Mkutano wa IMF ndani ya Dar es Salaam

KiuyaJibu

JF-Expert Member
Aug 29, 2007
841
175
Mkutano wa International Monetary Fund(IMF) yaani shirika la fedha duniani unafanyika jiji Dar es salaam,Tanzania kesho tarehe 10.03.2009 ambapo utawashirikisha mawaziri wa fedha na magavana wa benki kuu za Afrika.

Wakati mkutano huo unafanyika,taarifa zilizopatikana zinaonyesha kwamba Policy Support Instruments zilizomo ndani ya IMF ndiyo hizo hizo zilizomo katika mpango/programme ya MKUKUTA ndani ya serikali ya Tanzania na mpango huo ambao uko katika utekelezaji wake;binafsi na baadhi ya watu wameanza kuutilia mashaka baada ya kugundulika sera zimehamishwa kama zilivyo katika makablasha ya IMF. Wakati serikali(TZ) inadai kwamba hiyo ni sera ya nchi!

Mojawapo ya udhaifu huo ni kudai uchumi wa Tanzania umeendelea kukua kwa asilimia saba(7%) tokea mwaka 2000;wakati hali halisi ya maisha ya Watanzania haiendani na ukuaji wa uchumi wenyewe.Takwimu zinaonyesha kwa kipindi chote hicho maskini wameongezeka kutoka million 11-12 hivi sasa.Na shutuma zinaonyesha kwamba yote hiyo ni kutokana na serikali kukubaliana na kupangiwa utekelezaji wa masuala ya kiuchumi na IMF; kwa upande mwingine inawezekana pia viongozi wetu wanaogopa kusema ukweli wa hali halisi na matatizo tuliyonayo katika nchi yetu.Hii inamaanisha kuna upotoshwaji wa taarifa,ukizingatia IMF yenyewe haifanyi kazi ndani ya serikali husika wao ni wageni lakini kama tukisimama katika ukweli kwa pande zote mbili inaonyesha kutakuwa na hali nzuri tofauti na ilivyo sasa.

Au kuifukuza IMF isishiriki katika kutupangia mambo ya kufanya na kuyatekeleza kama ilivyofanya nchi ya Zambia,ambayo sasa imepata ahueni baada ya kulikacha shirika hili la kimataifa.

Hebu semeni wenyewe tunafaidika vipi kama kuna nchi zinalikacha shirika hili halafu sisi bado tunalikumbatia na umaskini unaongezeka ukilinganisha na hizo nchi nyingine!?
 
Last edited by a moderator:
Mkutano wa International Monetary Fund(IFM) yaani shirika la fedha duniani unafanyika jiji Dar es salaam,Tanzania kesho tarehe 10.03.2009 ambapo utawashirikisha mawaziri fedha na magavana wa benki kuu za Afrika.
Wakati mkutano huo unafanyika,taarifa zilizopatika zinaonyesha kwamba Policy Support Instruments zilizomo ndani ya IMF ndiyo hizohizo zilizomo katika mpango/programme ya MKUKUTA ndani ya serikali ya Tanzania na mpango huo ambao uko katika utekelezaji wake;binafsi na baadhi ya watu wameanza kuutilia mashaka baada ya kukundulika umehamishwa kama ulivyo katika makablasha ya IMF.Wakati serikali(TZ) inadai kwamba hiyo ni sera ya nchi!
Mojawapo ya udhaifu huo ni kudai uchumi wa Tanzania umeendelea kukua kwa asilimia saba(7%) tokea mwaka 2000;wakati hali halisi ya maisha ya Watanzania haiendani na ukuaji wa uchumi wenyewe.Takwimu zinaonyesha kwa kipindi chote hicho maskini wameongezeka kutoka million 11-12 hivi sasa.Na shutuma zinaonyesha kwamba yote hiyo ni kutokana na serikali kukubaliana na kupangiwa utekelezaji wa masuala ya kiuchumi na IFM;kwa upande mwingine inawezekana pia viongozi wetu wanaogopa kusema ukweli wa hali halisi na matatizo tuliyonayo katika nchi yetu.Hii inamaanisha kuna upotoshwaji wa taarifa,ukizingatia IMF yenyewe haifanyi kazi ndani ya serikali husika wao ni wageni lakini kama tukisimama katika ukweli kwa pande zote mbili inaonyesha kutakuwa na hali nzuri tofauti na ilivyo sasa.
Au kuifukuza IMF isishiriki katika kutupangia mambo ya kufanya na kuyatekeleza kama ilivyofanya nchi ya Zambia,ambayo sasa imepata ahueni baada ya kulikacha shirika hili la kimataifa.
Hebu semeni wenyewe tunafaidika vipi kama kuna nchi zinalikacha shirika hili halafu sisi bado tunalikumbatia na umaskini unaongezeka ukilinganisha na hizo nchi nyingine!?

Mkuu ni IMF na si IFM
 
Wakuu mlio Dar, tuelezeni kitakachojiri kwenye hiyo conference. Waziri wetu si atakuwepo, ataleta taarifa gani?
 
Hii IMF ni mufilisi ndo wanaotumamaskinisha na hawana nia ya kweli ya maendeleo ya nchi za dunia ya tatu,so solution ni kuachana nao kabisa.Hawana tija kwetu.Daima nasisitiza maendeleo ya kweli yataletwa na sisi watz kwa kila mmoja kuwajibika kwa nafasi aliyoko,na si sera za IMF,BW,wa nchi za nje,tuanze kujiamini sasa na kuwa na sera zetu zinazotokana na utamaduni wetu,vipaumbele vyetu,na asili yetu na si vinginevyo.INAWEZEKANA TIMIZA WAJIBU WAKO
 
KiuyaJibu!
International Monetary Fund (IMF)

Institute of Finance Management (IFM)
 
Kama mambo ni hayo yabidi tuwe makini zisije tolewa taarifa za uongo kuhusu kukua kwa uchumi wa nchi yetu pendwa Tanzania
 
Mkutano wa International Monetary Fund(IMF) yaani shirika la fedha duniani unafanyika jiji Dar es salaam,Tanzania kesho tarehe 10.03.2009 ambapo utawashirikisha mawaziri wa fedha na magavana wa benki kuu za Afrika.

Wakati mkutano huo unafanyika,taarifa zilizopatikana zinaonyesha kwamba Policy Support Instruments zilizomo ndani ya IMF ndiyo hizo hizo zilizomo katika mpango/programme ya MKUKUTA ndani ya serikali ya Tanzania na mpango huo ambao uko katika utekelezaji wake;binafsi na baadhi ya watu wameanza kuutilia mashaka baada ya kugundulika sera zimehamishwa kama zilivyo katika makablasha ya IMF.Wakati serikali(TZ) inadai kwamba hiyo ni sera ya nchi!

Makala hii inaelezea mantiki ya hizo Policy Support Instruments (PSI): UDADISI: Rethinking in Action: Because the IMF says so?
 
Heshima kwa wana JF wote
Jamani ukuaji wa uchumi mimi naupimia mfukoni kwangu pia. Pamoja na nyimbo zote kwanza global kraisisi naona ina madhala moja kwa moja kwangu halafu nashangaa wakubwa wanabishana na hilo, huo ukuaji wa uchumi siufeel kabisa naona kila kukicha mambo yanazidi kuwa magumu. Anyway acha nisubiri single mpya kutoka conference hii.
 
Kama mambo ni hayo yabidi tuwe makini zisije tolewa taarifa za uongo kuhusu kukua kwa uchumi wa nchi yetu pendwa Tanzania

Mkuu achana na taarifa zinazotolewa na Bretton Wood institutions, angalia hali toka Ben Mkapa alipochukua nchi kutoka kwa Mzee Mwiny na hali iliyopo sasa utaona tofauti kubwa. Nchi yetu sasa hivi inapesa sana, sio serikali maskini tena kama ilivyokuwa kama alivyoichukua mzee Mwinyi kutoka kwa JKN au kama alivyoichukua Ben Mkapa kutoka kwa Mzee Mwinyi, labda tatizo kidogo uchumi umedorora kwenye utawala wa JK, lakini still bado tuko kwenye hali nzuri.
Tatizo kubwa ni kwamba tumeshindwa kuzitumia vizuri fedha na kuzifikisha mifukoni au kwenye meza za watanzania wanaofanya kazi kufanya tuwe na hizo fedha. Mafisadi wanatuvuruga sana na wanatukwamisha sana. IMF ni wezi tu hawana jipya, watakuja na sera zao za kuwanufaisha wao, sisi wenyewe tunatakiwa kuwa na akili ya ku-deal nao. Kama sasa hivi ukiangalia hata waziri wa fedha hatuna(aliyepo ni ineffective), kwa hiyo utaona kuwa IMF wana easy ride na Tanzania.
 
Tatizo haliko IMF wala world Bank, wao kwa kawaida hushauri serikali na jukumu la serikali husika kukubali ushauri wao au kama wanauona haufai kukataa. Mwalimu Nyerere aliwahi kutofautuana na hizi multilateral institutions; lakini hivi sasa tatizo liko kwa viongozi wetu wa nchi kwa vile ni "VILAZA" wanakubali kila kitu wanachoambiwa na wageni na hawathamini ushauri wa nyumbani!! Tulifika mahali mpaka nchi yetu ilikuwa inamhusudu mtu YEBO YEBO kama George Walker Bush; haya yalikuwa matusi makubwa kwa watanzania tuliokuwa na heshima yetu huko nyuma na hili la kuwaua maalbino ndio limemaliza kabisa heshima yetu duniani!!
 
Umenfurahisha comment yako juu ya waziri wetu wapesa ''Kama sasa hivi ukiangalia hata waziri wa fedha hatuna(aliyepo ni ineffective)'' Ha ha haaaaaaaaaaaaaaa, mkuu JK sialiwaambia uwaziri hausomewi? hivyo mchezo wa ana ana anado unatosha kuchagua mawaziri
 
Hii IMF ni mufilisi ndo wanaotumamaskinisha na hawana nia ya kweli ya maendeleo ya nchi za dunia ya tatu,so solution ni kuachana nao kabisa.Hawana tija kwetu.Daima nasisitiza maendeleo ya kweli yataletwa na sisi watz kwa kila mmoja kuwajibika kwa nafasi aliyoko,na si sera za IMF,BW,wa nchi za nje,tuanze kujiamini sasa na kuwa na sera zetu zinazotokana na utamaduni wetu,vipaumbele vyetu,na asili yetu na si vinginevyo.INAWEZEKANA TIMIZA WAJIBU WAKO

Mkuu acha munkari, nikweli katika dunia tunasema ''there is no free lunch'' lakini mchango wa IMF unahitajika sana si katika nchi masikini bali hata katika nchi zilizoendelea. Hivyo kusema tuachane nao kabisa hiyo siosahihi mkuu wangu.
 
Tatizo haliko IMF wala world Bank, wao kwa kawaida hushauri serikali na jukumu la serikali husika kukubali ushauri wao au kama wanauona haufai kukataa. Mwalimu Nyerere aliwahi kutofautuana na hizi multilateral institutions; lakini hivi sasa tatizo liko kwa viongozi wetu wa nchi kwa vile ni "VILAZA" wanakubali kila kitu wanachoambiwa na wageni na hawathamini ushauri wa nyumbani!! Tulifika mahali mpaka nchi yetu ilikuwa inamhusudu mtu YEBO YEBO kama George Walker Bush; haya yalikuwa matusi makubwa kwa watanzania tuliokuwa na heshima yetu huko nyuma na hili la kuwaua maalbino ndio limemaliza kabisa heshima yetu duniani!!

Mkubwa mbona unatuchanganya, mara tulikuwa tunamhusudu YEBO YEBO Bush, mara mauwaji ya albino, mara heshima yetu duniani imepungua. Sijakupata unachotaka kuzungumza hapa kuu samahani lakini kwa hilo
 
KiuyaJibu!
International Monetary Fund (IMF)

Institute of Finance Management (IFM)
Samahani sana Wana-JF wote ni nilikosea(typing error)ukweli ni IMF=International Monetary Fund.
Hence,save the correction as provided herein.
 
Tatizo haliko IMF wala world Bank, wao kwa kawaida hushauri serikali na jukumu la serikali husika kukubali ushauri wao au kama wanauona haufai kukataa. Mwalimu Nyerere aliwahi kutofautuana na hizi multilateral institutions; lakini hivi sasa tatizo liko kwa viongozi wetu wa nchi kwa vile ni "VILAZA" wanakubali kila kitu wanachoambiwa na wageni na hawathamini ushauri wa nyumbani!! Tulifika mahali mpaka nchi yetu ilikuwa inamhusudu mtu YEBO YEBO kama George Walker Bush; haya yalikuwa matusi makubwa kwa watanzania tuliokuwa na heshima yetu huko nyuma na hili la kuwaua maalbino ndio limemaliza kabisa heshima yetu duniani!!

Bado tuna safari ndefu sana ya kupambana na huu umasikini, viongozi wetu wengi ni MAFISADI.
 
Guys , tulifutiwa madeni and guess what, our people todate didnt even get any relief on reducing poverty but we only ended up getting these "Generation & Isidingo dramas" of EPAS and etc....!!!
IMF will not help us unless we kick our corruption scandals and b serious on changing our country into real actions of positive development for everyone to play his/her part get rid of bad apples!!
 
Thats write, we dont have to count on "msamaha wa madeni tu" Na misaaada tunayopata inaishia wapi jamani? Hivi hela aliyotupatai bush hizo barabara watajenga lini? Maana kila cku tunashuhudia sahii tuu,hamna changes,jamani ufisadi ni mbya.Mimi binafsi naumia saana na umaskini wa nchi yetu. Tembalea nchi watu,utalia machozi,barabara ilijengwa ina miaka zadi ya 60 na ipo mpaka leo na ipo imara,sisi ukikaribia uchaguzi wanamwaga changarawe ili wagombea wasipate shida, lkn c wananchi waishio maeneo hayo. Uchaguzi ukiisha wananchi wanaugua magojwa mbalimbali kutokana na vumbi la barabara.Viongozi wa Tz usanii mtaacha lini?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom