Mkuu wa Usalama wa Utawala wa Gaddafi: Najuta kuwa sehemu ya Utawala wa Gaddafi

DSN

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
2,837
1,674
Mkuu wa Usalama Wa ndani wa Serikali Ya Libya [Libya's former internal security chief, Mansour Daw,] akiongea na CNN amesema anajuta ni kwanini amekuwa ni sehemu ya Utawala wa Gaddafi.Na anasema walimshauri Gaddafi toka mwezi wa Nne kuondoka Libya,lakini kwa Gaddafi na wanae walikataa na ilikuwa shida dakika za mwisho kiasi kuwa woga ulimzidi hata chakula ilikuwa shida kupata.

Point niliyoipenda ni pale aliposema GADDAFI kwa kukaa kwake Madarakani muda mlefu akuamini na wala hakutarajia kwamba angetoka Madarakani kwa muda wa Sekunde.Hivyo anasema anatamani kama asingekuwa hai kuyaona haya yaliyowatokea.

640x392_52329_172864.jpg
 
Huyu anatafuta kuonewa huruma tu hana lolote, yeye alifanya nini baada ya kumshauri na gadaffi akakataa? ni hatua zipi alichukua? anajua he was suppose to be the next person sasa anajisalimisha kijanja kwa wazungu.
 
former chief of internal security!!-mbona anaonekana mchovu hivi?
Hapa ni baada ya kukamatwa.Ukifuatilia alikua anaambatana na Gaddafi na watoto wa Gaddafi na alivyojieleza ni kuwa hapo walikuwa na hali mbaya hata chakula ilikuwa inakuwa shida kupata na hata kulala ilikuwa ni kwenye magofu.Kwa hiyo hiyo hali uanayomuoana nayo kwenye hiyo picha ni mara baada ya kukamatwa.Ili kwa picha ya leo CNN kaludi kwenye form tena anasema anawashukuru NTC kkwa kuwa wanamtendea wema.
 
former chief of internal security!!-mbona anaonekana mchovu hivi?

kweli ni mchovu kabisa ndo maana anaongea cowardly watu kama hawa mimi huwa na refer kwenye usemi wa TUPAC "A coward dies a thousand deaths... a soldier dies but once."
 
Kila binadamu hutafuta sehemu ya kutokea pale anapoona amani au maisha yake yapo hatarini,sioni tatizo kwa yeye kusema kuwa anajuta maana hakuna aliyemlazimisha kuwa sehemu ya utawala wa Ghaddafi bali kwa kuwa ndio iliyokuwa serikali halali kwa wakati huo na kazi yake ilikuwa si kwa Ghaddafi bali kuwatumikia wananchi.
Huwa napata shida sana na watu kujifanya kumchukia mtu pale anapoondoka madarakani,hivi tujiulize kwanini hakusema maneno haya wakati yupo katika utawala wa Ghaddafi?
 
nadhani kwa hawa jamaa wanaotutisha na Al-Shaabab pale wananchi wanapotaka kuandamana kwa kudai haki halali (utadhani wao hawaishi hapa) huenda siku sio nyingi wasiamini yatakayotokea hapa pia. ...japo ukiwauliza hata leo utaona wanatamba kuwa "hayo hayawezekani hapa Tanzania"!
Mkuu wa Usalama Wa ndani wa Serikali Ya Libya [Libya's former internal security chief, Mansour Daw,] akiongea na CNN amesema anajuta ni kwanini amekuwa ni sehemu ya Utawala wa Gaddafi.Na anasema walimshauri Gaddafi toka mwezi wa Nne kuondoka Libya,lakini kwa Gaddafi na wanae walikataa na ilikuwa shida dakika za mwisho kiasi kuwa woga ulimzidi hata chakula ilikuwa shida kupata.

Point niliyoipenda ni pale aliposema GADDAFI kwa kukaa kwake Madarakani muda mlefu akuamini na wala hakutarajia kwamba angetoka Madarakani kwa muda wa Sekunde.Hivyo anasema anatamani kama asingekuwa hai kuyaona haya yaliyowatokea.
Kwani Shimbo wenu yukoje? asipopigilia yale makanyaboya yake yenye X mabegani ana tofauti gani na wanywaGongo na Chimpumu wa tandale?
 
huwa najiuliza gadaffi angekaa kwenye ule mtaro kwa muda gani? Maisha bwana ya ajabu kweli. unaweza kuua watu kibao lakini ikija zamu yako, walahi woga wake ni kama hujawahi kuona kifo vile.
 
Anajuta baada ya kupoteza mlo!!!! Hata so called "Mtoto wa Mkulima" naye ataweza kuwa na kauli hiyo baada ya kumaliza muda wake kuwa alijuta kuwa kwenye serikali ya kifisadi.....watch..
 
kweli ni mchovu kabisa ndo maana anaongea cowardly watu kama hawa mimi huwa na refer kwenye usemi wa TUPAC “A coward dies a thousand deaths... a soldier dies but once.”

na akongeza ya kwamba "i would rather die like a man than live like a coward.,
 
Back
Top Bottom