Mkuu wa Upelelezi Dar akana kumkandamiza Jerry Muro

Wa Ndima

JF-Expert Member
Aug 13, 2010
1,526
323
MKUU wa Upelelezi wa makosa ya Jinai Kanda Maalumu ya Dar es Salaam,
Kamishna Msaidizi wa Polisi, Charles Mkumbo amekanusha kumshurutisha
mshitakiwa Deogratias Mgasa kutoa maelezo yanayomkandamiza mtangazaji
wa Kituo cha Televisheni ya Taifa cha TBC 1, Jerry Muro. Akitoa ushahidi katika
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Mkumbo alidai kuwa si kweli madai
yaliyotolewa na Mgasa kuwa yeye pamoja na askari wengine wengi waliojaa
chumba walimshurutishwa kusaini maelezo yanayomkandamiza Muro kwa madai
kuwa Muro amelidhalilisha Jeshi la Polisi.

"Siku ya Februari 3, mwaka huu mimi sikufika kabisa makao makuu ya polisi
nilikuwepo ofisini kwangu Kituo cha Kati cha Polisi siku nzima, kwa hiyo si kweli madai hayo,"
alidai Mkumbo. Katika kesi hiyo ndogo ndani ya kesi ya msingi ya kuomba na kupokea
rushwa ya Sh milioni 10 inayomkabili Muro, Mgasa na Edmund Kapama, upande wa
mashitaka jana ulileta mahakamani mashahidi watano akiwamo Mkumbo kuthibitisha
madai ya Mgasa kuwa alilazimishwa kusaini maelezo ya onyo ambayo yalikuwa yanamtaja
Muro kuhusika na kwamba polisi walifanya hivyo kwa sababu alikuwa amelidhalilisha
jeshi la polisi. Mkumbo alidai Januari 31, mwaka huu alitoa maelekezo ya kukamatwa
Mgasa na Kapama na kesho yake waliletwa ofisini kwake saa 7.45 ambapo alimuita
Inspekta William Solla kuandaa gwaride la utambulisho ambalo Mhasibu wa
Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, Michael Wage, alipita kuwatambua.
Wakili wa washitakiwa Mgasa na Kapama, Majura Magafu, juzi alipinga kupokelewa
maelezo ya onyo ya mshitakiwa Mgasa akidai kuwa mshitakiwa huyo wakati akitoa
maelezo hayo ya nyongeza ya onyo yaliyochukuliwa Februari 3 mwaka huu haikuwa
kwa ridhaa yake na alilazimishwa kuandika maelezo yanayomkandamiza Muro.

Source: HabariLEO August 21
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom