Mkuu wa Wilaya Ayacharukia Madhehebu

X-PASTER

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
11,610
1,809
Mkuu wa Wilaya Ayacharukia Madhehebu

Imeandikwa na Joachim Nyambo, Ileje.


MKUU wa Wilaya ya Ileje mkoani Mbeya, Ester Wakali ametishia kuyafungia madhehebu yanayoshawishi waumini wake wasiwapeleke watoto wao vituo vya afya kupatiwa chanjo ya magonjwa mbalimbali ikiwemo polio.

Mkuu huyo wa Wilaya ametoa onyo hilo siku moja kabla ya siku iliyopangwa kutoa chanjo kwa mikoa mitano iliyoko mipakani ya Mbeya, Rukwa, Kigoma, Kagera na Mara.

Alitoa kauli hiyo juzi wakati wa kikao cha kamati za huduma za afya ya wilaya cha kupanga mikakati ya kufanikisha chanjo hiyo.

Uzoefu unaonesha kuwa baadhi ya madhehebu wilayani hapa yamekuwa kikwazo cha utoaji chanjo mbalimbali kwa watoto.

Matukio ya viongozi wa dini kutowaruhusu waumini wao kutojitokeza katika kampeni za masuala ya afya yamekuwa yakijitokeza mkoani hapa.

Licha ya viongozi wa dini, pia baadhi ya wanasiasa wanadaiwa kuwa miongoni mwao kwani mwaka jana wanasiasa hao waliitisha mikutano ya hadhara kuwashawishi wananchi kutopokea vyandarua vilivyotolewa na Serikali bure.

Mratibu wa Chanjo ya Polio Wilaya ya Ileje, Yard Simkoko alisema wilaya hiyo ni miongoni mwa zilizoko mipakani ambazo watoto wamepatiwa chanjo ya polio wakati wakiwa wadogo lakini ugonjwa huo umeelezwa kulipuka katika nchi jirani na kwa hiyo kunahitajika chanjo nyingine.
 
Back
Top Bottom