Mkuu wa mkoa wa Dar vipi?

Safi sana mbunge wa mafia. Huyo mchina kwenye boti naye aalinaswa mafurikoni?
 
Kwa mfano watu waliokwama kwenye paa za nyumba zao wanahitaji taarifa au wanahitaji chombo cha kuwafikisha sehemu kavu? Au hizi taarifa za helicopta zinamfanya mtu ghafla ajikute yuko sehemu kavu? Huyu mkuu wa mkoa kapatwa na ugonjwa gani?

Mie mara nyingi nasema; hizi post za kusaidia wahanga wakushindwa sehemu fulani- u DC, RC, sasa naona na Ubalozi ni mzigo tuu kwetu walipa kodi!

Maneno ya KIENYEJI kama aliyosema RC wa Dar yanachefua!
 
Kwa mfano watu waliokwama kwenye paa za nyumba zao wanahitaji taarifa au wanahitaji chombo cha kuwafikisha sehemu kavu? Au hizi taarifa za helicopta zinamfanya mtu ghafla ajikute yuko sehemu kavu? Huyu mkuu wa mkoa kapatwa na ugonjwa gani?
Kwanza natoa pole saana, kwa wote walioathirika kwenye janga hili. Tu pamoja nanyi kwenye wakati huu mgumu. Mwenyezi Mungu ni mwema, tuzidishe kumuomba, atufanyie wepesi mambo yetu. Pili kuhusu Helikopta za uokoaji ni maalum kwa kazi hiyo, na hata rubani wake anakuwa na mafunzo maalum. Sio mradi kudandia tu kama toroli la mizigo, vinginevyo yanaweza kutokea maafa zaidi kuliko manufaa.
 
LOL. Ningependa nimwelezee lakini nikielezea kama akiwa anasoma hapa atanifahamu.

Kwa kifupi Mheshmiwa Hana UWEZO wa kuongoza DAR.

Kwa sasa na mwanae naye Kapata kazi Ikulu, sijui ni dietician wa Mkulu JK au ni msaidizi au nimpishi, sijafuatilia. Ila ndo hivyo. Sio kama huyu dada (mtoto wa Mecky) hana uwezo....nasema hapana kamaliza SUA fresh tu ila swali linabakia: MTOTO WA MWINYIKIHERI MWAPIBUSIPELI WA KULE Namkarango Kyaratutuga Karatu; ATAPATA KAZI KWELI IKULU au kazi nzuri serikalini kwa mtindo huu?
 
nimemsikiliza uyu jamaa..co mtaalam ila ni mwanasiasa kama lowasa..huyu jamaa ni panzi..anaongea upupu

Mi namlaumu zaidi MEYA! Ama hayumo kamati ya maafa? Kwa mara ya kwanza ndiyo najua kazi ya RC! Simsahau Rudy Giulliani wakati wa twin towers..
 
Sioni msingi wa kumlaumu Mkuu wa Mkoa mlitaka atoe maelezo ya aina gani? Hatujawa na vitengo madhubuti vya maafa bado. Lakini kibaya zaidi watanzania tumeendekeza siasa kwa mfano wakati Waziri Tibaijuka alipotaka kuleta hoja ya kuwaondooa waliojenga mabondeni Wabunge wa Dar walifanya nini zaidi ya kutishia kuandamana kupinga mpango huo ili kulinda wapiga kura wao. mamlaka ya hali ya hewa imetoa tahadhari kabla na kuwataka waliopo mabondeni wahame bado watanzania hatujali maisha yetu tunaishi kiaina aina hivi.
 
Vitu muwe munajaribu ku reason, kama helcopter zilizopo si wa ajili ya uokozi mlitaka adanganye? Ili iweje?
Msidhani kila gari yenye uwezo wa kubeba maji kwa wingi inafa kutumika kwa shuguli za kuzima moto (Fire & Rescue).
Try to think Big.
 
Back
Top Bottom