Job K
JF-Expert Member
- Oct 4, 2010
- 9,315
- 7,113
tatizo tunasubiri watawala walete mageuzi na kubadili katiba ili kubadilisha hali hii, hicho hakiwezekani ndugu yangu!!!
Kwa nini tusubirie wjukuu watuone na wakati sisi ndio tunaishi sasa na hatujafa bado!?
Badala ya kufa 'kibudu' na kuacha aibu ya kuishi ni kwa nini tusife na kuacha heshima nyuma!!???
"Tunaweza kufanya chochote kuweka sawa mambo" ...ndiyo sentensi ya kufanyia kazi!
Kwani bado wewe unawaamini (kwenye red hapo)
Sasa Mkuu tutafanyaje? (hapo kwenye red). Inabidi kuwaamini tu hivyo hivyo labda watakuja kubadilika? Juzi nikamsikiliza bwana mmoja ameletwa kwenye mdahalo wa umeme, haki ya nani ilikuwa ni aibu! Eti Engineer lakini hawezi kujieleza? Aaaaaagh! Yaani kwa kweli TZ tuna laana! Angalia wanasheria wanavyotuangusha na mikataba mibovu mibovu, njoo kwa wanauchumi, nenda kwa madaktari wa binadamu, tazama walimu. Kila sekta uozo mtupu, sasa tutatoka kweli?
Kuna mwaka niliwahi kusoma utafiti uliofanywa kwenye nchi za EAC (wakati huo zikiwa nchi 3), ikaonekana TZ wanajua kupanga mipango ila utekelezaji ni 0, Kenya hawajui kupanga, ila hata kile kibovu wanachokipanga wanajua kutekeleza, Uganda yenyewe ilionekana ni wazuri kwa ku-copy and paste na kile walichoiba kutoka kwingine wanakitekeleza kwa ufasaha.
Hebu wasomi wetu watuokoe na hili janga. Mawaziri kwenye vikao kazi yao ni kuchapa usingizi tuuuuuuu! Hawaji na mbinu mbadala za kuiokoa nchi na huu umasikini. Kama wakulima wetu wadogo wagekuwa wanatusikia tungeking'oa hiki chama madarakani tukajaribu na gari jingine maana hawa naona uwezo wao wa kufikiri umefikia kikomo.