Elections 2010 Mkutano Wa Hadhara Wa Wana-JF [Online]

naona nikuite mwenyekiti, ni sawa kabisa, nina uchungu sana na hawa mafisadi,la sivyo nitajichukulia hatua mkononi ya kuwachoma bisibisi za kichwani kama hawataadhibiwa

Asante sana Kijana wangu Jungu Mawe, kwa sasa usiniite Mwenyekiti maana uchaguzi bado haujafanyika na mimi sitaki kuibaka Demokrasia. So kwa sasa bado ni mratibu tu.

Hata hivyo tunajivunia kuwa na vijana kama nyie wenye mawazo chanya. Ni matumaini yangu kuwa Chama chako kama kitashinda kitakupa nafasi ya kuitumikia Nchi yetu.

Well done and Keep it Up!
 
Nimenyoosha mkono sasa unauma, naomba niongee.

Samaani kijana wangu nilikuwa nimetoka kidogo . . . Sasa nakupa nafasi na wewe uongee . . .

Halafu umechelewa sana kwenye mkutano. Kulikoni?
 
Mie yakhe napendekeza katika uundaji wa katiba mpya kuwe na kifungu cha sheria kinachomlazimisha yeyote ataekabithiwa madaraka ya usimamizi wa rasilimali za nchi, kula kiapo cha ikiwa atahujumu uchumi wa nchi na ikathibitika kisheria, basi akubali kwamba atanyongwa hadharani. Hii itapunguza msongamano wa watu wanaotafuta madaraka kwa gharama isiyomithilika. Kuna mifano iliyo hai wapo wanaoitafuta ofisi kwa kuteketeza bil 50. M/KITI NASISITIZA TENA LAZIMA WATU HAWA WALE KIAPO HIKI CHA KUNYONGWA HADHARANI IKIWA........

Asante sana Kijana wetu Kiby,

Hakika unaonyesha una uchungu sana na Nchi hii ya Maziwa na Asali . . . .

Kwa hiyo unachosema ni kuwa "Kiongozi Wa Kuchaguliwa Atakayepatikana Anahujumu au Kuifisadisha Mali ya Taifa, Anyongwe Hadharani Mpaka Afe"?

Sasa hapa pana mgogoro kidogo? hatutakuwa tumevunja haki za binadamu? Wanaharakati mnasemaje kwa hili?

Kuna mfano wowote wa Nchi wanaofanya hivi?
 
M/kiti, pointi ovu interapusheni! nilipitwa..
1. Tunahitaji viongozi waadilifu (credible) na wawajibikaji (accountable) wawe mfano kwa taifa la leo na vizazi vijavyo.
2. Tunahitaji kuandika katiba mpya kabisaa!

Asante sana Mfuatiliaji . . . nimekuona muda mrefu ulikuwa unatuma SMS unachat na nanihii ndo maana ulipitiwa . . . tuyaache hayo.

Hili la katiba tayari wengi wameafiki. Sasa hili la Uadilifu na Uwajibikaje tuliweke hivi.

Kwamba "JF inawataka Viongozi Wote Watakaoingia Madarakani Wafanye Kazi kwa Uadilifu na Uwajibikaji na Weledi Wa Hali ya Juu"

Katika hili, Tume ya Maadili iundwe upya iwe ya "Maadili, Uwajibikaji Na Weledi"
 
Asante sana Kijana wetu Kiby,

Hakika unaonyesha una uchungu sana na Nchi hii ya Maziwa na Asali . . . .

Kwa hiyo unachosema ni kuwa "Kiongozi Wa Kuchaguliwa Atakayepatikana Anahujumu au Kuifisadisha Mali ya Taifa, Anyongwe Hadharani Mpaka Afe"?

Sasa hapa pana mgogoro kidogo? hatutakuwa tumevunja haki za binadamu? Wanaharakati mnasemaje kwa hili?

Kuna mfano wowote wa Nchi wanaofanya hivi?

Mwenyekiti, napendekeza iundwe " task force" itembelee nchi kadhaa kujifunza uzoefu wa namna sheria kama hii inavyofanya kazi...tukianza na China.....( mhhh...sijui itatumia mabilioni mangapi!)
 
Jamni zamu yangu bado tuuu:confused2::confused2:

He, Maria Roza kumbe umeshakuja? Rev. Masa alikuwa anawatafuta sana wewe na wenzako, kampata WoS tu.

Sasa zamu yako unaweza kuongea, lakini lugha ya matusi hairuhusiwi please.
 
Naungana na wadau hapo juu Mwenyekiti, tunahitaji Katiba na Kiongozi atakayerudisha nchi na watu wake kwenye mstari! Mambo mengine yatajipa tu!

Nyanzura nimekusoma, nadhani hili la muhimu na litazingatiwa. Litaingia katika majumuisho tuliyokubaliana.
 
Tunahitaji mtu atakayefuata rule of law, utawala bora, atakayeimarisha Muungano kwa kuirudisha Tanganyika na cha msingi zaidi tuwe na katiba mpya.

Kamanda nimekusoma kuwa moja kati ya Agenda Kuu 2010 ni "Tunataka kiongozi atakayezingatia Utawala Bora", "Atakayeimarisha Muungano" na "Katiba Mpya".

Hili la Muungano, tutaliweka vipi? Maana sera za vyama vyenu lina mawazo yanayokingana. Au tuitishe kura ya maoni?
 
Kuna mahali nilisoma Slaa akipata ridhaaa ataweka katiba mpya ndani ya miaka michache ya uongozi wake! Jamani hebu nipeni info zaidi .....jirani zetu imewachukua zaidi ya miaka ishirinini (Kenya) hadi walipoiwekea sahihi juzi....

Haya WanaJF kuna hoja imetolewa na Rev. Masanilo, sasa kwa kuwa hatuongelewi vyama bali vipaumbele vya Taifa hasa suala zima la Uzalendo na Maslahi ya Taifa na kwa kuwa suala la katiba nimeafikiwa na wengi; Je, Chama kitakachoingia Madarakani kitumie muda gani kushughulia Katiba Mpya?
 
Jamaa kapotea na bahasha zetu za khaki!!!!!tunataka mgawo wetu haiwezekani.

Quinine nitake radhi; umeanza lugha ya matusi, kejeli na ambayo siyo ya Kistaarabu, rudi kwenye mstari tafadhali . . .

halafu umeshanipoteza . . . Aisee sijui nilifikia wapi vile . . .
 
Mwenyekiti, napendekeza iundwe " task force" itembelee nchi kadhaa kujifunza uzoefu wa namna sheria kama hii inavyofanya kazi...tukianza na China.....( mhhh...sijui itatumia mabilioni mangapi!)

WoS asante sana . . . Wana JF naomba tushauriane . . . tunahitaji kweli Task Force ili kujua agenda kuu 2010 ambazo tunataka zifanyiwe kazi?

Mimi naomba kwa kuwa hizi ni zama za utandawazi, basi pitieni katika wavuti na tovuti mbalimbali ili kupata facts. Hii itasaidia kuokoa mamilioni mabyo yangesaidia maendeleo ya nchi yetu kama kujenga shule na dispensary nk.

Sijui Wos na wengine mnalionaje hili? Kama tuko pamoja basi tupate data ya mifano ya huko China ni nini kinaendelea kabla hatujakubaliana.
 
You people can think. Thanx!

Kiongozi Genakai, nilikutafuta sana tulipoanza sikukuona? Vipi mbona umechelewa kwenye mkutano? majukwaa yote sikukuona ama ulikuwa "kwenye lile lingine"

Kwa heshima na taadhima naomba sasa nikukaribishe utoe maoni yako.
 
M/kiti..hoja yangu ya kupata uzoefu nchi nyingine umeipuuza?

Hapana WoS siwezi kuipuuza . . . hukuyasoma maoni yangu? Kama kuna umuhimu bado wa kuunda task force, basi tupendekeze njia za kupata fedha kwa ajili ya kufanikisha hiyo safari na ni watu gani waende (Uwioano wa jinsia tafadhali).
 
Kiongozi Genakai, nilikutafuta sana tulipoanza sikukuona? Vipi mbona umechelewa kwenye mkutano? majukwaa yote sikukuona ama ulikuwa "kwenye lile lingine"

Kwa heshima na taadhima naomba sasa nikukaribishe utoe maoni yako.

Si unajua mambo ya chuo, nilikuwa busy kudogo na my theses supervisor ananielekeza. But hakijaharibika kitu. Kimsingi nadhani hao jamaa watakao ingia basi wawe na uchungu na nchi kwelikweli na hii hali ya ubinafsi jamani tuiache ili yuwe na mtazamo wa maendeleo ya nchi kwa ujumla!
 
WoS asante sana . . . Wana JF naomba tushauriane . . . tunahitaji kweli Task Force ili kujua agenda kuu 2010 ambazo tunataka zifanyiwe kazi?

Mimi naomba kwa kuwa hizi ni zama za utandawazi, basi pitieni katika wavuti na tovuti mbalimbali ili kupata facts. Hii itasaidia kuokoa mamilioni mabyo yangesaidia maendeleo ya nchi yetu kama kujenga shule na dispensary nk.

Sijui Wos na wengine mnalionaje hili? Kama tuko pamoja basi tupate data ya mifano ya huko China ni nini kinaendelea kabla hatujakubaliana.

Kwa kweli mwenyekiti... baada ya kufikiria zaidi naona kama itaundwa task force /kikosi-kazi basi kisitumie kodi za wananchi.Fedha zichangishwa kwa harambee, watu wajitolee. Pia siku hizi kuna teknolojia ya mawasiliano - itumike kupata taarifa.Mikutano ifanywe kupitia tele/video conference kupunguza gharama.Tafiti za kwenye internet zifanyike kukusanya data.Pia wananchi wenye mapenzi mema walioko China na nchi za karibu wanaweza kupewa usihirikiano na ubalozi wetu na kwa pamoja wakakamilisha kile ambacho kingefanywa na Task force na kutuletea taarifa.Mwisho kabisa nadhani maofisa wetu wa ubalozi wanaweza kutufanyia kazi hiyo maana ndio wanatuwakilisha huko.
 
Si unajua mambo ya chuo, nilikuwa busy kudogo na my theses supervisor ananielekeza. But hakijaharibika kitu. Kimsingi nadhani hao jamaa watakao ingia basi wawe na uchungu na nchi kwelikweli na hii hali ya ubinafsi jamani tuiache ili yuwe na mtazamo wa maendeleo ya nchi kwa ujumla!

Haaa haaa asante sana Kiongozi . . .

Unanikumbusha Enzi za Nyerere na Sokione na maisha ya kujikana waliyoishi . . . sijaona kiongozi wa kada hiyo mpaka leo . . .

Ooops! No yuko Professor Mmari . . . Kiongozi ambaye amepata kila aina ya opportunity lakini kafanya kazi kwa uadilifu Mkuu.

So far ni kiongozi pekee ambaye akienda nje anaretire Imprest in cash.

nadhani hoja yako ina mantiki sana na tutaiingiza kwenye Uadilifu, Uwajibikaji na Utawala Bora
 
Back
Top Bottom