KIKAO NDO KINA ANZA Dr. Namala ameonge na anasisitiza kikao kiwe brief na detail, Dr. ulimboka kaongea amekwisha toa muhtasari wa mkutano wa tarehe 9/2/2012.
Dr. Namala anasisitiza sababu zilizosababisha kuhitilafiana/kutokukubaliana na meza ya majdiliano ya serikali. Madaktari wanatoa michango yao.
Kikinuka nitawajulisha
Kwa ufupi madaktari wamekubaliana kuipa serikali mpaka jumatano saa mbili usiku Bwana Mponda na Naibu wake Lucy wawe wameondoka pale wizara ya afya ili waweze kukaa meza mmoja na serikali kutatua mgogoro wao.
Serikali ikishindwa kufanya hivyo basi mgomo utanza jumatano,madaktari wametumia busara kubwa sana katika mkutano wao wa leo,lakini inaonekana ofisi ya waziri mkuu na chombo kimoja cha habari vinatumika vibaya kuupotosha umma wa Tanzania.
My take: serikali ifanye jitihada ya kuwaondoa hawa waliotuhumiwa ili wananchi wasije pata madhara tena kama mgomo ulio pita
Mungu ibariki Tanzania na watu wake
Mkuu ni kweli kwamba JK amechelewa sana kuwatimua lakini ni uungwana kwa mwanasiasa kupima na kujiuzulu pale mambo yanapoharibika chini yako. Na mbaya zaidi jambo lenyewe linapohusu sekta muhimu ktk taifa kama Afya. Kuna watu wengine ambao wanapaswa kuachia ngazi ni Mwandosya na Dr. Mwakyembe kwa misingi ya kiafya. Wawaachie hizi nafasi wenye nguvu ya mwili na afya njema wafanye kazi za wananchi muhimu serikali iendelee kuwahudumia mpaka wakipona.swali lingekua hivi JK anasubiri nini kuwaondoa??
Nahisi kama kuna sinema inataka kuanza hapa.
hebu ngoja nikae vizuri...
Namsikitikia sana JK kwani huyu jamaa hayuko serious na kitu chochote. Hata madr waliposema wafukuzwe hao jamaa bado alikuwa anadhani ni utani na kuja kuendelea kudanganya wanachi kuwa anajali hali ya nchi kumbe alikimbilia ughaibuni. Shauei yenu huenda jamaa limeshapata uraia wa nchi za nje ili akimbie mambo yakiharibika. JK si mtu!Hadi leo mshahara bado..! Poleni
Ni jumatano saa mbili asubuhi ndg..
Ila taarifa kamili itatolewa kwenye vyombo vya Habari na uongozi wa madaktari ..
Hoja tu mkuu.Umesema vyema mkuu madaktari hawataki siasa wala hawapo kwa ajili ya kumtukana kiongozi yeyote wa serikali,sas kuna watu wanaleta matusi ambayo yataharibu maana kuu ya huu mjadala
Mkuu niombee ila sitoi sadaka!
Kimbunga unahitaji maombi ya kufunga na kuomba..una matatizo makubwa sana.
Mkuu wangu ukweli unenwe tu hata kama unauma lakini matusi pia yaepukwe. Mkuu wangu unazikumbuka zile sheria 40 za kikandamizaji ambazo Jaji Nyalali alisema zifutwe? Hivi zilishafutwa au bado zipo na zinaweza tumika wakati wowote? Unazifahamu mkuu wangu?Mkuu kimbunga pole kwa matatizo yanayokusibu...kuongea ukweli ni matusi?