Mkuu wa Mkoa Wa Dar es Salaam: Wananchi kutibiwa Hospitali Binafsi kwa Gharama za Serikali...

sosoliso

JF-Expert Member
May 6, 2009
8,539
9,462
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Sadick amesema Serikali katika moja ya mikakati yake ya muda mfupi wa kupambana na mgomo wa Madaktari.. italipa Gharama za wananchi watakaokwenda kupata huduma kwenye hospitali binafci..

Source Channel 10..

Mytake.. Hivi wameshafanya mchanganuo na kujua gharama halisi ya kuwatibu hao wagonjwa..? Wanazo hizo hela..? Waache kuchanganya siasa na maisha ya watu..
 
Kingine eti hosp za mwananyamala na Temeke zitaboreshwa ili ziwe kama Muhimbili. je Temeke na mwana hawajagoma? na walikuwa wapi? Mkuu wa mkoa alikuwa amelewa sijui maana hizi ni pumba tu
 
Serikali iseme sasa tunaenda kuchukua wapi pesa nami niende India kesho.........
Kazi ipo hakika hatuna viongozi watanzania
 
Kumbe urais wa Tanzania ni mwepesi sana,hata mimi naweza kua rais wa Tanzania
 
Waongo bila aibu. This is another type of EPA heading to 2015 elections.

Wanakusanya hela za kampeni kupitia mgomo wa ma dr.
 
Mama mjamzito akienda aga Khan kujifungua tena ikahitajika opereshen ni sh. mil mbili na ushee.
consultation na vipimo vya harakaharaka vya emergence si chini ya laki tatu.
nadhani wanaweza.
 
Hivi bado kuna watu wenye akili timamu ndani ya jeshi la Tz...???
Wanaiona hali hii na wameridhika nayo kabisa?!
 
Waongo bila aibu. This is another type of EPA heading to 2015 elections.

Wanakusanya hela za kampeni kupitia mgomo wa ma dr.

Kila janga linatumika vizuri.
Sijui hili wazo limetolewa na nani!
Lakini serikali yetu ina watu makini wanaosumbua akili zao.
This is a million dollar decision.
 
Ungemwangalia vizuri wakati anaongea hili, huenda alikuwa maeneo ya TBL

Ha ha ha.. mkuu alikuwa anawahutubia akina dada.. alikuwa mgeni rasmi kwenye sherehe ya siku ya wanawake.. So vle vigele gele vilimchanganya na kujikuta anaongea pumba pitiliza..
 
Kweli Tanzania ni nchi ya ajabu sana! Mtu huwezi kuongea upumbavu mkubwa namna hii halafu ukaendelea kubaki madarakani!
 
Back
Top Bottom