Mkuu wa Mkoa Mtwara atunukiwa Nishani na Papa Benedict XVII

Shida yako nishaijua kuwa huweki mpaka kati ya uhuru wa mtu, hasa kiongozi kuabudu na nafasi anayoiongoza.
Nyerere kupewa uwenye heri ni ishu ya Kitaifa au ya imani yake binafsi?...waumini wenzie wametambua kazi yake, na kwa mujibu wa dini yao wameamua kumuenzi, wewe inakuhusu nini?
Suala la Basaleh na Ponda ni tofauti sana...ugomvi wao ni wa powers, ambapo ni ishu ya katiba yao moja kwa moja..
Utawasuluhisha kidini, lakini kama katiba ni mbovu, your woirk is futile...right?

we kijana yaelekea upeo ni mdogo sana wa kuchambua mambo in general,unaweza kuwa umesoma lakini unakijua hicho ulichosomea tu,wapo wengi wasomi wa aina yako nchi hii,yani mpaka leo huelewi umuhimu wa viongozi wadini katika siasa,basi kazi ipo kukuelimisha,kwa hiyo wale watu wa cuf kuchomana visu pale manzese bado unaona ni issue ya kikatiba.....dogo mambo yanapoharibika katiba huwa inakaa pembeni ndio pale unaposikiaga kuna watu wanaitwa wapatanishi,hawa wanakuwa ni watu ambao hawana upande katika mgogoro husika mfano hapa ni huo wa power,hawa wanaweza kuwa wazee wnaoheshimika na pande zote au viongozi wa dini kijana,tatizo mnakariri kila kitu wasomi wetu wa siku hizi

Nyerere kupewa tuzo kweli inawza kuwa tuzo ya heshima kwa bongo lakini tatizo ni pale may be chuo kikuu cha kiislam cha misri kitakapompa kikwete tuzo ya heshima au mwinyi,je wote tutaiona tuzo hiyo kama heshima kwa nchi au?be honest hapa...kama kujiunga na OIC Tu jambo ambalo lilikua namanufaa kwa kila mwananchi kwa kunufaika na misaada mlilipinga kwa nguvu zote na mkafanikiwa,tatizo mnajipenda sana na kuwasahau wengine
 
Kwa mjibu wa Katekisimu ya Kanisa Katoliki (Paulines Publications Africa) ukurasa wa 227-228, kifungu cha 897-898

Kwa neno walei humaanisha hapa waumini wote, isipokuwa walio katika Daraja Takatifu au katika utawa unaotambuliwa na kanisa. Walei ni waamini wale, ambao, baada ya kuingizwa katika Kristu kwa ubatizo, na kwa kufanywa Taifa la Mungu, wamefanywa kwa namna yao washiriki wa kazi ya Kristo ya kikuhani, ya kinabii na ya kifalme. Hutekeleza kwa sehemu yao katika kanisa na katika ulimwengu utume ulio wa taifa lote la kikristo.
Wito ulio hasa wa walei ni katika kutafuta ufalme wa Mungu hasa kwa kujishughulisha na mambo ya kidunia na kuyaratibu hayo kadiri ya mpango wa Mungu. Ni wao hasa walio na wajibu, kwa namna ya pekee, kuyaangaza na kuyaratibu mambo yote ya kidunia, ambamo wanahusika moja kwa moja, kwa namna hii kwamba, yanafanywa na yatakuwa daima kwa kadiri ya mpango wa Kristo, na yanakuwa kwa ajili ya utukufu wa Muumbaji na Mwokozi. Niendelee?
 
aliyemtangaz uaminifu yeye pia anakabiliwa na ya kwake huko ujerumani ssa atakuchaguaje ww kama sio wale wale ,tusubili ya mzee wa siku yaani anayechagua pasipo upendeleo.mengine haya ya kiduna sana je?na ile ya nyerer kutangazwa sijui mtakatifu imefikia wapi
 
Bulesi,
Aliiba specifically nini akiwa NDC?...au ndo generalization ya mtu akiwa kiongozi mwandamizi?
Suala la kununua nyumba halikuwa conceived na yeye personally, bali ilikuwa ndio sera ya wakati huo wa Mkapa.
yeye kama mchamungu, akujua kama anatenda kosa?
 
KIONGOZI wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Benedict wa XVI amemtunuku nishani ya Mtakatifu Gregory Mkuu, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Joseph Simbakalia kwa utumishi uliotukuka kwa kanisa na jamii. Nishani hiyo ilikabidhiwa kwa Simbakalia aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma kwa karibu miaka sita, na Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Kigoma, Protas Rugambwa kwa niaba ya Papa katika misa ya Ibada ya Krismasi iliyofanyika kwenye Kanisa la Bikira Maria mshindaji mjini Kigoma.

Simbakalia alitiririkwa na machozi wakati akikabidhiwa nishani hiyo kutokana na kutoamini kile anachokiona hali iliyofanya kanisa kuzizima kwa hali hiyo katika tuzo hiyo ambayo ni ya kwanza kutolewa kwa muumini wa Kanisa Katoliki Jimbo la Kigoma tangu kuanzishwa kwake. Akikabidhi medali na hati ya nishani hiyo, Askofu Rugambwa alisema imetolewa katika kuunga mkono Jubilee ya miaka 50 ya Tanzania Bara ambayo kanisa iliona haina budi kushiriki kwa hali na mali kwa kufanya kitu ambacho kitakumbukwa kwa miaka 50 mingine.

Askofu Rugambwa alisema Simbakalia kama kiongozi wa kijamii, alitumia wakati wake kulitumikia kanisa na kuonesha mchango wake na utumishi wake kwa kanisa bila kujali mamlaka na madaraka aliyonayo. Akisoma hati hiyo, Katibu wa Kanisa hilo Jimbo la Kigoma, Kiliani Teleba alisema anamtangaza Joseph Simbakalia kutoka Jimbo la Kigoma kuwa shujaa wa ukoo bora wa Mtakatifu Gregory Mkuu wa Daraja la Kiraia na kumpatia uwezo wa kutumia haki zote zinazotokana na hadhi hiyo. Akishukuru kwa nishani aliyotunukiwa na heshima aliyopewa, Simbakalia alisema wakati akija Kigoma kutumikia nafasi yake ya ukuu wa mkoa, hakuwaza kama siku moja atatunukiwa heshima hiyo kubwa katika kanisa.

Alisema amekaa Kigoma kwa zaidi ya miaka mitano, anaamini amefanya kile alichotumwa kuja kufanya na nishani hiyo ni heshima kwake wananchi wa Mkoa wa Kigoma na Tanzania kwa jumla kwa heshima waliyopewa ndiyo maana Mungu ameonesha uwezo wake kwa nishani hiyo na heshima aliyopewa. Naye mke wa Mkuu huyo wa Mkoa, Janet Simbakalia alisema wakati mume wake alipoteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma kutoka kuwa Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC), walijua ni kumkomoa, lakini Mungu ameonesha shani yake kwa yale yote aliyofanya alipokuwa Kigoma.

Habari Leo
 
Akisoma hati hiyo, Katibu wa Kanisa hilo Jimbo la Kigoma, Kiliani Teleba alisema anamtangaza Joseph Simbakalia kutoka Jimbo la Kigoma kuwa shujaa wa ukoo bora wa Mtakatifu Gregory Mkuu wa Daraja la Kiraia na kumpatia uwezo wa kutumia haki zote zinazotokana na hadhi hiyo.

Habari Leo

Hapo kwenye red hapo. Emu tufafanulieni sisi wengine tusiofahamu hizo haki!
 
Hapo kwenye red hapo. Emu tufafanulieni sisi wengine tusiofahamu hizo haki!

kwa ufahamu wangu mdogo wa masuala ya kanisa Mt. Gregory mkuu ni moja ya watu mashuhuri sana katika kanisa katoliki duniani hivyo Simbakalia kuhesabiwa kama moja ya wanaukoo ni hadhi na sifa kubwa sana kwa kanisa la Tanzania na familia yake kwa ujumla. Kuna haki kadhaa anazokuwa entitled nazo unapokuwa kwenye mmoja ya wanafamilia kama hii mfano kila wanapoadhimisha kumbukumbu ya Mt. Gregory Mkuu basi ni lazima wanafamilia mshirikishwe kwa ukaribu pia anakuwa na ruhusa ya kutumia jina la Mt. Gregory Mkuu katika majina yake kama sijakosea ngoja nitawasiliana na wakuu wa kanisa wanipe details kwa undani
 
Hapo kwenye red hapo. Emu tufafanulieni sisi wengine tusiofahamu hizo haki!

kumpatia uwezo wa kutumia haki zote zinazotokana na hadhi hiyo.

Ukitaka kujua maana na heshima aliyopata ya Mtakatififu Gregory Mkuu soma yafuatayo:

Doctor of the Church; born at Rome about 540; died 12 March 604. Gregory is certainly one of the most notable figures in Ecclesiastical History. He has exercised in many respects a momentous influence on the doctrine, the organization, and the disciplineof the Catholic Church. To him we must look for an explanation of the religious situation of the Middle Ages; indeed, if no account were taken of his work, the evolution of the form of medieval Christianity would be almost inexplicable. And further, in so far as the modern Catholic system is a legitimate development of medieval Catholicism, of this too Gregory may not unreasonably be termed the Father. Almost all the leading principles of the laterCatholicism are found, at any rate in germ, in Gregory the Great. (F.H. Dudden, "Gregory the Great", 1, p. v).

Kwa habari zaidi bovya hapa CATHOLIC ENCYCLOPEDIA: St. Gregory the Great kupata kinogaubaga cha Gregory Mkuu.

Kwa nyongeza tu ndiye aliyeweka vizuri mfumo wa utaratibu wa nyimbo za liturujia kufuata majira ya mwaka wa kanisa inayojulikana kama Gregorian Chant. Yale mavitabu makubwa meusi ya nyimbo za kilatini ambayo hadi leo yanatumika ndiye mwanzilishi. "Kyrie eleison, Groria in excesis Deo, Credo in unum... Santus, Pater, Agnus dei quitolis pecata mundi miserere nobis, Ite misa Est, nk.

Kwa lugha nyepesi ndiye aliyeratibu mfumo mzuri wa choir unaoendana na theme ya siku husika, badala ya kujiimbia tu kiholela kile moyo unapenda, ila lazima kile kinachosomwa kwenye masomo ya ibada ndicho kiimbwe.




 
kwa ufahamu wangu mdogo wa masuala ya kanisa Mt. Gregory mkuu ni moja ya watu mashuhuri sana katika kanisa katoliki duniani hivyo Simbakalia kuhesabiwa kama moja ya wanaukoo ni hadhi na sifa kubwa sana kwa kanisa la Tanzania na familia yake kwa ujumla. Kuna haki kadhaa anazokuwa entitled nazo unapokuwa kwenye mmoja ya wanafamilia kama hii mfano kila wanapoadhimisha kumbukumbu ya Mt. Gregory Mkuu basi ni lazima wanafamilia mshirikishwe kwa ukaribu pia anakuwa na ruhusa ya kutumia jina la Mt. Gregory Mkuu katika majina yake kama sijakosea ngoja nitawasiliana na wakuu wa kanisa wanipe details kwa undani

Nashukuru kwa kunijuza Mkuu. Endelea kutafuta 'MADESA' ya ziada utuwekee hapa jamvini.

 
Mkuu huenda ameelekeza utumishi uliotukuka kanisani na kusahau majukumu ya serikali!

Jambo moja ambalo naweza kujifunza toka kwa huyu Mkuu wa Mkoa ni uwajibikaji wake kwa dini yake bila kuingiliana na mambo ya majukumu yake serikalini. Viongozi wengi wawapo na vyeo serikalini hujiona kama heshima ile wanatakiwa waipate tena hata kanisani badala ya kutumikia kanisa.

Rais wa zamani wa Zambia Keneth Kaunda licha ya kuwa mkuu wa nchi anapoenda kanisani aliomba apangiwe jukumu la kufanya, hivyo kanisa lilimpa kujumu la kusoma moja ya masomo katika ibada, alijisikia kushirikiana na wamumi wengine akiwa kama muumini si kama rais kinyume cha wengi wetu kujiona miungu.
 
Hawa wenzetu huwa wanafanya kazi mbili. Kwanza kanisa halafu serikali na wananchi baadaye. Jamaa amepewa tuzo kutokana na kutekeleza matakwa ya kanisa ktk shughuli zake za kila siku za serikali. Kwa kusimamia mambo ya kanisa akiwa kama mtumishi wa serikali wakubwa huko Vatican wameona bora wamtunuku tuzo ili kuwatia moyo wakereketwa wengine wa kanisa kuendeleza hiyo ajenda. Kwa mwenendo huu Waislamu andikeni maumivu zaidi.
 

Askofu Rugambwa alisema Simbakalia kama kiongozi wa kijamii, alitumia wakati wake kulitumikia kanisa na kuonesha mchango wake na utumishi wake kwa kanisa bila kujali mamlaka na madaraka aliyonayo.
Habari Leo

Behind the scene....
 
Back
Top Bottom