Mkuu wa polisi afukuzwa kazi Nigeria

sulphadoxine

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
2,257
644
Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan, amemfuta kazi kamishna wa polisi kutokana na ongezeko la visa vya mashambulizi yanayotekelezwa na kundi la wanamgambo wa Kiislamu la Boko Haram.
Taarifa kutoka ikulu ya Nigeria imesema kuwa Hafiz Ringim amelazimishwa kwenda likizo ya lazima huku akisubiri kustaafu rasmi.
Hatua ya kumstaafisha mapema mkuu wa Polisi , wiki chache tu kabla ya kustaafu rasmi inaonyesha jinisi gani swala la Boko Haram limeitatiza serikali ya Goodluck Jonathan.
Baada ya mashambulizi ya hivi karibuni ya kundi hilo la Boko Haram serikali imekuwa ikishinikizwa kuchukua hatua madhubuti kukabiliana na hali hiyo.
Hivyo hatua ya kumtimua kazi mkuu wa polisi inaonekana kuwa ni njia mojawapo ya kuwafanya wa Nigeria wawe na imani na kikosi cha polisi cha nchi hiyo.
Ishara kuwa mkuu huyo wa polisi alikuwa amelemewa na kazi ni pale mshukiwa mkuu wa Boko Haram ambaye ana tuhumiwa kupanga mashambulizi katika kanisa moja na kusababisha vifo vya watu karibu 30 siku ya krismasi alipotoroka jela.
Mambo yalionekana kumlemea Hafiz Ringim, wakati alipotangaza kuwa atakabiliana vilivyo na kundi la Boko Harama hadi alimalize ,lakini siku chache baadaye kituo cha polisi kikashambuliwa na kundi hilo la Boko Haram.
Taarifa toka ikulu ya Nigeria inasema kuwa hivi karibuni kikosi kizima cha polisi kinatarajiwa kufanyiwa marekebisho ili kuimarisha utendaji kazi wake.
 
Hapo kuna udini umejificha kwa mbaaaali! GoodLuck aliwahi kusema kuna watu wanaunga mkono kikundi cha Boko Haram ndani ya serkali yake! Kwa kuwa jamaa hi Hafiz from North....you can onnect the dots!
 
kumbe hata huko Nigeria mambo ya kutazamana sura yanafanyika.... mi nilifikiri ametimuliwa kazi kikwelikweli kumbe kaambiwa aende likizo tu wakati akisubiri kustaafu rasmi!
 
Back
Top Bottom