Mkutano wa wawekezaji - Rukwa

jambo la kushangaza kapew mmraekani zaidi hekari 250,000 na atalipa kwa mwaka Tsh 700 @hekari ikiwa na mgawanyo Tsh 200 kwa halmashauri husika na Tsh 500 kwa serikali kuu
hii ni ujinga iliopita kiwango hakuna mwenye uchungu na nchii hii ardhi hii wangepewa watz wao wangezalisha vizuri
viongozi hajiamini na hawawamini watu wao kuwa wanaweza ila anayeweza ni mzungu tu na hii ni falasafa ya mtu mweusi
 
Huu ni ukanda ambao umeishatengwa kuwa 'JATROPHA CAPITAL' duniani for better or for worse. Katika picha ya washiriki wawekezaji unaweza ukabaini kuwa idadi ya akina kanjibahi ni kubwa - hao ndio vinara wa jatropha industry duniani. Perhaps we need to look at this initiative with an open mind:
"...Jatropha seeds are also very resilient against diseases and poor soil conditions. Because the Jatropha tree can grow on inferior soil, infertile land that is thereby effectively upgraded for usage. Jatropha plantations thus play an important role in the reforestation and reclaiming of derelict tracts of land in developing economies, providing real income in regions with an impoverished populace.
Jatropha offers the best possible proposition of all biofuel crops as it is a toxic crop that does not compete with food production. Jatropha actually augments the food chain because food crops may be interbred between the trees on the plantations. A well balanced intercropping scheme enhances a symbiotic and complimentary plant relationship to the benefit of both, food and fuel crops. Moreover, Jatropha generates very effective organic fertilizers as a by-product." (jatrophainternational.com))
:focus:
 
Huu ni ukanda ambao umeishatengwa kuwa 'JATROPHA CAPITAL' duniani for better or for worse. Katika picha ya washiriki wawekezaji unaweza ukabaini kuwa idadi ya akina kanjibahi ni kubwa - hao ndio vinara wa jatropha industry duniani. Perhaps we need to look at this initiative with an open mind:

Kwahiyo wakulima wazawa wakipanda hizi mbegu hazikui mpaka tuombe watu nje waje watupandie, tena basi wanachukua ardhi nzuri na yenye rutuba..., si waende jangwani wakapande kama kweli this plant is drought resistant
 
Kwanini hawaendi Singida na Dodoma ambapo Jatropha ni indigenous plant na ni dry area wanaenda Rukwa kwenye fertile land?
 
Kwanini hawaendi Singida na Dodoma ambapo Jatropha ni indigenous plant na ni dry area wanaenda Rukwa kwenye fertile land?

Kweli kabisa hizi story za uwekezaje ni kupiga propaganda na kuwahadaa wananchi wakati watu wanauza nchi, mbaya zaidi watakaopata sana shida ni wajukuu zetu.., na watatuona sisi babu zao tulikuwa wapuuzi wakubwa.
 
Lake Tanganyika kuna oil exploration. Ukanda unaanzia kivu mpaka chini. Ni mahesabu mazuri kuanza kuinvest huko, haya mambo ya kilimanjaro yanatuyeyusha!
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Kwahiyo wakulima wazawa wakipanda hizi mbegu hazikui mpaka tuombe watu nje waje watupandie, tena basi wanachukua ardhi nzuri na yenye rutuba..., si waende jangwani wakapande kama kweli this plant is drought resistant
Jamani kilimo cha kibiashara kinahitaji utaalam na capital investment kubwa. Hili swala la kudhani kuwa wakulima wadogo wanaweza kuwa transformed kuwa wakulima wa kisasa ni very theoretical. Wawekezaji katika kilimo ni muhimu kwa sasa ili thru wao watu wetu watajifunza na baadae kuweza kulima kisasa. By the way wawekezaji katika kilimo hakuanza leo wala jana. Tuwe na positive mind katika baadhi ya initiatives.
 
Jamani kilimo cha kibiashara kinahitaji utaalam na capital investment kubwa.

Utaalam?? Hivi hawa jamaa wanaokesha kufundisha na kufundishwa pale SUA ni wa kazi gani?
Capital Investment?? Hivi kazi ya Serikali siyo kuwawezesha wananchi wake ili waweze kuzalisha kikubwa na serikali kupata kodi..

Hivi kama nchi za hao wawekezaji zisingeweka mazingira mazuri kwa wananchi wake kwa kuwawezesha kihali na kimali,unadhani leo hii wangekuwa wanatamba kuja kuwekeza huku kwetu? Serikali lazima ibadili mtazamo wake kuhusu uwekezaji manake ishadhihirika watanzania hatufaidiki kulingana na rasilimali zetu tunazowagawia hao wawekezaji..Serkali lazima iwekeze kwa watanzania ili hiyo miradi mikubwa ifanywe na msukuma,myao,mjaluo mmakua n.k..
 
Nafikiri kinacho kosekana hapo ni uzoefu wa shughuli za kilimo takita ukiliima mkubwa! niamabie wapi tumekuwwa na ukulima mkubwa unao tuwezesha kutoka kifua mbele na kusema mashamba fulani yanao uwezo wa kulisha au kukidhi mahitaji ya nchi hii kama si porojo na njia za kutufanya mazuzu waliwao?
 
Jamani kilimo cha kibiashara kinahitaji utaalam na capital investment kubwa. Hili swala la kudhani kuwa wakulima wadogo wanaweza kuwa transformed kuwa wakulima wa kisasa ni very theoretical. Wawekezaji katika kilimo ni muhimu kwa sasa ili thru wao watu wetu watajifunza na baadae kuweza kulima kisasa. By the way wawekezaji katika kilimo hakuanza leo wala jana. Tuwe na positive mind katika baadhi ya initiatives.

Kwani sisi hatuwezi kuwa wakulima wakubwa ama mpaka awe foreigner? Acheni utumwa wa akili jamani....kuna technology gan ya kwenye kilimo ambayo hatuna wataalamu Tanzania? Kwa taarifa yako hakuna fani yenye wasomi wengi nchini kama kilimo tena kwenye kila fani au una dhani watu wakisema capital wanamaanisha pesa? Basi kama ndivyo wachukue hao wataalamu geuza value zao kwenye pesa; chukua ardhi iweke kwenye fedha na labor iliyopo alafu rudi hapa kutuambia ni kiasi gani cha dollar utuambie hatuna capital. Botswana ambayo inaendelea kupaa kwaajili ya kilimo na madini ilikuwa inatumia wataalamu wetu wa Kilimo na mpaka leo wengine bado wapo huko. Tatizo letu kubwa ni la uongozi na sera zake no more no less!
 
]Jamani kilimo cha kibiashara kinahitaji utaalam na capital investment kubwa[/B]. Hili swala la kudhani kuwa wakulima wadogo wanaweza kuwa transformed kuwa wakulima wa kisasa ni very theoretical. Wawekezaji katika kilimo ni muhimu kwa sasa ili thru wao watu wetu watajifunza na baadae kuweza kulima kisasa. By the way wawekezaji katika kilimo hakuanza leo wala jana. Tuwe na positive mind katika baadhi ya initiatives.

Mkuu capital investment kiasi gani na je wataalamu hata kama hawapo hatuwezi kuwaleta watoe education au vyuo kama suia vina kazi gani..?

Kumbuka mimi sisemi kila mkulima abaki na jembe lake au hekari moja au mbili hapana bali badala ya kuwapa hawa jamaa ardhi yetu kwa faida yao na kumaximize profit yao ni bora hii ardhi wapewe vyama vya ushirika ambavyo vitawezeshwa na kuzalisha kisasa kwa manufaa ya jamii husika na nchi kwa ujumla.., yaani 100% iwe mali ya wananchi hakuna sababu ya kugawana keki yetu na watu wa nje eti hatuna capital investment...

Watu kama Libya waliweza kutengeneza the biggest man made river in the world bila hata mkopo kidogo kutoka nje sisi hata kuanzisha kilimo cha kisasa hatuwezi..., mkuu tafadhali tuondokane na hizi fikra potofu.., kama wenyewe wachache wanaweza kwanini na serikali na wananchi isianzishe corporation tuone tutafika wapi?

Big four wameweza kutulisha na jembe la mkono leo unasema hawawezi kwa msaada kuangalia mashine na matrekta yanafanya kazi usiku na mchana...? Give me a Break !!!
 
Wawekezaji katika kilimo ni muhimu kwa sasa ili thru wao watu wetu watajifunza na baadae kuweza kulima kisasa. By the way wawekezaji katika kilimo hakuanza leo wala jana. Tuwe na positive mind katika baadhi ya initiatives.

Ha ha haa kwahiyo baadae wakishajifunza na wameshakufa hao wakulima wawekezaji watawaambia hao wajukuu wa wakulima ahh mmeshajifunza ndugu zetu haya chukueni hizi ardhi zote na hizi mashine ili kuendeleza kilimo sisi tunaondoka tunashukuru sana kwa kutoa elimu...!!! ??

Mkuu kilimo kikubwa nchi zote kinaendeshwa na big corporations point yangu ni kwamba kwanini hizo big corporations isiwe home born vyama vya ushirika kwa niaba na manufaa ya mwananchi, yaani sio profit driven peke yake bali service driven ili kutoa service na welfare kwa wananchi wake.
 
Nafikiri kinacho kosekana hapo ni uzoefu wa shughuli za kilimo takita ukiliima mkubwa! niamabie wapi tumekuwwa na ukulima mkubwa unao tuwezesha kutoka kifua mbele na kusema mashamba fulani yanao uwezo wa kulisha au kukidhi mahitaji ya nchi hii kama si porojo na njia za kutufanya mazuzu waliwao?

Mkuu baada ya kuua vyama vyama vya ushirika na kuacha kuwekeza kwenye kilimo serikali yenyewe badala ya ku-mobilize watu walime pamoja na kuleta mashine za kisasa wanatoa power tillers.., mazao yanaoza shambani sababu hakuna miundo mbinu wewe unategemea nini..., tatizo hapa ni kwamba tuna serikali ya 10% na wapiga porojo ambao hawana vision..,

Na huu uzoefu wa ukulima mkubwa unapatikana kwa kuuza ardhi..?, na kule SUA hivi wanafundishwa kufanya nini..? kutibu mbuzi na bata ? au kumfanyia kazi mwekezaji?
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Mkuu we need global companies in technology sectors, we need global companies in things we cant do.., we need global companies if they can to come here and build their industries to increase employment.

What we don't need is to give these people our fertile land to till (something which even the local mkulima has been able to till the land with jembe la mkono na kulisha nchi).. We dont need this global companies to do something which we can do ourselves and keep all the profits..!! How much does it cost ku-invest kwenye umwagiliaji (and some places we dont even need kumwagilia..!!) how much does it cost to buy combined harvesters and big machines which can till the land night and day... mhhh Okay tell me hatuwezi kuwa na vyama vya ushirika vikafanya hayo hapo juu...

Kwanini tuweke rehani mtaji wa wajukuu zetu...!!??? (hii ni kama mtu mtaji wa pesa unao, unaweza kuzalisha mwenyewe lakini unaita jirani akuzalishie ili mgawane mapato.., tena wewe akupe kidogo..)

VoR hapo umesema kweli mkuu!

Tatizo hii nchi sijui tunakosa kitu gani hata nashindwa kuelewa! wasomi wetu tunaowaamini ndo hao hata hawawezi kujieleza vizuri wakaeleweka. Tuna wasomi waliobobea kwenye uchumi lakini yote hayo hawayaoni. Tangu lini ukaagiza wakulima kutoka nje? Si ujinga huu! Nchi inashindwaje kuwawezesha hawa wakulima wetu wakaitumia ardhi kikamilifu kuzalisha mazao ya chakula na biashara? Ingependeza sana kama hao wanaoitwa wawekezaji wangekuja kujenga viwanda (ingawa Ngeleja naye kanuna) vya kusindika hayo mazao ya wakulima na hao wakulima wakapata soko la uhakika.

Utasikia hao wawekezaji wanaomegewa ardhi yetu wanalima na kusafirisha mazao hayo kwenda nchini kwao ambako ndo kutakuwa na viwanda vya kusindika hayo mazao na hivyo kuongeza ajira nchini kwao. Subiri uje uone kama Wa-Kenya hawatamiminika hapa kwa mlango wa uwekezaji na kujichukulia ardhi yetu, mara utasikia ardhi yetu inatumika kuzalisha Jatropha! Nchi la wajinga hili!!

Leo hii wafugaji wanaishi kwa hofu katika nchi yao huku ardhi ambayo ingegawiwa kwa wafugaji inaporwa kwa mlango wa uwekezaji! Kuna faida gani nchi kujivunia wingi wa mifugo wakati wafugaji hawajawekewa mazingira wezeshi? Leo hii tunapiga mbiu dunia nzima inatusikiliza eti Tanzania ni nchi ya 3 kwa wingi wa mifugo barani Afrika, lakini hapo hapo wafugaji wananyanyasika na hakuna mtu wa kuwasemea! Hivi nchi hii inashindwa nini kumega ardhi ya kutosha na kuwagawia hao wafugaji wakafuga kibiashara?

Bila kuing'oa hii Serikali ya magamba tumekwisha!
 
tatizo tunasubiri watawala walete mageuzi na kubadili katiba ili kubadilisha hali hii, hicho hakiwezekani ndugu yangu!!!
Kwa nini tusubirie wjukuu watuone na wakati sisi ndio tunaishi sasa na hatujafa bado!?
Badala ya kufa 'kibudu' na kuacha aibu ya kuishi ni kwa nini tusife na kuacha heshima nyuma!!???
"Tunaweza kufanya chochote kuweka sawa mambo" ...ndiyo sentensi ya kufanyia kazi!
Kweli kabisa hizi story za uwekezaje ni kupiga propaganda na kuwahadaa wananchi wakati watu wanauza nchi, mbaya zaidi watakaopata sana shida ni wajukuu zetu.., na watatuona sisi babu zao tulikuwa wapuuzi wakubwa.
Kwani bado wewe unawaamini (kwenye red hapo)
VoR hapo umesema kweli mkuu!
Tatizo hii nchi sijui tunakosa kitu gani hata nashindwa kuelewa! wasomi wetu tunaowaamini ndo hao hata hawawezi kujieleza vizuri wakaeleweka. Tuna wasomi waliobobea kwenye uchumi lakini yote hayo hawayaoni. Tangu lini ukaagiza wakulima kutoka nje? Si ujinga huu! Nchi inashindwaje kuwawezesha hawa wakulima wetu wakaitumia ardhi kikamilifu kuzalisha mazao ya chakula na biashara? Ingependeza sana kama hao wanaoitwa wawekezaji wangekuja kujenga viwanda (ingawa Ngeleja naye kanuna) vya kusindika hayo mazao ya wakulima na hao wakulima wakapata soko la uhakika.
.....
...
Bila kuing'oa hii Serikali ya magamba tumekwisha!
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Jamani kilimo cha kibiashara kinahitaji utaalam na capital investment kubwa. Hili swala la kudhani kuwa wakulima wadogo wanaweza kuwa transformed kuwa wakulima wa kisasa ni very theoretical. Wawekezaji katika kilimo ni muhimu kwa sasa ili thru wao watu wetu watajifunza na baadae kuweza kulima kisasa. By the way wawekezaji katika kilimo hakuanza leo wala jana. Tuwe na positive mind katika baadhi ya initiatives.

Kiimo cha kibiashara hakiwezi kutegema wawekezaji kutoka nje peke yake. Kwa nini Serikali isiwawezeshe hao wakulima wadogo wakapanua kilimo chao. Kwa mfano kuondokana na kilimo cha kutumia jembe la mkono na kuingia kwenye kilimo cha kutumia machinery hapo hapo wataalamu wetu wakiwafundisha wakulima kuhusu utunzaji wa mazingira. Sasa kichekesho cha Serikali ya magamba wao wakaona kilimo kitainuka kwa kutumia Power Tillers (Pinda's Machineries) matokeo yake zimeshindwa kufanyakazi kwenye maeneo mengi ya nchi yetu na karibia vingi vitauzwa kwenye vyuma chakavu (AIBU KWA SERIKALI YETU!).

Ili kupanua ajira Serikali imeshindwaje kuwawezesha vijana wanaomaliza masomo yao kwenye vyuo vya kilimo ili wajiingize moja kwa moja kwenye shughuli za kilimo na ufugaji? Sasa huko kukimbilia wawekezaji wakubwa madhara yake ni makubwa sana kuliko tunavyofikiria (hapa inajumuisha upatikanaji wa ardhi yenye rutuba kwa mkulima mdogo, bei ya mazao ya mkulima mdogo, uzalishaji wa mazao kwa mkulima mdogo, upatikanaji wa pembejeo kwa mkulima mdogo n.k). Hivyo kama tutajiingiza kwenye kilimo cha kutegemea wakulima wakubwa tutarajie hapo baadaye wajukuu zetu hawatakuwa na ardhi tena ya kulima na hii itawafanya wakulima wadogo kubaki vibarua kwenye mashamba makubwa ya wawekezaji!

Hivyo sikubaliani na wewe kabisa katika suala la kutegemea ukulima mkubwa (tena wa kutegemea wawekezaji wa nje). Tunatengeneza bomu hapa!!
 
VoR hapo umesema kweli mkuu!

Tatizo hii nchi sijui tunakosa kitu gani hata nashindwa kuelewa! wasomi wetu tunaowaamini ndo hao hata hawawezi kujieleza vizuri wakaeleweka. Tuna wasomi waliobobea kwenye uchumi lakini yote hayo hawayaoni. Tangu lini ukaagiza wakulima kutoka nje? Si ujinga huu! Nchi inashindwaje kuwawezesha hawa wakulima wetu wakaitumia ardhi kikamilifu kuzalisha mazao ya chakula na biashara? Ingependeza sana kama hao wanaoitwa wawekezaji wangekuja kujenga viwanda (ingawa Ngeleja naye kanuna) vya kusindika hayo mazao ya wakulima na hao wakulima wakapata soko la uhakika.

Utasikia hao wawekezaji wanaomegewa ardhi yetu wanalima na kusafirisha mazao hayo kwenda nchini kwao ambako ndo kutakuwa na viwanda vya kusindika hayo mazao na hivyo kuongeza ajira nchini kwao. Subiri uje uone kama Wa-Kenya hawatamiminika hapa kwa mlango wa uwekezaji na kujichukulia ardhi yetu, mara utasikia ardhi yetu inatumika kuzalisha Jatropha! Nchi la wajinga hili!!

Leo hii wafugaji wanaishi kwa hofu katika nchi yao huku ardhi ambayo ingegawiwa kwa wafugaji inaporwa kwa mlango wa uwekezaji! Kuna faida gani nchi kujivunia wingi wa mifugo wakati wafugaji hawajawekewa mazingira wezeshi? Leo hii tunapiga mbiu dunia nzima inatusikiliza eti Tanzania ni nchi ya 3 kwa wingi wa mifugo barani Afrika, lakini hapo hapo wafugaji wananyanyasika na hakuna mtu wa kuwasemea! Hivi nchi hii inashindwa nini kumega ardhi ya kutosha na kuwagawia hao wafugaji wakafuga kibiashara?

Bila kuing'oa hii Serikali ya magamba tumekwisha!

Ndugu yangu ukifanya hivyo change kama za rada (10% ambayo ilitakiwa iwe zaka kwa Mungu CCM na members wake walafi wameamua kula laana kwakuifanya yao) kwa cash zitatoka wapi ili kuhonga wapiga kura na kutambia wadanganyika? Au umesahau mhimili mkuu wa CCM ni ufisadi? Not until we remove hawa mafisadi kwa nguvu ya umma!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom