Elections 2010 Mkutano Wa Hadhara Wa Wana-JF [Online]

INAELEKEA MADA KUU YA MKUTANO HUU NI UCHAGUZI 2010.

HIVYO NASHAURI KAMA KUNA WASHIRIKI WANA NAKALA ZA ILANI KUTOKA VYAMA MBALIMBALI KUHUSU MIKAKATI YAO IKIWA WATAPITA (NGAZI ZOTE KUANZIA DIWANI HADI RAIS) KWA MIAKA IJAYO, ITAFAA WAZIBANDIKE (attach) HAPA, TUZISHUSHE (download), TUZIPITIE KISHA TUTOE MICHANGO YENYE MASLAHI YA TAIFA NA SI KUTAFUTA CHAMA KIPI KIMEPUNGUKIWA WAPI.

BINAFSI NIMELAZIMIKA KUFIKA HATUA AMBAPO NITAISHIA KUCHAGUA DIWANI WA CHAMA FULANI, MBUNGE CHAMA KINGINE, NA RAIS PENGINE HATA CHA TATU!

HII NI KWA SABABU MASLAHI YA NCHI INAELEKEA HAYAPO NDANI YA VYAMA BALI NDANI YA WAADILIFU WACHACHE KATIKA VYAMA MBALIMBALI LAKINI HAWANA SAUTI KUBWA KICHAMA/KITAIFA.

NAOMBA KUCHANGIA. WASALAAM
 
Mkuu, hizo ni idara tisa tu ambazo kwa kiasi kikubwa zinasimamiwa na nidhamu za kijeshi zaidi ya utawala wa kisiasa. Naamini kabisa kuwa, zinaweza kuwa chini ya wizara moja na zikawa na ufanisi mkubwa kuliko ilivyo sasa.

JKT iko chini ya JWTZ. Japokuwa kuna mkuu wa JKT, lakini vile vile ni afisa wa jeshi la wananchi. Hilo hakina issue. Na hasa sasa ambapo JKT ni kama imezimika.

Sioni tofauti kati ta Uhamiaji na wakimbizi. Sina uhakika kama katika muundo wa serikali kuna Idara inayojitegemea inayoitwa "Wakimbizi". Ila kama ip, inabidi iwe chini ya Uhamiaji.

Usalama wa Taifa haipo chini ya Wizara ya mambo ya ndani wala Ulinzi. Iko chini ya Wizara ya Utawala Bora (ambayo pia nadhani ingeweza kuitwa Wizara ya Utumishi na Utawala Bora).

Kwa kuongezea tu, si vyema PCCB kuwa chini ya Waziri/Wizara yoyote. Inatakiwa iwe either chini ya Rais au Chombo kikubwa kama Bunge. Hiyo ingeongeza uwezo wao wa kutekeleza majukumu yao na kuwafanya wawe na kinga kubwa zaidi ya ilivyo sasa.

Uongozi wa serikali jeshini ni tofauti na katika nyanja nyingine ambazo zinagusa jamii moja kwa moja. Kama afya, kilimo, elimu n.k. Ambazo kuziunganisha na idara nyingine zinaweza kudhurika beyond repair.

Sijui kama nimejielezea vya kutosha katika hili la kuunganisha wizara hizi mbili?

Recta; asante sana Kiongozi.

Umeliweka vizuri sana na bila ya shaka katika majumuisho litakuwa very unique kwa kuwa hakuna hoja kama hiii iliyotolewa.
 
Wankuu zangu,
Mengi yamezungumzwa na yote ni muhimu sana kwa mapana yake. yaani vichwa vipo JF isipokuwa moja tu naloomba mliwekee maanani kwa sababu haya myatakayo ndiyo yanaunda DIRA ya TAIFA (TANZANIA DEVELOPMENT VISION). Sasa sielewi kama mwenyekiti na wasaidizi wako mumeweza kuyapanga yoote kwa kadri jinsi wanabodi wanavyochangia ili kupata kitu kimoja saafi.
Sina zaidi isipokuwa kutoa shukran zangu kwa wachangiaji ambao hakika wamegusia kila sehemu ipaswavyo. Tahadhali ni moja tu kwamba hatuwezi kwenda mbele pasipo kurekebisha kile kilichotukwamisha...Na nyote mnakijua vizuri..

Mkandala asante sana kwa mwongozo wako . . .

Ingawa huu mjadala unaendeshwa kiutani lakini kuna mambo mengi sana ya kimsingi ambayo binafsi nayaona yana manufaa sana.

Ngoja mara baada ya kikao kumalizika leo saa 6 usiku, tuanze kuandaa majumuisho kisha tukubaliane ni yapi ya kuazimia.
 
Wana-JF, Wakuu Wote; Viongozi Wote; Vijana Wetu (hasa wale wa jukwaa la mapenzi na mambo ya nanihii . . .)

Itifaki imezingatiwa!

Amandla!
Asalaam Aleykhum!
Bwana Yesu Asifiwe!
Haki Sawa . . .
Kidumu Chama . . .
Power to the . . .

Leo tumekutana hapa, ili kuzungumzia "Agenda Kuu 2010" ambazo wana-JF watapenda chama kitakachoingia madarakani wazisimamie . . . . Agenda zetu zimeegemea zaidi katika kuweka mbele uzalendo wetu na maslahi ya taifa . . .

Lugha ya matusi (LOL), hairuhusiwi, wala kejeli wala kutumia lugha isiyo ya kistaarabu. Mnatakiwa muwe na uvumilivu wa kisiasa.

Pia tusiegemee katika Udini wala Ukabila . . .

Baada ya Mjadala Mzito; Tutakuja na Vipaumbele vyetu vitatu kama "Agenda Kuu 2010".

Kwa maneno hayo machache sasa niwakaribishe ili muweze ku-propose "Agenda Kuu 2010" ambazo hazitafungamana na chama chochote!

Kila mmoja wenu anakaribishwa kushiriki Mkutano Wa Hadhara wa JF:
https://www.jamiiforums.com/uchaguz...-hadhara-wa-wana-jf-[online].html#post1058999

karibuni sana!

So far mpaka sasa CHADEMA inashikilia rekodi kwenye hilo jekundu wanachama wanaonyooshea kidole kuwa cuf ni waislam wao kwa kusema hivyo ni wadini
 
kumbe ni porojo tu za kusogeza muda mbele ndicho kinachoendelea hapa....:becky:

Heee, kwanza NN ulikuwa wapi? Siku 2 umetafutwa kwenye mkutano uje hukupatikana halafu unakuja unaanza kutukana matusi makubwa hivyo wakati unajua tuko live TBC, nani amekupa MIC bila ruhusa ya Wenyeviti? Kova ondoka naye huyu, akirudi ndiyo tusikilize hoja zake kama anazo.
 
mmmh mie yangu macho

Gloria, uchaguzi ni wako, ama kuangalia ama kuwa sehemu ya mabadiliko kwa kuchangia yale unayoona ni ya msingi . . . Ukiwa na hoja yoyote nijulishe nikupe Mic.
 
INAELEKEA MADA KUU YA MKUTANO HUU NI UCHAGUZI 2010.

HIVYO NASHAURI KAMA KUNA WASHIRIKI WANA NAKALA ZA ILANI KUTOKA VYAMA MBALIMBALI KUHUSU MIKAKATI YAO IKIWA WATAPITA (NGAZI ZOTE KUANZIA DIWANI HADI RAIS) KWA MIAKA IJAYO, ITAFAA WAZIBANDIKE (attach) HAPA, TUZISHUSHE (download), TUZIPITIE KISHA TUTOE MICHANGO YENYE MASLAHI YA TAIFA NA SI KUTAFUTA CHAMA KIPI KIMEPUNGUKIWA WAPI.

BINAFSI NIMELAZIMIKA KUFIKA HATUA AMBAPO NITAISHIA KUCHAGUA DIWANI WA CHAMA FULANI, MBUNGE CHAMA KINGINE, NA RAIS PENGINE HATA CHA TATU!

HII NI KWA SABABU MASLAHI YA NCHI INAELEKEA HAYAPO NDANI YA VYAMA BALI NDANI YA WAADILIFU WACHACHE KATIKA VYAMA MBALIMBALI LAKINI HAWANA SAUTI KUBWA KICHAMA/KITAIFA.

NAOMBA KUCHANGIA. WASALAAM

Juanita, tumekusoma. Kwa ujumla unazungumzia Uadilifu, Uwajibikaji na Weledi. Hili litaingizwa katika utawala bora.

Kuhusu Ilani ya vyama, hapa tumeona ni bora tuongelee vipaumbele vya taifa ambavyo tukukubaliana zitakuwa Agenda Kuu 2010 ambazo chama kitakachoingia madarakani kitapewa kama mchango wetu ili yafanyiwe kazi.
 
So far mpaka sasa CHADEMA inashikilia rekodi kwenye hilo jekundu wanachama wanaonyooshea kidole kuwa cuf ni waislam wao kwa kusema hivyo ni wadini

Sokomoko, umetoka nje ya maada, hapa tunazungumzia vipaumbele vya taifa na uzalendo. Ni nini cha kufanya ili tufanikiwe.

Kama utapenda unaweza kujenga hoja yako kuwa Serikali itakayoingia madarakani "Isimamie kwa vitendo kuondoa aina yoyote ya Ubaguzi na makundi kama udini, ukabila, rangi, jinsia nk na kuleta mshikamano kama taifa na jamii moja"

Hiyo imekaaje?
 
Wana JF, naona muda umekwenda sana na sasa tunakaribia kufunga mkutano wetu . . .

Kabla ya kufanya hivyo, yeyote mwenye hoja ya ziada aje hapa jukwaani kwenye kipaza sauti.
 
Mkuu mwenyekiti
nashauri kwamba katika jopo lako la wataalam wa kuchambua na kujumuisha hoja zetu wasiwe watu bias na waweke uzalendo mbele. ila pia kama ikibidi wafanye kazi ndani ya siku chache kama tano hivi watuletee dummy kabla ya kuwa muswada kamili.
Ama nikushukuru kwa kunialika kuja humu kutoa hoja na kwa kuniamini kukaimu one time.
Shukrani kubwa kwa wote mlioshiriki na kutoa haja za fikra zenu. Tanzania ilipata uhuru pasipo kumwaga DAMU naamini itawezekana kabisa tena kwa amani chama kukabidhi hatamu za uongozi kwa chama mshindi.

Daima tuiweke Tanzania na WATANZANIA kwanza ndiposa tutaweza kujadili hali yetu na hatima yetu kama watu wamoja lakini wenye kupingana kifikra na si kimwili.

Idumu Tanzania
Sisi ni wapitaji tu
 
Mheshimiwa mwenyekiti nimenyoosha mkono muda mrefu nadhani hukuniona kwa sababu ya wingi wa wajumbe. Hata hivyo nilipenda kuchangia.

AGENDA KUU IWE KUBADILISHA KATIBA. Hii ifanywe kwa kushirikishwa wananchi wote, ikibidi sura kwa sura, ili wanaochaguliwa walazimike kulinda wakijua kuwa waliowaweka madarakani wanafahamu hilo.

Pia naunga mkono mawazo mengi +ve kwa maendeleo ya nchi yetu ya wajumbe waliotangulia
 
MkuuDopas
utuwieradhi skehke kwa kutokukuona.
ila dah sijui niseme kwa kuwa zogo limezidi na jopo linataka kwenda upenuni na kuzipanga hoja zetu ndo maana mwenyekiti alitaka kufunga kikao.
nakupa muda wa lala salama ujimwage

Kuhusu suala la katiba limechangiwa na wengi sana. kwa kuwa ni kilio cha wote naamini litapewa kipau mbele zaidi.
sasa ukimaliza nawaomba hawa hapo chini waseme chochote kabla pazia halijakunjwa.
Nguruvi3
rolemodel
 
Asante mwenyekiti kwa kunipa nafasi.

Agenda nyingine iwe 'kufanya 'usafi'-kuchukua hatua za kisheria

Maelezo
Kusafisha uozo wote uliopo ndani ya chama kuanzia na waliopo katika 'list of shame', ambao kwa namna moja ama nyingine wameliingizia Taifa hasara kubwa na kukwamisha maendeleo yetu kwa kiasi kikubwa.

Sambamba na hilo kuharakisha hukumu ya kesi zinazoendelea kiusanii, kama kiini macho za kina Mramba, Yona, Grey, na kuweka sheria ya kuwazuia kujiuhusisha na shughuli zozote na umma, hao na wote wenye tuhuma mbalimbali, ambazo ama zimedhihirika au la, ili uchunguzi uanze mara moja.

Ni vigumu kuendelea mbele ikiwa uchafu uliopo ndani ya chama "ng'atuka" haujaondolewa. Hilo litasaidia viongozi wetu wapya walazimike kulinda Katiba mpya na kutanguliza maslahi ya Taifa mbele.

Naomba kuwakilisha
 
Asante Dopas;

Majumuisho yote yanafanyiwa kazi na mara yakikamilika tutayapeprerusha hewani . . .
 
Asante Dopas;

Majumuisho yote yanafanyiwa kazi na mara yakikamilika tutayapeprerusha hewani . . .
Mwenyekiti wetu wa MHADHARA wa hadhara
tulipendekeza iwe wiki moja tupate majumuisho tuyaweke kwenye frontdoors zetu.
imepita wiki na zaidi.
Wadau wamenituma mkuu
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom