Mkuu wa shule ajinyonga akidaiwa kubaka mpwawe

Kiranja Mkuu

JF-Expert Member
Feb 18, 2010
4,066
4,085
MKUU wa Shule ya Sekondari ya Matimila Isdory Mrema (45) iliyopo mkoani Ruvuma amejiua kwa kujinyonga baada ya kukamatwa na kisha kuachiwa kwa tuhuma za kumbaka mtoto wa dada yake .

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Michael Kamuhanda amesema tukio hilo lilitokea jana saa 1:00 asubuhi ambapo mwalimu huyo alikutwa akiwa amejinyonga katika nyumba yake ya Mahenge Mabatini mjini Songea kwa kile kinachodaiwa kuwa ni kuona aibu kutokana na kitendo alichofanya.

Alisema, Mwalimu huyo alikamatwa juzi baada ya kudaiwa kuwa alimbaka mwanafunzi wa Chuo Kikuu Mlimani (22) jina limehifadhiwa ambaye ni mtoto wa dada yake ambaye alifika mjini Songea kwa ajili ya kufanya mazoezi na kufikia nyumbani kwa mjomba wake.

Alisema, mwalimu huyo ambaye mara baada ya kutiwa mbaroni aliachiwa huru 22 Agosti mwaka huu baada ya kupewa dhamana, lakini aliamua kujiua baada ya kuona aibu kutokana na mpwaye kulipoti polisi na kueleza tukio zima lilivyotokea hali ambayo ilimsababisha aamue kujiua.

Mwili wa marehemu huyo umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti hospitali ya mkoa wa Ruvuma na hakuna mtu yoyote ambaye anashikiliwa kuhusiana na kifo hicho.

Wakati huo huo, baadhi ya wananchi wa manispaa ya Songea wameelezea kusikitishwa kwao na vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto ambavyo vinaendelea mkoani Ruvuma.

Source:- MWANANCHI
 
Huyo mpwaye si mtu mzuri,angemweleza mama yake wayamalize nyumbani hata kwa akina Mbowe,Slaa na Ndesamburo.Sasa kumripoti polisi ili afungwe maisha anafikiri kitu chema!
 
Huyo mpwaye si mtu mzuri,angemweleza mama yake wayamalize nyumbani hata kwa akina Mbowe,Slaa na Ndesamburo.Sasa kumripoti polisi ili afungwe maisha anafikiri kitu chema!

Una watoto mkuu? Basi fikiria shemeji yako (kaka yake mkeo) amembaka mwanao!!!! narudia tena, AMEMBAKA! Yeye angetaka kuyamaliza kifamilia si angepeleka posa akaozwa na kumlala mpwae kihalali?!!!!
 
Una watoto mkuu? Basi fikiria shemeji yako (kaka yake mkeo) amembaka mwanao!!!! narudia tena, AMEMBAKA! Yeye angetaka kuyamaliza kifamilia si angepeleka posa akaozwa na kumlala mpwae kihalali?!!!!

Hatari hatari hatari doooh hatari
 
una watoto mkuu? Basi fikiria shemeji yako (kaka yake mkeo) amembaka mwanao!!!! Narudia tena, amembaka! Yeye angetaka kuyamaliza kifamilia si angepeleka posa akaozwa na kumlala mpwae kihalali?!!!!

ndio amfunge mwenzie wakati starehe wamepata wote?angalia sasa mwenzie kashatangulia kuzimu!
 
Starehe gani wakati upande mmoja haukuridhia kama wangekuwa wamekubaliana tusingesikia habari za kujinyonga wangekuwa wanaendelea kimyakimya mpaka ammimbe ndo msala ungesanuka
 
Wanawake wooote hawa! Yy anang'ang'ana na Mpwa wake loh! Ametia doa kwenye familia yake! Kina Mrema poleni kwa double tragedy... Binti huyo pia anahitaji counseling ya nguvu... Kwani naye anaweza akajiua...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom