Mkuu wa wilaya Dodoma atekwa na wanafunzi

King Suleiman

JF-Expert Member
Dec 27, 2010
496
327
Ndg wanajamii, nina habari za uhakika mkuu wa wilaya wa Dodoma ametekwa na msafara wake na wanafunzi wa chuo cha elimu, wakimtaka waziri mkuu Pinda aje na kuondoka na makamu mkuu wa chuo fedha na utawala Mlacha.

Waziri mkuu alikitembelea UDOM tangu mchana lakini mpaka sasa ameshindwa kukutana na makundi kadhaa ya wana UDOM hususa Wanataaluma ambao wapo kwenye mgomo baridi tangu J3.

Wanafunzi hao wametoa upepo msafara wa mkuu wa wilalaya na kuziba kioo cha mbele kwa mabango huku wakipiga kelele kumuomba Pinda aje.

Nitazidi kuwapasha...
 
Mpaka sasa wahadhiri na wafanyakazi wa chuo kikuu cha Dodoma wapo nje ya ukumbi mkuu wa chuo hicho uitwao Chimwaga wakimsubiri w/mkuu ambae kuna tetesi ameshaenda mjini.

bado hakujawa na taarifa rasmi za nini kitafuata ila minon'gono ya wanataaluma ni kuendeleza mgomo j3 kama w/mkuu hatafika na kutatua mgogoro wao.
 
Asante kwa taarifa. Kwa mwendo huu itabidi JK aseme mwenyewe na wala sio kutuma watu.
 
Inaonekana kuna usanii unataka kufanyika ili kuwpooza wahadhiri warudi madarasani huku madai yao yakiwa bado yanachakachuliwa.

kila kundi la wanajamii wa Udom wanamtaka prof.Mlacha ambae kuna tetesi ni ndg na Jk, apigwe chini na kupatikana mtu makini kusimamia fedha na wafanyakazi wa Udom
 
Mbona makamu mkuu wa chuo fedha na utawala Mlacha yipo afisini kwa Waziri Mkuu hapa Dodoma
nahisi kama vile kaitwa kujieleza halafu wayafunike hukuhuku, huko chuoni wakija ni geresha tu.
 
Watoto wa wakulima wenye shida toka wakiwa nyumbani kwani wanaonesha msimamo wao bila kuogopa mda pamefanyika uchaguzi mpya wa raisi mwingine pia wametoboa matairi ya magari ktk msafara wa w/mkuu Pinda ila kabla w/mkuu ajaenda ng'ong'ona alikuwa social science alizomewa uku gari la Pr Mlacha likizuiwa kutoka uku wanafunzi wakipanda juu ya gari wakilipiga.
Hali ni tete hapa udom
 
Kazi wanayo mwaka huu. wamezoea kula bata kiulani.

Kaza uzi mpaka wakome ufisadi wa kijinga.

Ubinafsi na roho mbaya za viongozi wetu.
 
Naona sasa ndio waziri mkuu anakaribia kuwaona wahadhiri wa udom. Ni ahadi ya saa saba na nusu sasa kumi na mbili, kweli viongozi wetu wa kiafrika na ahadi za muda zinasumbua
 
Piza sidhani kama atakuwa na msaada zaidi ya majibu ya kisiasa, kwanza achelewi kuanza kulia mkimbana sana
 
Jamani wana jamii, maajabu kabisa. Waziri mkuu kapitliza kweli town na kuwaacha wafanyakazi wa Udom hususani wahadhiri wakiwa hawana la kufanya.

kinachonishangaza hata Pinda nae kadanganya kwamba ataongea na wafanyakazi kawaacha solemba.

ninafuatilia habari za mkuu wa mkoa na wilaya waliotekwa na wanafunzi huko ngo'ng'ona chuo cha elimu kisha nitawajuza
 
kuna dalili zinaonyesha kuna mawaziri watakimbia serikali ya kikwete hali ni mbaya kila ukigusa moto.chakula hakiliki,tukaze buti jamani
 
Taking away of a person against the person's will is kidnapping, and kidnapping is criminal (unlawful act).
 
Ndg zangu baada ya mtoto wa mkulima Pinda kukimbilia mjini sasa wahadhiri wapo ndani ya ukumbi, wanataka kuhalalisha mgomo wao uendelee.

viongozi wao wameenda kupata uhakika kama kweli haji na kawaweka toka saa saba wakimsubiri bila kutokea.

ni aibu kwa kiongozi wa taifa kuwa mzushi katika muda na kuamua kutowapa taarifa mapema bali kuwaacha solemba.

jamani nipeni jibu, M.Pinda bado ni mtoto wa mkulima? Au kachakachuliwa?
 
View attachment 20533 871006_b.jpg here we go hadi kieleweke, UWIZI WA KURA unawaandama,
 
serikali ya sasa imezoea yale mambo ya zamano kuwa hakuna mgomo,na wanatii watambue sio vizazi vya sasa mtoto anazaliwa leo anakwambia baba hiyo ni nini?wabadilike kwani wananchi watawaumbua,anagalieni ya tunisia rais amekimbia nchi yake nguvu ya umma hiyo
 
Back
Top Bottom