Mkuu wa Chuo Cha Kikuu cha Mkwawa Aliyekula hela za Mikopo ya Wanafunzi naye Awajibishwe.

Kinyungu

JF-Expert Member
Apr 6, 2008
17,369
33,012
Juzi tarehe 21/04/2012 wakati wa kikao cha bunge jioni Mbunge wa Ludewa Mh. Deo Fulukunjombe alimtaja mkuu wa Chuo Cha Mkwawa kuwa alishiriki kula hela za mikopo ya Wanafunzi wa chuo hicho na hivyo kupelekea wanafunzi wa chuo hicho kugoma na hatimaye kupigwa mabomu na polisi.

Mh. Fulukunjombe alienda mbali na kusema Wanafunzi waliopigwa mabomu walionewa na aliyestahili haswa kupigwa mabomu ni huyo mkuu wa Chuo hicho ambaye alikula hela ya wanafunzi na kupelekea mgomo ule.

Kwa hili vugu vugu hili la uwajibikaji linalowakabili mawaziri wezi tunamtaka na mkuu huyo wa chuo cha mkwawa naye ajiuzulu na hatimaye sheria ichukue mkondo wake.

Kama kuna anayejua jinala mkuu huyo atuwekee hapa
 
Prof. Philimon Mushi anazijua ngawila toka tumboni mwa mama yake
 
Hao ndio maprofesa wa kibongo ambao michango yao haionekani kwa taifa.Hakuna kuangalia uso wa m2 hapa,lishitakiwe haraka.
 
Back
Top Bottom