Mkutano wa Mwakyembe na Hoja za Mgongano wa Maslahi

Anasema:

Dhamira ya kampuni ile ni kuzalisha umeme wa Megawati 1800 na hakuna kampuni hata moja kwa Tanzania itaweza.

Na anasisitiza ziangaliwe annual returns za kampuni hiyo za mwaka 2007/08 tutagundua kuwa shares zilishakuwa transfered siku nyingi.

Ameulizwa kuwa ametoa tuhuma kadhaa kwa RA na wote wawili ni wajumbe wa NEC... Haoni kama baadae itakuwa tatizo?

Kajibu: Hilo swali angeulizwa Rostam, kwakuwa yeye ndo anayefanya kuchafua wenzake na anajua siku si nyingi mambo yake (RA) yatalipuka tu.

Conference imeisha wakuu
 
Anasema: "Sina mkataba na Bunge. Nina profession yangu na natamani mambo mengi kama mtanzania."

Anasema kuna projects nyingi ambazo ameziona zimeandaliwa ili ziwe read story za kumchafua Mwakyembe.

Anasema kuna magazeti yanayoandika "Sasa Umoja wa Mataifa unamuunga mkono dhidi ya Mwakyembe". Anasema Profession ya uandishi wa habari imeingiliwa!

umoja wa mataifa unamuunga mkono nani dhidi ya Mwakyembe kuhusu nini?
 
Nimechoshwa na siasa za Tanzania hasa awamu hii ya nne. Yaani zimeishusha siasa kiasi kwamba ni afadhali ukawe mchunga ng'ombe. Kila siku ni scheming after scheming. Watu hawana mikakati ya kuiendeleza nchi. Afadhali hata mchunga ng'ombe anakuwa na mikakati ya kuendeleza uzazi wa mifugo yake
 
Mkuu

Tukipata "FULL TEXT" ya hii press conf tutashukuru sana...

So far asante sana kwa updates
 
Anasema kuna watanzania wangapi ambao wanaweza ku-declare interest kwenye mambo kadhaa ati kwakuwa wamesajili kampuni tu?

Akatoa mfano: Kuna waandishi wangapi wamesajili magazeti na hawajaacha kazi kwakuwa wameanzisha magazeti?

Akauliza tena: Ingewezekana vipi afanye ku-declare interest kwa kusajili kampuni tu ati akiwa na memorandum of articles? Anasema labda itawezekana lakini si rahisi kwa sababu unakuwa huna kazi in hand.

Anajikanganya, umekosea umekosea tu. Huwezi toa mifano kuwa kuna watanzania kibao wanafanya hivyo. Kwani kuwa watanzania wangapi wezi, kama kuna watanzania wezi haimaanishi tuhalalishe wizi. Kumbe naye ni JUHA kama CCM wenzake. Kwenda zako Mwakyembe na liCCM lenu.
 
Wakuu kifupi Mwakyembe amesema YEYE alishajiondoa kwenye kampuni kama mwana hisa lakini yeye pamoja na wabunge wengi wanaiunga mkono kampuni hii na wanaendelea mpaka sasa kuwa interested nayo kwani ni ya wazalendo na haijawahi kupata mkopo toka benki yoyote japo ni ya wazawa.

Nadhani kwa sasa niwaachie uwanja wakuu... Am around
 
Anasema:

Dhamira ya kampuni ile ni kuzalisha umeme wa Megawati 1800 na hakuna kampuni hata moja kwa Tanzania itaweza.

Na anasisitiza ziangaliwe annual returns za kampuni hiyo za mwaka 2007/08 tutagundua kuwa shares zilishakuwa transfered siku nyingi.

Ameulizwa kuwa ametoa tuhuma kadhaa kwa RA na wote wawili ni wajumbe wa NEC... Haoni kama baadae itakuwa tatizo?

Kajibu: Hilo swali angeulizwa Rostam, kwakuwa yeye ndo anayefanya kuchafua wenzake na anajua siku si nyingi mambo yake (RA) yatalipuka tu.

Conference imeisha wakuu

Vita vya panzi furaha ya kunguru, sisi tuendelee kununua popcorns, hili sinema haliishi leo.
 
Anajikanganya, umekosea umekosea tu. Huwezi toa mifano kuwa kuna watanzania kibao wanafanya hivyo. Kwani kuwa watanzania wangapi wezi, kama kuna watanzania wezi haimaanishi tuhalalishe wizi. Kumbe naye ni JUHA kama CCM wenzake. Kwenda zako Mwakyembe na liCCM lenu.

umepewa code umeshindwa kuelewa may be unahitaji na tone.
Huwezi kuogopa kusema maovu ya Richmond or whoever kwa kuogopa kuonekana na conflit of interest,hey wake up!
 
Anasema:

Ameulizwa kuwa ametoa tuhuma kadhaa kwa RA na wote wawili ni wajumbe wa NEC... Haoni kama baadae itakuwa tatizo?

Kajibu: Hilo swali angeulizwa Rostam, kwakuwa yeye ndo anayefanya kuchafua wenzake na anajua siku si nyingi mambo yake (RA) yatalipuka tu.

Something is is truly COOKING!

Tujipe muda tu - kabla ya June 2010 hata Mwalimu anaweza KUFUFUKA...
 
Vita vya panzi furaha ya kunguru, sisi tuendelee kununua popcorns, hili sinema haliishi leo.
I see,

Hii mechi bado chaaanga!

Kuna mambo nimehisi yatatokea soon... RA akiamua kujibu hapo patakuwa patamu.

Ila jamaa kaamua kuongea direct bila kuzunguka. Kuwa RA anajaribu kumchafua kwa kutumia magazeti yake na akasema RA ni mchafu na hawezi kujisafisha (RA) kwa maji machafu (nadhani akimaanisha hata vyombo vyake ni vichafu)
 
Kama ni kweli Mwakyembe alijitoa kwenye hiyo kampuni basi waandishi wa habari waliotoa hii habari wangekuwa si wa boss fisadi wangefukuzwa kazi mara moja - kwa sababu wanazidi kumexpose boss wao!

Hata tuliodhani ni watu makini kama akina Zitto naona wamedandia bandwagon - bila kujua wanaenda wapi - wachafu kujiosha kwa kwa maji taka!

Mkuu Invisible many thanks kwa updates!
 
No wonder Rostam anatuchezea. Wasomi mahiri, waandishi magwiji, wafanyabiashara wakubwa na wanasiasa wenye majina wote wakitoka wanalia ROstam, Rostam, Rostam. Inaudhi na pia inakera. Kwangu mimi Rostam ni mbunge tu Igunga, sasa kama kila mtu akitoka anasema Rostam hiki Rostam kile Rostam huku. Jamani wanasiasa na waandishi maarufu huo ni upuuzi na kumjenga mtu bure. Kwa sababu kama Rostam ana nguvu za kuwaumiza wenzie anazitoa wapi-CCM, kama anapesa za kuwaliza na kuwaweka viongozi anazitoa wapi-CCM (ambao ndiyo wanatuibia BoT, PPF, NSSF, nk), kama Rostam ana kiburi anakitoa wapi-CCM (kwa rafiki yake JK). Kwa hiyo kwangu haiingii akilini kila siku kulalamika Rostam, Rostam wakati tunajua mbaya ni CCM. Kingine Mwakyembe kama Rostam anakuchafua ni kwamba CCM ya mafisadi inakuchafua. Kwa hiyo badala ya kulalamikalalamika hama Chama au Anzisheni Chama kingine sisi tutawaunga mkono tu. Hiyo itasaidia kuondoal jinamizi Rostam kwenye ndoto zenu for good. Lakini najua hamna ubavu wa kuhama wala kuanzisha vyama kwa sababu na nyie hamko kwa ajili ya wananchi na pia mnajua mtashughulikiwa kama nyie wenyewe (CCM) mlivyowashughulikia wenzenu waliojaribu kuhama (mfano Njelu Kasaka). Kwa hiyo tumechoka na hizo nyimbo zenu ambazo hazina kibwagizo kama hamtafanya kitendo cha kijasiri sasa.

100 kwa 100 kaka! Ayubu alimng'ang'ania Mungu kwa sababu alimjua kuwa yeye ni alpha na omega sasa sijui hawa jamaa nao ccm kwao ni alpha na omega. Ndiyo maana pengine Mungu haingilii haya mapambano kwa sababu anaona tunacheza tu. Ametuletea demokrasia hatuitumii kazi kulalamika
 
Kama ni kweli Mwakyembe alijitoa kwenye hiyo kampuni basi waandishi wa habari waliotoa hii habari wangekuwa si wa boss fisadi wangefukuzwa kazi mara moja - kwa sababu wanazidi kumexpose boss wao!

Hata tuliodhani ni watu makini kama akina Zitto naona wamedandia bandwagon - bila kujua wanaenda wapi - wachafu kujiosha kwa kwa maji taka!

Mkuu Invisible many thanks kwa updates!
Tupo ukurasa mmoja mkuu.

Naitafuta latest doc ya 2007/08 ili tuone kama yuko sahihi.

Ilikuwa ni vema tuweke ile doc ambayo ilikuwa inatumiwa na vyombo vya habari katika kuongelea issue ya Mwakyembe... Kwakuwa katoa hints za nini kifuatiliwe kwa karibu nadhani ni vema kumtendea haki, kuangalia nyaraka ambazo ni latest
 
Vita vya panzi furaha ya kunguru, sisi tuendelee kununua popcorns, hili sinema haliishi leo.

Kweli MTZ,
Lakini tatizo ni kwamba hii sinema inaharibu macho (maendeleo ya nchi). Somebody need to call a short kwa hizi scheming za kijinga. Kwa wanasiasa kufanya scheming ni jambo la kawaida lakini kwa hawa sasa imezidi mno. Kuna msemo anapenda kuutumia Chinua Achebe-stealing more than the owner can ignore. Siasa inahitaji mtu kucheza uchafu, lakini hawa jamaa wa sasa wameenda mbali mno kiasi kwamba sasa wanakera watanzania ambao wamezoea kuwavumilia wanasiasa wao.
 
Wakuu kifupi Mwakyembe amesema YEYE alishajiondoa kwenye kampuni kama mwana hisa lakini yeye pamoja na wabunge wengi wanaiunga mkono kampuni hii na wanaendelea mpaka sasa kuwa interested nayo kwani ni ya wazalendo na haijawahi kupata mkopo toka benki yoyote japo ni ya wazawa.

Nadhani kwa sasa niwaachie uwanja wakuu... Am around

Mkuu Ivisible,

Kwanza asante sana kwa kutupasha hii press conference ya mheshimiwa.

Kama waandishi wa Tanzania wanajua kwenda chini kufuatilia info, huenda hili jambo likazua mambo mengine kibao.

Kama mheshimiwa ka transfaer hizo shares zake inatakiwa awe amelipa pesa nyingi kweli kwenye hiyo process, kwa mtaji wa karibu bilioni 2, huenda ikawa mamilioni. Bila kufanya hayo malipo, hata ukirudisha hizo form zinakuwa hazina maana na bado unaendelea kuwa mmiliki wa shares hizo.

Labda mnaojua sheria ya kuuza au ku transfer shares ikoje naomba tuelemisheni zaidi.
 
Back
Top Bottom