Wakuu kifupi Mwakyembe amesema YEYE alishajiondoa kwenye kampuni kama mwana hisa lakini yeye pamoja na wabunge wengi wanaiunga mkono kampuni hii na wanaendelea mpaka sasa kuwa interested nayo kwani ni ya wazalendo na haijawahi kupata mkopo toka benki yoyote japo ni ya wazawa.
Nadhani kwa sasa niwaachie uwanja wakuu... Am around
Mkuu Ivisible,
Kwanza asante sana kwa kutupasha hii press conference ya mheshimiwa.
Kama waandishi wa Tanzania wanajua kwenda chini kufuatilia info, huenda hili jambo likazua mambo mengine kibao.
Kama mheshimiwa ka transfer hizo shares zake inatakiwa awe amelipa pesa nyingi kweli kwenye hiyo process, kwa mtaji wa karibu bilioni 2, huenda ikawa mamilioni. Bila kufanya hayo malipo, hata ukirudisha hizo form zinakuwa hazina maana na bado unaendelea kuwa mmiliki wa shares hizo. Kama nakumbuka vizuri inatakiwa kulipa TRA 1% ya thamani ya shares kabla ya BRELA kuhalalisha hiyo transfer. I hope Dr. alifanya hivyo.
Labda mnaojua sheria ya kuuza au ku transfer shares ikoje naomba tuelemisheni zaidi.