Mkutano wa CPA toka ndani ya AICC

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,466
113,548
Salaam,

Niko ndani ya ukumbi huu wa AICC unapofanyika mkutano wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola. CBA.

Kinachoendelea sasa ni wajumbe wameshakaa sehemu zao, unasubiriwa ujio wa Rais Kikwete kuja kufungua rasmi.
 
Last edited by a moderator:
Maandalizi yalikuwa kabambe sio shaghala baghala kama Sullivan. CBA jamaa wamejipanga vizuri. Usajili umefanyikia mahotelini wageni walikofikia hivyo hapa ukumbini ni kuingia tuu sio kama lile zogo la Sullivan usajili ukumbini.
 
Hali ya hewa huko nje ni vimanyunyu . Hapa ndani wajumbe wanapata burudani ya Brass Band ya polisi huku wakisindikizwa na filamu za vivutio mbalimbali vya utalii kwenye big screen mbili kubwa zilizomo ndani ya ukumbi.
 
Maandalizi yalikuwa kabambe sio shaghala baghala kama Sullivan. CBA jamaa wamejipanga vizuri. Usajili umefanyikia mahotelini wageni walikofikia hivyo hapa ukumbini ni kuingia tuu sio kama lile zogo la Sullivan usajili ukumbini.

Sulllivan iliboa kupita maelezo, naona hawa wamejitahidi sana,hata huku juu wanapoandaliwa kwa ajili ya chakula napo pamependeza sana, kwa ujumla jamaa wameiandaa vya kutosha.....nitaingia Simba hall mida mida.
 
Kama kawaida ya shughuli yoyote inayoandaliwa na waSwahili, Mswahili kamwe haachi asili yake. Lazima aingize uswahili japo kidogo. Ratiba inaonyesha mambo yanaanza saa tatu kamili. Mpaka saa nne na nusu kulikuwa hakuna taarifa yoyote ya kinacho endelea.

Ni saa nne na nusu ndipo MC akaibuka kuomba excuse ya JK kuchelewa. Kusema ukweli JK ni Mswahili tuu, hana excuse yoyote kuchelewa. Mkapa pamoja na maroroso yake, alikuwa serious. JK ni total lack of seriousness.
 
Na atachelewa sana kwa sababu ndege yake hata KIA haijatua na haijulikani itafika saa ngapi. si ajabu wakakaa humo ndani hadi jioni
 
nilikuwa nackia ngoma ngoma mfululizo nikajua mzee mzima ndio anaingia....kumbe holaaa!...
 
tunashukuru mkuu kwamba upo hapo ...embu tupe kinachoendelea sasa hivi. jee mkuu ameshaingia?
 
Naam,

Mwandishi nadhani kuna kipengele aidha kakiruka kwa makusudi ama hajui au hata ameandika na wachapishaji wakaona wakiweke kapuni.

Katika kundi la Sita basi kasahau kitu. Basi mimi nitaliita kundi la saba.

Kundi la saba na la ajabu ni la waganga wa kienyeji na wapiga ramli. Rais wetu ni mwafrika halisi kwa hiyo hajakumbatia kikweli kweli dini yoyote ya kigeni. Kwa hali hiyo, si vibaya nikisema, kwa uafrika wake ni mfuasi wa siri wa dini za jadi. Hili si tusi, dhambi wala dharau. Nimemshuhudia mwenyewe kwa mazungumzo ya ana kwa ana akihangaika na kulalamika juu ya mnyukano wa dini mbili kubwa hapa nchini (Uislamu na Ukiristo) na kweli haumpi raha hata kidogo.

Anajua jinsi dini hizi mbili zinavyotuhumiana juu ya maamuzi ya rais na serikali yanayozigusa dini hizi mbili. Wakiristo wanadai kwa wazi na sirini kuwa rais anawapendelea waislam wakati waislam nao wakidai wakiristo wanapendekelewa sana na serikali ya rais wetu. Matokeo yake ni rais kukosa msimamo na kubaki kulalamika na kutilia shaka kila ushauri anaopewa na watu watokao pande hizi mbili.

Kuna “uvumi” wa muda mrefu sasa kuwa rais wetu anapata faraja pale anaposhauriwa na waganga wa kienyeji kwa sababu anaamini hawana mgongano wa maslahi katika dini hizi mbili kuu! Kimantiki na kimsingi hii ni njia nzuri ya kutatua mnyukano wa dini kubwa pale unaposhauriwa na mtu wa tatu au wa katikati.

"Uvumi" huu umeendelea kueleza kuwa katika harakati za kuwasikiliza hawa waganga, rais amejikuta njia panda katika maamuzi mbalimbali. Ushauri wa waganga humfikia rais ama moja kwa moja au kupitia wapambe maalum, lakini utekelezaji wa ushauri huo huonekana kwa njia mbalimbali kama vile tabia sugu ya rais kuchelewa katika matukio mbalimbali na tabia ya rais kutoroka na kwenda sehemu huria kama michezoni. Mara kadhaa ndani na nje ya nchi, rais amekutwa katika maeneo yasiyo rasmi bila maandalizi wala kuwamo katika ratiba. Najua rais ana maisha binafsi lakini ni ruksa kuyahoji hasa yanapoonekana kuwa rasmi kwa kuwa yanatokea mara kwa mara.

Inasemekana kuwa kwa ushauri wa waganga rais pia amejikuta katika misiba, mazishi, kutembelea wagonjwa nyumbani na hospitali, sherehe za harusi, na hafla za asasi za kiraia zenye utata. Imesikika pia waganga hawa ndiyo wanaosikilizwa hata katika masuala ya afya yake kuliko hata madaktari wa ndani na nje ya nchi.

Eneo hili limejaa “uvumi”, umbeya na maneno ya mitaani yanayochangamsha mabaraza na vijiwe, lakini cha msingi na kinachogomba ni pale yanayosemwa yanapofanana na yanayosemwa. Ikiwa uvumi huu au sehemu yake ina ukweli, basi kundi hili ndilo pekee linalomshauri mheshimiwa rais katika mambo mengi na kwa hiyo ndilo limeshikiliwa mustakabali wa taifa letu kwa sasa.

Katika mazingira ambamo makundi mengine yamenyamazishwa, salama yetu iko wapi tunapokuwa mikononi mwa hawa washauri ambao ushauri wao haujapimwa na chombo chochote kinachojulikana?

Pimbi

Kama kawaida ya shughuli yoyote inayoandaliwa na waSwahili, Mswahili kamwe haachi asili yake. Lazima aingize uswahili japo kidogo. Ratiba inaonyesha mambo yanaanza saa tatu kamili. Mpaka saa nne na nusu kulikuwa hakuna taarifa yoyote ya kinacho endelea.

Ni saa nne na nusu ndipo MC akaibuka kuomba excuse ya JK kuchelewa. Kusema ukweli JK ni Mswahili tuu, hana excuse yoyote kuchelewa. Mkapa pamoja na maroroso yake, alikuwa serious. JK ni total lack of seriousness.

Na atachelewa sana kwa sababu ndege yake hata KIA haijatua na haijulikani itafika saa ngapi. si ajabu wakakaa humo ndani hadi jioni
Nawaza, kisha nawaza na kisha nawaza....
 
JK ndio anaingia sasa saa hizi saa 5: 10 Watu wanasimam nyimbo ya taifa inimbwa. Wenye ukumbi wao wamewasha mtambo wa kuzuia mawasiliano. Naombeni samahani,wanajamvi wenye accses na ITV naomba muendeleze update.
 
Back
Top Bottom