafra ya kukabidhi msaada wa vifaa vya michezo iliyofanyika mjini Liwale
jana. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya hiyo Paul Chiwile.
(Source:Global Publishers)
Oooh masikini Mwalimu Paul Chiwile.
Alikuwa mwalimu wangu pale shule ya sekondari Kibaha miaka ya 1971-1976.
He was a gentleman.
Nimeenda kumuoana mwaka jana alipofiwa na mke wake aliyepata ajali kule Moshi.
Mke wake vile vile alikuwa mwalimu wangu.
Poleni sana watoto wa Mr & Mrs Paul Chiwile kwa kupoteza wazazi wote wawili in a span of one year, what tragedy.
Bwana Mungu aliwatoa na sasa amewatwaa, Jina lake lihimidiwe.
Amen
 
hahaaaa ....pumzika mkuu wangu wa wilaya ya liwale..unachezee viuno vya wana Lindi....pigwa mapangaboi ya kufa mtu mpaka mzee wetu anapata cardiac arrest kama ya Muamba...

jamani huku JF! R. I. P. mkuu wa wilaya!
 
Back
Top Bottom