Mkuu wa wilaya Dodoma atekwa na wanafunzi

Pinda ameomba radhi, na kusingizia kwamba anaumwa malaria kwa hiyo waahirishe mkutano, na kuwapa ahadi eti anakuja kesho saa tano mpaka tano.

kamtuma waziri wa elimu aombe radhi kwa kilichotokea na kwamba keshoa aendelee. Wahadhiri wanalalamika kwanini awanyanyase kuwapangia muda kesho?
Na anauhakika gani kesho atakuwa okay? Kama sio usanii?
 
hahahahaha!

12_10_6scme1.jpg
 
Sasa waziri Kawabwa kwa niaba ya Pinda amekuja kuomba radhi kwa usanii waliowafanyia wanataaluma.

hivi ndg zangu ipo hii? Waziri kusingizia anaumwa na kumtuma mwingine amuombee radhi? Ipo hiyo?

na wanataaluma wanahoji kapanga kesho kuwa ndio ataongea, hw sure he is kwamba atakuwa okay kama sio usanii ili waandae majibu na kuyachakachua hiyo kesho?

Tanzania haitafika kwa usanii kama huu ukiendelea
 
Nchi hii itaendelea kuwa chini kama viongozi wetu wataendelea kucheza na kudumaza maendeleao ya nchi kila siku.
 
Pinda ameomba radhi, na kusingizia kwamba anaumwa malaria kwa hiyo waahirishe mkutano, na kuwapa ahadi eti anakuja kesho saa tano mpaka tano.

kamtuma waziri wa elimu aombe radhi kwa kilichotokea na kwamba keshoa aendelee. Wahadhiri wanalalamika kwanini awanyanyase kuwapangia muda kesho?
Na anauhakika gani kesho atakuwa okay? Kama sio usanii?
Amewaomba radhi mnataka nini? Halafu nyie wahadhiri ndio mnataka mumpangie muda Waziri Mkuu? Wakulima wa Mahindi nao wakifanya hivyo? Kesho wa Korosho? Na kesho kutwa wauza mitumba!!! Inawezekana mnayo ya msingi ya kulalamika lakini hoja kama hii ni ya kitoto, amewataka radhi tayari ni heshima. Uungwana unahitajika.
 
Mbona makamu mkuu wa chuo fedha na utawala Mlacha yipo afisini kwa Waziri Mkuu hapa Dodoma
nahisi kama vile kaitwa kujieleza halafu wayafunike hukuhuku, huko chuoni wakija ni geresha tu.

mkuu si taarifa za kiinteligensia hizi? wakimfuata huko ofisini na kumfanyia fujo je?
 
Nathani sasa Chuo cha Dodoma kimejitambulisha kwamba kinapambana na haki. Ningeomba tuwaunge mkono, yaliyopita si ndwele kwa sababu thread za huu mgomo zinasuasua sana na wakati mwingine zinakumbana na kejeli tu. Lakini wakifanikiwa madai yao, inaweza kufaidisha vyuo vingine pia
 
Kweli watanzania wamechoka haswa; wanachotaka sasa ni haki tu itendeke kila eneo! Hope viongozi wetu watafumbuka macho na kuona sasa si zile nyakati za kula na kipofu... sasa kipofu ameanza kuona..:)
 
Amewaomba radhi mnataka nini? Halafu nyie wahadhiri ndio mnataka mumpangie muda Waziri Mkuu? Wakulima wa Mahindi nao wakifanya hivyo? Kesho wa Korosho? Na kesho kutwa wauza mitumba!!! Inawezekana mnayo ya msingi ya kulalamika lakini hoja kama hii ni ya kitoto, amewataka radhi tayari ni heshima. Uungwana unahitajika.

Mkuu, MH PInda ndo aliwapa muda, kisha akachelewa masaa 6 na akamtuma mtu kuomba radhi na kuwapangia tena muda mwingine. Hii ni dharau. Kama alijua hawezi kuhudhuria mkutano angetoa taarifa mapema. Hii haina excuse hata uwe President Obama ni lazima uheshimu muda wa watu. Ni tabia mbaya na dharau kubwa! Hata angewafanyia hivyo wakulima wa korosho bado ukweli unabaki kuwa ni dharau.
 
I hate u Pinda kwani wewe ni mnafiki usiye na haya kuwaweka waadhiri wakikungojea pamoja na wanafunzi kisha kuwakimbia. Pinda siyo kiongozi kama nilivyomjua naye kumbe yupo kundi lile lile ya uozo wa viongozi.
 
Kinachouma ni kwa nini aombe radhi baada ya muda mrefu kupita??? Ndiyo usanii unaoongelewa hapa. Hata kama ni waziri mkuu lazima nae atumie hekima na awe muungwana.
 
Kwa jinsi sakata lilivyo zito inawezekana pinda amekosa majibu ya kuwapatia wahadhiri baada ya kuelezwa issue yenyewe jinsi ilivyo. Sina hakika kama kweli PM kawatosa wahadhiri inawezekana kachelewa tu kwenda huko ila kitu nachojiuliza ni kwamba huyu MLACHA ni nani hasa mpaka aendelee kung'ang'ania madarakani maana ni wazi wanafunzi na wahadhiri hawamtaki na anaonekana kua chanzo cha matatizo yote pale udom. Inasikitisha kuona kwamba rais bado anashindwa kuchukua maamuzi mazito yenye maslahi kwa taifa. Prof MLACHA, na viongozi wengine wanapaswa kuwajibishwa il kurejesha amani chuoni hapo wakati madai mengine yanaendelea kushughulikiwa. Hata kama ataendelea kubakia madarakani hata ongoza na amani na nina wasiwasi kwa haya yaliyomkuta leo huenda wanafunzi wakamfanyia kitu mbaya. Please MLACHA you better resign before you are forced to resign.
 
Amewaomba radhi mnataka nini? Halafu nyie wahadhiri ndio mnataka mumpangie muda Waziri Mkuu? Wakulima wa Mahindi nao wakifanya hivyo? Kesho wa Korosho? Na kesho kutwa wauza mitumba!!! Inawezekana mnayo ya msingi ya kulalamika lakini hoja kama hii ni ya kitoto, amewataka radhi tayari ni heshima. Uungwana unahitajika.

mkuu sijasema kwamba kakosea kuwaomba radhi wahadhiri, tatizo ni mbinu aliyotumia kwamba anaumwa malaria, naamini ni usanii kwani kesho ana uhakika gani atakuwa na afya? Swala ni kwamba alizidiwa na mambo na alitakiwa kuwa mkweli, nadhani angeeleweka vema zaidi kuliko alivyofanya.
 
Waziri mkuu Pinda amefanikiwa kuvuka viziwizi vya wanafunzi baada ya kubadili gari alilokuwa anatumia mwanzo na kupita kabla ya wanafunzi kustuka. Ila swali kwa wana JF je pinda amekuja udom kufanya nini ikiwa kilichomleta ata moja ajatatua! Huu ni usanii na haukubaliki.
 
Mkuu, MH PInda ndo aliwapa muda, kisha akachelewa masaa 6 na akamtuma mtu kuomba radhi na kuwapangia tena muda mwingine. Hii ni dharau. Kama alijua hawezi kuhudhuria mkutano angetoa taarifa mapema. Hii haina excuse hata uwe President Obama ni lazima uheshimu muda wa watu. Ni tabia mbaya na dharau kubwa! Hata angewafanyia hivyo wakulima wa korosho bado ukweli unabaki kuwa ni dharau.
Hata hao viongozi uliwataja wa Western pia nao hukumbwa na dharura na kuahirisha kama sikusogeza muda mbele. Wengine hucancel kabisa hata hizo safari. Well kasema anaumwa, kuna tatizo gani? Mbona watu tunajitishwa mno uwanamkubwa. Bahati mbaya hawa wahadhiri wengi miongoni mwao huwazungusha wanafunzi kwa appointment zisizo eleweka. Amesema atawasikiliza!
 
Back
Top Bottom