Mkutano wa Jangwani Mei 26: Polisi walumbana na CHADEMA!

Kwa hali ilivyo inabidi tuanzishe movement ya WALK TO WORK kama ya Besigye.Hali ni ngumu.
 
Nafikiri kama raia siku zote wanatembea kutokana na ugumu wa maisha uliosababishwa na ccm wakiwamo polisi basi itakuwa vema iwapo polisi wakatoa nauli siku hiyo ili amri yao iwe sawa,vinginevyo ni kunyanyasa wananchi na hii inaanza kuwa tabia tanzania.Siku zote hakuna anayezuiwa kutembea why now? Kwa nini wasingezuia watu kutembea siku ya muungano,uhuru na sherehe nyingine,wakumbuke tanzania sio yao yetu wote
 
Wasitutanie, hapa kitaani tumeshaandaa uwanja na Spika za kufa mtu, watu watamiminika kwa pamoja uwanjani kuona live ITV ukombozi wa nchi ikisonga mbele zaidi. Tunategemea watu mamia kwa mamia kumiminika hapa wakiitikia pipoz pawaaaaaaaaaaaaaaaa, kukunja ngumi na michango ya ukombozi itaendelea. Kina Magamba lazima mwaka huu wasimamie kucha, Tumewapangisha ikulu mmeifanya pango la walanguzi kina Riz1, tupisheni hata kama kodi haijaisha
 
Tumejiandaa vyema kuhakikisha tunaharibu huo mkutano, sasa kama mnabisha andamaneni muone!
Wanafiki wakubwa nyie.
CCM OYEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


KURUGENZI ya Ulinzi na Usalama ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) inapenda kutoa taarifa kuwa matembezi ya wanachama wake kutoka maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam kuhudhuria mkutano mkubwa wa hadhara utakaofanyika Viwanja vya Jangwani, yako pale pale kama ilivyopangwa na kutolewa taarifa kwa Jeshi la Polisi.

Itakumbukwa kuwa mkutano huo wa hadhara utakaofanyika Mei 26, 2012 umeshakamilisha taratibu zote, ikiwemo kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi, ambalo tayari limesharidhia kushiriki kwa kutoa ulinzi kwa mkutano huo, siku hiyo ya Jumamosi.

Katika barua yetu ya Mei 23, 2012, kwenda kwa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, tulisema kuwa kutokana na hamasa kubwa ambayo imejitokeza kwa wanachama wetu juu ya mkutano huo mkubwa wa hadhara, katika majimbo yote ya jiji na kutokana na hali halisi ya ugumu wa maisha unaowakabili wananchi wengi unaopelekea kutomudu gharama mbalimbali za maisha zikiwemo za usafiri (nauli za mabasi) wamejipanga kufanya matembezi ya amani, ya mshikamano, kuhudhuria mkutano wa Jangwani.

Katika mazungumzo na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam leo, tumeona dhahiri kuwa jeshi letu linajenga hoja dhanifu zaidi na kufanya kazi kwa mtindo wa kupiga ramri badala ya kufanya kazi kisasa kwa kutumia hoja yakinifu zenye mantiki, katika kutimiza jukumu lao kubwa la ulinzi na usalama wa raia na mali zao.

Ni vigumu kwa mtu yeyote makini kuweza kukubaliana na hoja za Jeshi la Polisi kuwa hawataki wananchi watembee kwa amani kutoka maeneo mbalimbali kwenda eneo la mkutano eti tu kwa sababu kunaweza kuibuka vitendo vya ukabaji, uporaji katika matembezi hayo! Huku ni kufanya kazi kwa mtindo wa kupiga ramri!

Kumbukumbu zinaonesha kuwa hakuna maandamano yoyote ya CHADEMA yamewahi kuwa na vurugu au vitendo vyovyote vile vya uvunjifu wa amani isipokuwa tu pale ambapo Jeshi la Polisi liliingilia kati na kusababisha vurugu, likapiga watu, likatesa watu hata kusababisha vifo kwa visingizio na hoja zisizokuwa na msingi kama hizi wanazotoa sasa, huku wakitumia lile maneno yao maarufu 'taarifa za kiintelijensia'.

Pamoja na madai ya jeshi hilo kuwa hakuna askari wa kutosha kulinda matembezi hayo ya amani na mshikamano, kutokana na mantiki hiyo hapo juu, hatutashangaa wakipatikana askari wengi wa kuanzisha vurugu, kupiga watu, kutesa na hata kusababisha vifo, kama ambavyo imetokea katika maeneo mengine kwa kisingizio cha kuzuia maandamano.

Imetokea hivyo Arusha, imetokea hivyo Songea (Ruvuma), imetokea hivyo Ikwiriri, Rufiji, ambako Jeshi la Polisi lenyewe limekiri wazi kabisa kuwa lilikuwa chanzo cha vurugu hata wananchi kupoteza maisha. Imetokea hivyo sehemu mbalimbali ambako polisi hudai hawana askari wa kutosha kuwalinda wananchi na mali zao, lakini wanapatikana askari wengi wakati wa kuvuruga na kupiga watu hata kusababisha vifo.

Tunawaomba ndugu zetu wa Jeshi la Polisi watoe ushirikiano kwa wananchi. Wasifanye kazi kwa ubaguzi wa aina yoyote ile katika makundi mbalimbali ndani ya jamii wala maelekezo ya kisiasa, hasa kutoka kwa chama tawala, CCM kama ambavyo imedhihirika mara kwa mara.

Tunapenda kusisitiza kuwa polisi wasifanye kazi kwa mtindo wa kupiga ramri na kujenga hoja dhanifu. Wanachama na wapenzi wa CHADEMA wamedhihirisha mara kadhaa, pasi na shaka yoyote kuwa wanaweza kufanya matembezi ya mshikamano bila kuathiri haki za watu wengine. Kwa amani na utulivu.

Tutaendelea kuthibitisha hivyo Mei 26, 2012, kuelekea Jangwani na mahali pengine popote ambapo tutatumia haki ya kikatiba kufanya matembezi ya mshikamano au kuandamana katika misingi ya kutoa elimu ya uraia kwa wananchi, kudai haki, mabadiliko ya kweli katika utawala na mfumo, kudai uwajibikaji wa serikali kwa watu au katika kupiga vita ufisadi na uonevu wa watawala dhidi ya wananchi.

Imetolewa leo Mei 24, 2012 Dar es Salaam na;

Wilfred Muganyizi Lwakatare
Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama-CHADEMA
 
Tanzania, yaani imefikia kutembea kwa mguu kwenda upendapo wewe ni kosa. Maajabu ya kuogopa kivuli. Sasa kateni miguu ya watu isifanye kazi. Je mtu akikutwa anatembea kwa mguu kuelekea jangwani atashitakiwa kwa kosa gani? Tanzania! Tanzania! nakupenda kwa moyo wote! na popote niendapo nakuota wewe!

mkuu polisi hawajitambui kwani si unajua hata vyeti vyao vya kuunga unga vile.

Peoples...........\/
 
Kuna tofauti kubwa kati ya mkutano na maandamano.

Kwani mkikutana jangwani tu mkafanya mkutano wenu halafu kila mtu akaondoka zake inakuwa na shida gani?

Kama wanakatazwa kuingia kwa maandamano ili kuzuia watu wengi kutembea kwa pamoja, mkutano ukiisha wataondokaje bila kuonekana wanaandamana ukitilia maanani kuwa waliohudhuria wataondoka wote kwa wakati mmoja?
 
KWENYE MAANDAMANO KUNA 'INTEREJENSIA',KATIKA KULINDA MALI ZA UMMA ZISIPOLWE NA MAFISADI HAKUNA 'INTEREJENSIA',Nchi hii bwana.
 
Tumejiandaa vyema kuhakikisha tunaharibu huo mkutano, sasa kama mnabisha andamaneni muone!
Wanafiki wakubwa nyie.
CCM OYEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Magamba mavi debe! Na bado!
 
KWENYE MAANDAMANO KUNA 'INTEREJENSIA',KATIKA KULINDA MALI ZA UMMA ZISIPOLWE NA MAFISADI HAKUNA 'INTEREJENSIA',Nchi hii bwana.

Hizi intelejensia duuu zingekuwa zinakuwepo wakati wezi wanatuibia mali za uma hakika Mkuu wa kaya angezipata hizo dola billioni moja kwa mwezi anazoziota. Lakini ndo hivyo tena POLICCM kazini.
 
Mkuu wangu makene ,kwa sisi ambao tuko mikoani tutaona mkutano kupitaia kituo gani ?waamsheni hao wanaojiita wabongo sisi huku tulishawapiga bao.

ITV, Itakua LIVE kutoka jangwani jijini DSM... Nimewaambia bibi na babu huko kijijini waangalie ITV siku na muda huo!!
 
"Hivyo wanachama kutoka maeneo ya Ukonga, Ilala, Kawe, Temeke, Ubungo, Kigamboni, Kinondoni watatembea kwa amani na mshikamano kwenda eneo la mkutano."

Ingekuwa vema na busara kama Mbowe angeenda kuanza nao Kawe akatembea kwa miguu na hawa watu kutoka Kawe mpaka Jangawani na Slaa akaanzia Temeke mpaka JAngwani MGUU KWA MGUU, na Prof Safari akianzia Ubungo, najua Zito ataweza kuanza nao Ubungo, wasipofanya hivo NITAWAONA SIO WAZALENDO !

Imetokea hivyo Arusha, imetokea hivyo Songea (Ruvuma), imetokea hivyo Ikwiriri, Rufiji, ambako Jeshi la Polisi lenyewe limekiri wazi kabisa kuwa lilikuwa chanzo cha vurugu hata wananchi kupoteza maisha. Imetokea hivyo sehemu mbalimbali ambako polisi hudai hawana askari wa kutosha kuwalinda wananchi na mali zao, lakini wanapatikana askari wengi wakati wa kuvuruga na kupiga watu hata kusababisha vifo.


Umeisahau Pemba walivokimbia kisiwa chao miaka ya Comandoo!
 
Nimefurahishwa na taarifa za Police kuwa mfanye Mkutano ! hatutaki fujo kwenye MJI WETU ! na msipotii mkikimbizwa msilaumu mtu ! maana mmeshaambiwa kuwa mfanye mkutano! unaambiwa " Dont break the Law , bend it " sikumbuki sijui nani humu JF, sasa mkivunja sharia kitakachowatokea msilaumu mtu !
 
Tutafikaje huko jangwani?

Ndio mtajiju, kama kweli CDm wangekuwa wazalendo wangeprovide usafiri, hata kuwakodia magari watu wenu mnashindwa?! kwanini hamtugezi sisi CCM ? pikipiki zipo ! magari bweleleeeee eeh! kweli CCM ndio chama pekee jamani !
 
Nnaomba niwatie moyo wakazi Wa Dsm kuwa wawe wajasiri kufanya jambo.Polisi ktk maandamano ya tareh 5 Arusha waliyakataa kwa sababu zisizokuwa na kichwa wala miguu kwa mtu mwenye akili timamu(anaefikiri zaidi kuliko mapokeo)wakatupiga mabomu na kuua raia zaidi ya waliotangazwa ktk vyombo vya habari,lakini tulikomaa nao mpaka sasa hivi polisi wakipelekewa taarifa za kuwapo mkutano Wa Chadema matumbo yanawauma.Hata ktk kesi ya Lema mwanzoni wananchi walizuiwa lakini kwa sbb tulikuwa wajasiri(kuingia mahakamni kwa nguvu)walikubaliana na sisi.Polisi ni wajanja wanawatisha watu kwa mabomu ya machozi/maji ya pilipili/risasi mkigwaya tu inakula upande wenu lakini mkikomaa nao wanakuwa wadogo Kama piriton.Siwashawishi mzivunje sheria za nchi,zitekelezeni Ila msiwe waoga muwe wajasiri Wa kuhoji na kutekeleza kwa vitendo.Amani iwatangulie hiyo kesho ktk harakati hizi ambazo siku zote huwa na vikwazo vingi vigumu,,,,,,Peplesssss Powerrrs mpaka huku A-town tuwasikie makamanda mkiwakilisha.
 
Back
Top Bottom