Mkutano wa Mkuu wa wilaya wakosa watu kijiji cha Ikola.

Kengedume

Senior Member
Jan 19, 2012
115
19
Mkuu wa wilaya ya Mpanda alikuwa na mkutano hapa kijiji cha Ikola, wananchi wamesusia mkutano na badala yake kaendesha mkutano wa wakereketwa wa ccm na mtendaji wa kata!

Cha ajabu zaidi nilichokisikia baada ya mkuu wa wilaya kuhoji kwanini watu hawajajitokeza? wajumbe na wakereketwa hawakuwa na majibu na wameamua watumie jeshi kwa kutumia kambi ya jeshi iliyoko hapa kijijini kuwapiga wanakijiji ati hawajahudhuria mkutano wa mkuu wa wilaya! Jamani wana JF nawaonea huruma watanzania na wakazi wa kijij hiki.
 
Liwalo na liwe alisema eti hao ni makada wa magamba sasa hivi wananchi wote ni chadema unategemea nani ataenda kuwasikiliza magamba ya mavi?
 
Kama jeshi la wananchi wa Tanzania wakijiingiza kwenye ujinga huo sasa hivi wataingia kwenye vyombo vya dola vya serikali vinavyodharaulika watapuuzwa kama Polisi na TISS wanavyopuuzwa.
 
Mporomoko wa mvuto wa watu wa ccm na serikali yake kwa sasa ni wa kutisha.
Sasa kwa kuwapiga wananchi wanategemea kuwa wananchi wale wamejifunza nn? ...kama kuzidisha chuki?
 
Chanzo ni mimi mwenyewe nilikuwepo eneo la tukio na mkuu wa wilaya kashaondoka! kafura vibaya!!!!
 
Hendeboy. hii habari nimeitoa hapahapa eneo la tukio nilikuwepo mimi mwenyewe!
Kilosa mkutano kama huu ulisambaratishwa na mkutano wa chadema baada ya tarehe kugongana na mkuu wa wilaya alisalimu amri. sasa huku Jeshi limepangwa kukusanya watu kwa marungu kuhudhuria mkutano wa mkuu wa wilaya!
 
Habari kama hii ni muhimu kuweka source mkuu, ili kulinda heshima ya JF.
 
Hiyo imeishatokea pia huko Bunda. Mkuu wa wilaya alikuwa anazungukia vijiji vya wilaya hiyo kwa ajili ya kujitambulisha. Katika baadhi ya vijiji mahudhurio yahayakuridhisha hivyo mkuu wa Wilaya akaamuru viongozi wa vijiji husika watiwe (waswekwe) ndani.
 
Hiyo imeishatokea pia huko Bunda. Mkuu wa wilaya alikuwa anazungukia vijiji vya wilaya hiyo kwa ajili ya kujitambulisha. Katika baadhi ya vijiji mahudhurio yahayakuridhisha hivyo mkuu wa Wilaya akaamuru viongozi wa vijiji husika watiwe (waswekwe) ndani.

Pia nimepata taarifa toka jamaa yangu Igunga hata mkuu wa wilaya kimemtoke mara mbili ameitisha kikao na akakosa watu wa kuwahutubia:yawn:
 
kwan lazima wanakijiji kuhudhuria mikutona?wananchi wanatafakari namna watakavyoingiza cdm madarakan 2015.hvyo kwa sasa hawataki bughuza
 
Back
Top Bottom